image

Kitabu Cha Afya

Kitabu Cha Afya

Kitabu cha Afya

By Rajabu Athuman

KITABU CHA AFYA


MAANA YA AFYA
Afya ni hali ya kuwa mzima kimwili na kiakili. Kuna mahusiano makubwa kati ya kuwa mzima kimwili na akili. Mtu anaweza kuwa mwili upo mzima kabisa lakini akaambiwa hana afya salama kwa maana anaweza kuwa akili yake haipo vizuri. Kuathirika kiakili pia ni ugonjwa na ndio maana kuna wagonjwa wa sikolojia.


Hivyo mtu mwenye afyqa ni yule a,baye ni mzima wa mwili na akili. Na tunaposema akili haimaanishwi mgonjwa wa akili ni yule mkichaa hapa na bali hata ambaye saikolojia yake haipo vizuri nae ni mgonjwa.


Ndani ya mwili wa binadamu kuna mifumo ambayo hiyo kazi yake ni kuhakikisha kuwa mwili haudhuriki kimwili na kiakili. Mifumo hii ipo kazini muda wowotw kupambana na mamilioni ya wadudu hatari waliopo kwenye mazingira yetu. Kwa mfano kwenye hewa kuna mabilioni ya wadudu kama bakteria ambao huambukiza maradhi.


Mwili unaweza kuthibiti maradhi kupitia njia zake nyingi kwa mfano;- katika mfumo wa damu kuna seli hai nyeupe za damu hizi zinapambana na vijidudu vya maradhi. Halikadhalika mna katika damu antibodies hizi zinafanya kazi hii pia. Kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kuna asidi ambazo zinakazi ya kuuwa bakteria na vijidudu vingine vya maradhi. Kwenye mfumo wa upumuaji kuna uttelezi na vijinywele ambavyo hukamata vijidudu pamoja na mavumbi na kutolewa nje.


Hivyo mwili una mfumo madhubuti kabisa wa kuweza kupambana na maradhi. Na ikitokea umepambana na kushindwa hapo hutokea mtu akaumwa. Pia ijulikane kuwa kinga za mwili zinaweza kutengenezwa na mwili wenyewe au kuzipata kwa kutumia chanjo. Mwili huanza kutengeneza kinga hizi hata kabla ya kuzaliwa kwa mtoto na hivyo hivyo mwili huendelea kuzitengeneza kinga hizi wakati wa kukua na kuendelea kwa maisha baada ya kuzaliwa.


Pia wakati mwingine mapambano yanapokuwa makali ndani ya mwili huweza kutokea maumivu katika sehemu za mwili. Kwamfano mfumo wa lymph unapopambana vikali huweza kusababisha maumivu ya mtoki.


NYANJA SITA ZA AFYA
Kama tulivyosema hapo juu kuwa afya ni kuwa mzima kimwili na kiakili. Hata hivyo nadharia ya afya haiishii hapa ila inaendelea hata kujengwa katika mambo makuu sita. Mambo haya wataalamu wa afya wanayaita components of health. Mambo haya nitayataja hapa chini kwa ufupi tuu kama ifuatavyo


1.afya ya kimwili (physical health); hapa ni kuwa mzima kimwili, na afya hii huweza kujenga kwa kula vizuri, kufanya mazoezi ya mara kwa mara, kuepuka unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara na matumizi ya madawa ya kulevya. Ukifanya hivi unaweza kuboresha mwili wako na kuboresha afya ya kimwili.


2.afya ya kiakili (mental health); hapa tunaangalia kuwa salama kiakili. Mtu akiwa na afya salama ya kiakili anakuwa na uwezo wa kujiamini, anapenda kujifunza vitu vivya na anavifurahia. Mtu mwenye hali hizi tunasema ana afya ya kiakili. Uwoga wa kuogopa watu ni katika maradhi ya kiakili.


3.afya ya mawazo na hisia (emotional health); hapa mtu anauwezo wa kuelezea hisia zake na mawazo yake. Kama kuna jambo limemuudhi analisema. Matu mwenye afya hii anauwezo wa kutaka msaada kwa mtu mwingine bia ya wasi.


4.Afya ya kiroho (spiritual health); hii ni afya inayojengwa na kuwa na imani juu ya mambo fulani. Na mara nyingi hapa tunazungumzia kuwa na imani juu ya dini. Watalamu wa afya wanaonesha mahusiano makubwa kati ya dini na mtu. Wataalamu wanatuambia zaidi matu mwenye imani ya kuna uwezekano mdogo wa kupata maradhi ya moyo kuliko mtu asiye na imani ya dini.


5.afya ya kijamii (social health); hii ni afya inayojengwa na kuwa na mahusiano mazuri na jamii. Kusaidia watu, kuitikia watu wanapokuita na kucheka nao na kuzungumza nao ni katika mambo yanayojenga afya hii. Wataalamu wa saikolojia wanatueleza mengi kuhusu afya hii.


6.afya ya mazingira (environmental health); hii afya hujengwa na mazingira yanayotuzunguka. Mtu awe na uwezo wa kupata hea safi na maji safi. Hivi hujenga afya hii. Mazingira kuwa safi na salama huweza kutengeneza afyahii.


YANAYOATHIRI AFYA
Afya yamtu inaweza kuathiriwa kuwa njema au kuwa mbovu kwa kuzingatia mambo kadhaa wakadhaa. Hapa nimechagua mambo makuu matano ambayo nitakwenda kuyaangalia ambayo ni;-
A).vyakula
B)Mazingira
C)Shughuli za kila siku
D)Tabia na mazoea
E)Vizazi, familia ama kurithi.


1.VYAKULA
Vyakula ni katika sababu kubwa ambazo husaidia kwa kiwango kikubwa kuathiri afya za watu. Wataalamu wa afya leo wanaeleza na kutaja magonjwa mengi sana ambayoyo yanapatikana kwa kupitia vyakula. Pia yapo magonjwa ambayo huambukizwa kwa kupitia ulaji wa chakula. Hivyo magonjwa mengi na hatari zaidi yamekuwa na mahusiano na vyakula vyetu. Chakula kinaweza kuwa msaada kwako au kuwa ni chanzo cha matatizo ya afya yako. Mfano mzuri ni kuwa leo wataalamu wa afya anaeleza kuwa mamilioni ya watu wanakufa kwa ugonjwa wa saratani kila mwaka. Tafiti zinaonesha kuwa miongoni mwa sababu za ugonjwa huu ni vyakula. Vyakula ambavyo tunavila leo sio rafiki kwa afya zetu. Tumekuwa tukila vyakula ambavyo vimejaa kemikali nyingi na matatizo kadha wakadha.


Mfano wa pili ni ugonjwa wa kisukari, huu ugonjwa umekuwa ukienea kwa kasi sana duniani leo. Kuanzia watoto, vijana wazee na wajawazito wote wapo hatarini kuapata maradhi haya. Wataalamu wa afya wanataja kuwa vyakula ni katika sababu mjawapo ya kupata maradhi haya. Kuongezeka kwa uzito nje ya uzito wa kawaidi ni katika sababu za kutokea kwa kisukari. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa vyakula ni sababu ya kuongezeka kwa uzito mwilini na kutofanya mazoezi ijapokuwa zipo sababu zingine.


Magonjwa ya moyo kama shinikizo la damu (presha) pamoja na shambulio la moyo (heart attack) ni katika magonjwa yanayowapata watu weng duniani na kusababisha vifo vingi sana. Wataalamu wa afya wanaeleza katika sababu kubwa za kutokea kwa maradhi haya ni vyakula. Hususan vyakula vyenye mchanganyiko mkubwa wa mafuta ya viwandani.


Maradhi ya utapiamlo kama matege, baadhi ya matatizo ya macho, unyafuzi na kwashiakoo pamoja na kudumaa ni katika maradhi ambayo husababishwa na vyakula. Majeraha kutokupona haraka, kuchelewa kupona kwa vidonda na makovu, ngozi kupasuka na kutokwa na vidonda kwenye mdomo ni katika baadhi ya matatizo yanayosababishwa na vyakula


Kwa ufupi ni kuwa vyakula ni katika sababu kubwa sana ya maradhia mabayo tuanayapata. Tutazungumzia kwa undani zaidi somo hili kwenye kurasa zijazo na tutaona kwa undani vipi vyakula vinaweza kusababisha yote hayo.


2.MAZINGIA
Mazingira yamekuwa leo ni sababu ya kupata maradhi mengi sana. Maradhi mengi yanayotupata kutokana na mazingira yetu yanaweza kusababishwa na uchafu wa mazingira. Ijapokuwa mazingira yanaweza kuwa safi na pia yakasababisha maradhi. Mazingira pia yanaweza kuwa msaada kwetu kwa kuweza kulinda na kuimarisha afya zetu. Ila kwa ufupi hapa tutazungumzia tuu mazingira yanavyoathizi afya zetu kuwa dhoofu.


Mfano mzuri ni maradhi ya malaria ambayo leo yamekuwa yakipelekea mamilioni ya vifo duniani hususani watoto waliopo chini ya umri wa miaka mitano. Malaria yanaenezwa na mbu aina ya anofelesi na mbu huyu ni jike. Mbu hawa wanazaliana sehemu zenye majimaji. Mbu hawa hawahitaji maji mengi sana, hapana hata tone moja linamtosha yeye kutaga na kutoa watoto. Mbu hawa wamekuwa wakipatikana kwenye mazingira yetu. Wataalamu wa afya wanaeleza usafi wa mazingira kama kufyeka nyasi na kufukia madimbwi ni katika njia za kupambana na maradhi haya.


Mfano mwingine ni m aradhi ya kipindupindu, haya yamekuwa yakisababishwa na bakteria ambao wanaingia mwilini kwa njia ya chakula. Mazingira yanaweza kuwa njia ya kuenezxa maradhi haya kama usafi wa mazingira hautazingatiwa. Nzi wanaweza kubeba vijidudu vya maradhi na kuvipeleka kwingine katika mazingira yasiyokuwa safi.


Maradhi ya mafua yamekuwa ji kawaida sana kwa nchi zilizopo kwenye tropic. Maradhi yaya yanaweza kupatikana sana kwenye mazingira yenye vumbi sana. Pia kupitia hewa kutoka mgonjwa kwenda mtu mzima. Hivyo tunaweza sema mafua yanaenezwa sana kwenye mazingira kupitia hewa.


Wataalamu wa afya wanaeleza maradhi mengi sana ambayo hupatikana kwenye mazingira yetu yakila siku. Mazingira haya yanaweza kuwa kwenye maji kama maradh ya kichocho, kwenye hewa kama kifua kikuu na mafua au mazingira ya chini kama vile maradhi ya kipindupindu.


3.SHUGHULI ZA KILA SIKU
HAlikadhalika shughuli zetu za kila siku zinaweza kuwa sababu mojawapo ya kupata maradhi mablimbali za kutafutia riziki zinaweza kuwa sababu tosha ya kupata maradhi. Wataalamu wanaeleza maradhi kazaa ambayo yanaweza kuwa chanzo chake ni shughuli zetu za kila siku.


Vifaa vya kufanyia kazi kama visipotumika ipasavyo kwa mfano kuvaa viatu maalumu na nguo maalumi kwa ambao wanafanya kazi viwanda vya kemikali, wanaweza kupata madhara. Wafanyaji kazi sehemu zenye mionzi hatari kama x-ray wasipovaa mavazi maalumu kwa utaratibu husikwa wanaweza kuapata madhara.


Muda wa kufanya kazi usipizingatiwa pia madhara yanaweza kuapatikana. Kwa mfano sehemu zenye mionzi mikali kama x-ray kuna muda maalumu wa kufanya kazi na ukipita anatakiwa aingie mtu mpya. Hivyo jkazi kama hizi muda usipizingatiwa madhara ya kiafya yanaweza kutokea.


Halikadhalika teknolojia inayotumika kufanyika kazi kama haitakuwa katika hali nzuri inaweza kusababisha madhara. Vifaa vya kisasa vinatakiwa vitumike zaidi kwa ajili ya usalama kuliko kuendelea na vile vya zamani vinavyohitaji nguvu nyingi na kufanya kazi mazingira ya hatari.


Hivyo shughuli zetu za kufanyia kazi zsipowekwa katika hali nzuri zinaweza kuwa ni sababu ya sisi kuapata madhara makubwa kama kupiteza mali, kupoteza uhai au kupoteza viungo vya miili yetu. Somo hili tutaliona kwa undani zaidi kwnye kurasa zijazo.


4.TABIA
Tabia za watu pia zinaeza kuwa ni sababu ya kupata maradhi na kuathiri afya. Watu wamekuwa wakikulia katika koo, familia na kabila mbalibali ambapo wanajifunza tabia tofautitofauti. Tabia hizi kama hazitakuwa katika hali inayotakiwa zinaweaa kusababisga kupata maradhi


Nitoe mfano mzuri kuhusu maradhi ya fangasi sehemu za siri. Fangasi hawa wanafurahia sana mazigira yenye majimaji. Mara nyingi usafi wa nguo za ndani na mwili kwa ujumla hususan sehemu zile umaweza kuwa sababu ya kuendelea kuwalea wadudu hawa. Tabia ya kuvaa nguo mbichi hususani zile za ndni inaweza kuendelea kuwalea fangasi hawa.


Tabia ya kula mara kwa mara inaweza kusababisha kupata kitambi. Mtu akiwa anakula mara kwa mara bila ya kufanya mazoezi anaweza kupata tatizo la kuzidi kwa uzito. Tatizo hili linaweza kuathiri mwili kushindwa kuzalisha homoni za insulin kwa kiwango kinachotakiwa na hatimaye kupata kisukari.


Tabia ya kuchelewa kualal yaani kukosa muda mzuri wa kulala inaweza kuwa sababu ya kupata matatizo ya kiafya. Mwili unahitaji muda wa kutosha wa kulala ili uweze kurekebisha mwili ndani ya muda huo. Mwili unahitaji kupumzika pia.


Tabia ya kukaana misongo ya mawazo na kupenda kukasirika na kukaa na vinyongo. Hii ni hatari sana ka afya ya mtu kisaikolojia na kimwili pia. Misongo ya mawazo inaweza kuwa sababu nzuri ya kupata maradhi kama vidonda ya tumbo. Maumivu ya kichwa na tumbo pia huweza kuletwa na misongo ya mawazo


5.VIZAZI, FAMILIA NA KURIDHI (GENETICS)
Afya ya mtu inaweza kuathiriwa na kurithi kutoka kwa wazazi. Hapa mtu hana chaguo maana kurithi huku kumetokea toka tumboni kwa mama. Mtu anaweza kurithi maradhi kama pumu, moyo, kisukari, siko seli na mengineyo.


Kwa ufupi hivi vipengele vinavyoathiri afya tutaviona kwa undani zaidi kwenye kurasa zijazo. Hapo tumeona tuu juu juu namna ya mabo yalivo. Sasa hebu tuone vitu tutaweza kuboresha afya zetu.


KUBORESHA AFYA
1.TAHADHARI KWENYE VYAKULA
Ukiweza kuchukuwa tahadhari kwenye vyakula na kujua chakula salama cha kukila kulingana na mahitaji ya mwili hapa unaweza kufanikiwa kuulinda mwili wako na maradhi mengi sana. Uwe na elimu sahihi ya vyakula na faida zake kwenye mwili. Kwani unaweza kukusanya vyakula vingi kumbe ni sawa na kual chakula kimoja


Vyakula vya protini ni m uhimu katika ukuaji wa watoto na ukuaji wa tishu. Vyakula hivi huhusika katika kuurekebisha mwili na ni muhimu hsana katika kuhakikisha afya ya mtu ipo kwenye msitari mzuri. Kwa ufupi tunasema kuwa vyakula vya protini ni vyakula vya kujenga mwili. Unaweza kupata protini kwenye maziwa, samaki, nyama, maini, maharage na mayai. Upungufu wowote wa vyakula hivi unaweza kuleta mdahara makubwa kama tulivyoona hapo juu.


Vyakula vya wanga ni mujarabu sana kwa ajili ya kuupa mwili nguvu. Tumia vyakula hivi hasa kama unafanya kazi za nguvu. Vyakula hivi pia ni muhimu kwa ajili ya kuhakikisha kuwa m ifumo ndani ya mwili inafanya kazi kwa usahihi. Kwa mfano mfumo wa upumuaji na uunguzwaji wa chakula (espiration) unahitajia vyakula hivi kwa ajili ya kuzalisha nguvu ya kutosha ndani ya mwili. Vyakula hivi vinaweza kupatikana kwenye nafaka kama mahindi, ngano na mchele.


Vyakula vya madini, Mwili unahitaji vyakula hivi ili uwezesj\he matumizi ya vyakula vingine yawe mazuri tunahitaji viyamini kwa kuulinda mwili dhidi ya magonkwa. Vitamin c hujulikana kwa kusaidia ugonjwa wa scuvy ugonjwa huu humfanya mtu atoke samu mwenue mafinzi. Vitamin A husaidia kurekebisha afya ya macho. Vitamin K husaidia kuganda kwa damu unapopata jeraha. Mwili unahitaji madini pia ili uweze kujikinga na hatari zingine. Madini ya chuma ni muhimu katika kujenga seli nyekundu za damu.madini ya calcium ni muhimu kwa afya ya mifupa na meno. Madini na vitamin hpatikana zaidi kwenye mboga za majani, na matunda. Matunda yenye uchachu kama limao, chungwa husaidia kwa vitamin C na mapapai pi hujulukana kwa kuwa na vitamin C. spinachi ni muhimu kwa vitamin A. samaki husaidia kwa madini mengine.


Vitamin ni muhimu katika kuhakikisha kuwa mwili unatumia virutubisho vingine kufanya kazi zake. Kuna vitamin A,B,C,D,E na K. vitamin B vimegawanyika katika makundi kama vitamin B1,B2,B6, na B12. Ukosefu wa vitamin vyovyote kati ya hivi unaweza ukapelekea matatizo makubwa kwa afya ya mtu. Vitamin A,D,E na K, vinaitwa fat soluble vitamin. Hivi nhuweza kuhifadhiwa ndani ya mwili. Hivyo hatuhitaji kula vyakula kuvipata kwa kila siku. Kwa upande mwengingine vitamin B na C huitwa water soluble vitamin, hivi havihifadhiwi ndani ya mwili, hivyo tunahitaji kula vyakula vyenye vitamin hivi kwa kila siku. Hivyo mtu awe na tahadhari zaidi juu ya kupangilia vyakula vyake. Tuatona zaidi aina hizi na madhara yake kwenye kurasa zijazo.


Unywaji wa maji ni jambo linalolazimishwa sana. Kwama mtu hana sababu yeyote anatakiwa anywe maji mengi zaidi. Wataalamu wa afya wanashauri angalau kwa siku mtu anywe maji bilauri (glass) nane kwa kiwango cha chini. Mwili wa kiumbe hai asilimia 50-90 ni maji. Hivyo maji yakipungua mwilini kunaweza kutokea madhara makubwa zaidi. Maji huhitajika karibia katika mifumo yote mwilini. Maji hutumika katika kurekebisha afya ya mtu.


2.TAHADHARI KWENYE MAZINGIRA
Kama tulivyoona hapo juu, mazingira yetu ni sababu tosha ya kuathiri ubora wa afya zetu. Hivyo mtu ahakikishe sikuzote anaishi katika mazingira salama na safi. Wataalamu wa afya wanatueleza kusafisha mazingira yetu ya ilasiku ili tuweze kukabilia na na wadudu hatara.


Hakikisha hewa unayoipata ni safi na salama. Futa mavumbi ndani ya nyumba na nguo za kujifunika ziwe safi, kwa namna hii ni rahisi kukabilia na na mafua. Epuka moshi kutoka viwandani, pia usilale ukiwa na jiko la mkaa linalowaka na ikawa madirisha na milango umefunga. Unaweza kupata tatizo la kukosa oxkyjeni na kufariki dunia. Kaa mbali na wavuta sigara kwani hewa yao inaweza kukuathiri na wewe pia. Jambo la msingi hapa ni kuchukua tahadhari dhidi ya hewa ambayo tunaipata kwenye mazingira hetu.


Hakikisha unafyeka na kupunguza nyasi zilizo karibu na wewe. Fukia madimbwi na majimaji yoyote yalotuwama hata kama yapo kwenye kifuniko cha soda kwani hayo ni machache lakini mamia ya mbu yanaweza kuzaliana hapo. Mashimo ya kutupia taka yawe mbali kidogo na nyumba na kuwepo utaratibu wa kuchoma moto mashimo hayo bada ya muda. Usafi wa mazingira unaweza kuwa njia tosha ya kuanza harakati za kukabiliana na malaria na kipindupindu.


Watu wahakikishe wanakunywa maji safi na salama pamoja na kula vyakula ambavyo vimehifadhiwa kwa usalama. Usafi wa maji unaweza kuwa njia ya kupambana na typhod (taifodi) na maradhi mengine ya tumbo. Kuwepo na utaratibu wa kuyatibu maji kama yamepatikana sehemu ambazo sio salama na safi. Maji yanaweza kutibiwa kwa njia za kisasa kama kuweka madawa. Lakini pia unaweza kutumia njia ya kuyachemsha na kuyachuja na kuyatumia.


Sikuzote hakikisha unaishi katika mazingira rafiki na afya yako. Watu ambao tayari wanamaambukizi ya maradhi maalumu wanatakiwa waishi katika mazingira ambayo ni rafiki na hali zao.


TAHADHARI KWENYE SHUGHULI ZETU
Kama tulivyotangulia kuona hapo juu kuwa shughuli za kuwapatia watu rizikinazo zinaweza kuwa chanzo cha maradhi. Hivyo tahadhari maalumu zinatakiwa zitumike ili kuweza kujiepusha na madhara ambayo yangeweza kuthibitiwa. Kwa mfano uaweza kujikinga na baadhi ya adhari kwa kuvaa mavazi maalimu kama gkovs, gunboot makoti maalumu kulingana na kazi husika. Soma vizuri nembo za tahadhari unapofungua kifaa cha kufanyia kazi. Tahadhari zaidi zinategemeana na kazi yenyewe na sehemu husika.


TAHADHARI NA TABIA ZETU
Usafi w mwili ni katika tabia njema na ni rafikipia. Kuufanya mwili iwe na uwezo wa kujikinga. Usafi wa nguo ni njia tosha ya kupambana na maambukizo na maradhi mengineyo kama tulivyotoa mfano huko juu. Mtu anatakiwa kujenga tabia rafikia na afya kama kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi angalau mara tatu kwa wiki. Kutokuwa na abia ya kupenda vyakula vyenye chumvi nyingi hii huweza kumuepushha mtu na athari za kupata maradhi ya moyo kama presha na shambulio la moyo. Kupiga mswaki zaidi ya mara moja kwa siku na ukishindwa basi angalamu unapoamka na unapokwenda kulala. Tabia za kiafya zinaweza kujengwa kwenye vyakula, mazoezi, matendo na mazungumzo pia.


TAHADHARI JUU YA MARADHI YA KURITHI
Ni vigumu sana kujitahadhari kutopata maradhi haya kama kuwa albino. Ila inawezekana wazazi kulinda familia zao na maradhi ya kurithi ila pia ni ngumu. Kwani it itajika kupima kati ya wanandoa wawili kabla ya kupata watoto. Hapa ndio itaweza kugundulika maradhi haya ya kurithi kama yapo kwa wazazi na je upo uwezekano wa kuendelea kwa watoto. Kwa teknolojia iliyorahaisi kwa sasa ni kumlinda mtoto atakayezaliwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Ijapokuwa yapo matatizo mengine ya kurithi anaweza kukingwa mtoto akiwa tumboni asijedhurika. Tutaona zaidi matatizo haya kwenye kurasa zijazo.


AFYA NA LISHE.
Hapa tutaona zaidi mahusiano yaliyopo katika afya na vyakula ambavyo tunakula. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa vyakula tunavyokula hujulisha namna tulivyo kimwili na kiakili. Ijapokuwa uwezo wa akili hueza kusababishwa na kurithi kutoka kwa wazazi lakini vyakula pia vina nafasi kubwa katika hili. Kwa mfano ulaji wa samaki husaidia katika maendeleo ya ubongo na ukuaji salama wa kiakili hasa kwa watoto. Hapa tutaangalia zaidi aina za vyakula na atharizake kama visipopatikana kwa kiwango kinachotakiwa mwilini.


1.AINA ZA VYAKULA
1.VYAKULA VYA PROTINI
Hivi ni vyakula ambavyo vinakazi ya kuujenga mwili pamoja na kuukarabati mwili. Kupona kwa vidonda na makovu vyote ni kazi ya protini. Uotaji wa nywele mpya pamoja na kukuwa kwa kucha baada ya kuzikata vyoye hivi hufanyika shukrani kwa vyakula vya protini.


Unaweza kuvipata vyakula vya protini kutokana na maziwa, nyama, mayai, na samaki. Katika mimea pia unaweza kupata protini kwa kula maharage, mchele na baadhi ya nafaka zingine. Pia ulaji wa mboga za majani unaweza kusaidia kupatikana kwa protini. .


2.VYAKULA VYA FATI NA MAFUTA
Vyakula vya fati husaidia katika kuupa mwili nguvu. Fat husaidia kulinda seli zilizomo mwilini zisizurike. Vyakula hivi huupa mwili joto hususan wakati wa baridi. Na inashauriwa wakati wa baridi kula vyakula vya fat kwa wingi ili kuupa mwili joto. Vyakula vya fat pia husaidia kuganda kwa damu pindi mtu anapopata jeraha.


Vyakula vya fati ni maziwa, mafuta ya wanyama, mayai na nyama. Pia katika matunda fat inapatikana kwa wingi pia kwa mfano katika avocardo, olive, karanga , alizeyi pamoja na mafuta ya mimea yaani vegetable oil. Samaki ni chanzo kizuri cha fat. . .


3.VYAKULA VYA WANGA
Vyakula vya wanga ndio vyanzo vikuu vya nguvu ndani ya mwili. Vyakula hivi hupatikana kwenye starch. Mwili unatumia vyakula vya wanga katika hali ya glucose. Ambayo huenda maeneo mengine ya mwili kwa ajili ya kuzalisha energy.


Unawza kupata wanga kwa kula nafaka kama maharage, matama, mihogo. Pia asali, miwa na viazi ni vyanzo vizuri vya wanga. inashauriwa kwa watu wanaofanya kazi ngumu zinazohitaji nguvu kubwa wale vyakula hivi.


4.VYAKULA VYA MADINI
Mwili unahitaji vyakula hivi ili uwezesj\he matumizi ya vyakula vingine yawe mazuri tunahitaji viyamini kwa kuulinda mwili dhidi ya magonkwa. Mwili unahitaji madini pia ili uweze kujikinga na hatari zingine. Madini ya chuma ni muhimu katika kujenga seli nyekundu za damu.madini ya calcium ni muhimu kwa afya ya mifupa na meno Madini na vitamin hpatikana zaidi kwenye mboga za majani, na matunda.


1.Madini ya sodium (table salt) Madini haya unaweza kuyapata kwenye spinach, maharage,punje za maboga n.k.


2.Madini ya chuma. Haya hupatikana kwenye maini, nyama, maharage, na mboga za majani. Madini haya ni muhimu kwa utengenezwaji wa hemoglobin yaani chembechembe nyekundu za damu.


3.Madini ya kashiam(calcium). Haya hupatikana kwenye maziwa,maini, mboga za majani na cheese. Madini haya husaidia katika uimarishwaji wa mifupa, meno, misuli na utengenezwaji wa neva. Husaidia piaa kuwezesha kuganda kwa damu kwenye majeraha. Husaidia katika mfumo wa mmeng�enyo wa chakula kwa kuzifanya enzymes kuwa active.


4.Madini ya phosphorus, haya hupatikana kwenye nyama, maziwa, samaki, na mayai. Husaidia katika uimarishwaji wa mifupa, meno,misuli na shughuli za mfumo wa fahamu na utengenezwajiwa genetic materials.


6.Madini ya Potashiam (potassium) Hupatikana kwenye ndizi, machungwa,nyama na kaa. husaidia katika kurekebisha kiwango cha majimaji mwilini.


7.Madini yakopa ( copper) Haya hupatikana kwenye nyama, samaki, na maini.husaidia katika mifupa na utengenezwaji wa hemoglobin (chembechembe nyekundu za damu).


8.Madini yamanganese Madini haya hupatikana kwenye figo,maini, chai na kahawa. Husaidia katika utengenezwaji wa mifupa, na katika mmeng'enyo wa chakula kwa kufanya enzymes ziwe active.


9.Madini ya iodine Madini haya hupatikana kwenye chumvi na vyakula vya baharini kama samaki. Husaidia katika uzalishaji wa homoni ya thyroid.


5.VYAKULA VYA VITAMINI
Vitamin ni muhimu katika kuhakikisha kuwa mwili unatumia virutubisho vingine kufanya kazi zake. Kuna vitamin A,B,C,D,E na K. vitamin B vimegawanyika katika makundi kama vitamin B1,B2,B6, na B12. Ukosefu wa vitamin vyovyote kati ya hivi unaweza ukapelekea matatizo makubwa kwa afya ya mtu.


Vitamin A,D,E na K, vinaitwa fat soluble vitamin. Hivi nhuweza kuhifadhiwa ndani ya mwili. Hivyo hatuhitaji kula vyakula kuvipata kwa kila siku. Kwa upande mwengingine vitamin B na C huitwa water soluble vitamin, hivi havihifadhiwi ndani ya mwili, hivyo tunahitaji kula vyakula vyenye vitamin hivi kwa kila siku.


Vitamin A hupatikana kwenye maziwa, maini, karoti,machungwa, na mboga za rangi nya njano.. Vitamin B1 hivi hupatikana kwenye nyama, maini, mayai,hamira na mchele. Vitamin B2 hivi hupatikana kwenye nyama, maini, nafaka na hamira. Vitamin B3 hupatikana kwenye samaki, karanga,nyama, mchele usio kobolewa na hamira.. Vitamin B12 hivi hupatikana kwenye samaki,nyama, mayai,maziwa na maini.


Vitamin C hivi hupatikana kwenye matunda yenye uchachu kama limao na machungwa. Mboga za kijani,na nyanya. Vitamin D hupatikana kwenye mayai, maziwa, samaki na maini. Mitamini E hupatikana kwenye alizeti, butter, mchele na peanuts. Vitamin K hupatikana kwnye maini na mboga za majani.


Mtu atapata matatizo pia kama hata kunywa maji ya kutosha kwa siku. Maumivu ya kishwa huweza kusababishwa na kutokunywa maji ya kutosha. Choo kuwa kigumu huweza kusababishwa na uchache wa kunywa maji.


6.MAJI
Zaidi ya 70% ya mwili wa binadamu ni maji. Tunahiyaji maji ili tuweze kuishi. Mmaji ni muhimu kwa afya. Mtu anahitaji kunywa maji bilauri 8 mpaka 10 za maji. Mtu anaweza kuishi siku ziaizopungua 8bila kunya maji lakini anaweza siku nyingi zaidi bila ya kutokula chakula.


Maji husaidia kurekebisha mifumo mbalimbali ndani ya mwili kama vile mfumo wa utoaji takamwili, mfumo wa chakula na mfumo wa damu. Maji husaidia katika kutibu maumivu ya kichwa amabayo yamesababishwa na unywaji mchache wa maji.


7.ROGHAGE (vyakula vyenye asili ya kambakamba)
Hii si katika aina vya virutubisho. Hivi ni vyakula ambavyo husaidia katika msukumo wa chakula tumboni. Husaidia katika kufanya haja kubwa itoke kwa usalama. Matatizo ya kuziba kwa choo au kupata hajakubwa kwa kiasi kidogo husababishwa na kutokula vyakula vyenye hali hii kwa kiwango kinacho hitajika.


Tunaweza kupata roughage kwenye nafaka zote zisizo kobolewa, matunda, maharage, kabichi spinach, mihogo na nyanya zisizo menywa na jamii zingine za vyakula hivi.


2.UPUNGUFU WA VYAKULA HIVI NA MADHARA YAKE.
Kama tulivyosema huko awali kuwa upungufu wa chochote katika vyakula hivi unaweza kuleta madhara zaidi. Halikadhalika kuzidi kwa baadhi ya virutubisho mwilini kunaweza kusababisha madhara. Kwa mfano madini ya chumvi yakizidi zaidi mwilini yanaweza kusababisha presha ya kushuka. Halikadhalika madini ya chuma yakizidi pia ni hatari. Mwili unahitaji virutubisho hivi kwa kiwango maalumu. Na mwili wenyewe unafanya kazi hii ya kuchukua kiwango unachohitaji na kinachozidi kinatoka kwa njia ya haja kubwa au ndogo. Sasa hebu tuone kwa ufupi vyakula hivi vinaleta adhari gani pindi virutubisho vikipungua.


1.UPUNGUFU WA VYAKULA VYA MADINI
1.Madini ya sodium (table salt) Upungufu wa madini haya utapelekea udhaifu wa misuli na udhaifu wa mifupa. Pia mapigo ya moyo kutokuenda vizuri husababishwa na upungufu wa madini haya.


2.Madini ya chuma. Upungufu wa madini haya hupelekea matatizo katika mfumo wa damu. Ugonjwa wa anaemia unamahusiano ya moja kwa moja na upungufu wa madini ya chuma. Madini ya zink, hupatikana kwenye kamba, kaa, nyama na hamira. Husaidia pia katika afya njemaya mfumo wa kinga (immune system) na uponaji wa majeraha.


3.Madini ya kashiam(calcium). Madini haya yakipunguwa mwilini mifupa na meno huwa na udhaifu. Halikadhalika damu hutoka kwa muda mrefu baada ya jeraha kabla ya kuganda.


4.Madini ya phosphorus,Husaidia katika uimarishwaji wa mifupa, meno,misuli na shughuli za mfumo wa fahamu na utengenezwajiwa genetic materials.


5.Madini ya Potashiam (potassium) husaidia katika kurekebisha kiwango cha majimaji mwilini. Upungufu wa madini haya unaweza kupelekea matatizo katika misuli.


6.Madini yakopa ( copper) Upungufu wa madini haya unaweza ukapelekea urahisi katika kupasuka kwa mishipa ya damu, matatizo mkatika mifupa na viungio (joints).


7.Madini ya manganese Upungufu wa madini haya unaweza ukapelekea kupoteza kwa joto mwilini, mifupa kuwa nyepesi, kutokwa na damu za pua na kupata kizunguzungu.


8.Madini ya iodine Husaidia katika uzalishaji wa homoni ya thyroid. Ugonjwa wa goita (goiter) husababishwa na upungufu wa madini haya.


2.UPUNGUFU WA VITAMINI
1.Upungufu wa vitamini A hupelekea kukauka kwa ngozi, uoni hafifu na kuathirika kwa koo na ngozi


2.Upungufu wa vitamin B1 hupelekea kukosa hamu ya kula, udhaifu wa miguu, kupungua kwa hisia kwenye neva kudhoofu kwa misuli na kuathirika kwa akili.


3.Upungufu wa Vitamin B2 hupelekea kupata ugonjwa wa pellagra yaani vidonda vya mdomo na ulimi, ukuaji hafifu, kupasuka kwa nbgozi hasa sehemu za sikio na pua.


4.Upungufu wa Vitamin B12 husababisha matatizo katika uzalishaji wa seli hai nyekundu za damu. Na kusababisha aina ya ugonjwa wa anaemia


5.Upungufu wa vitamini C husababisha kutoka damu kwenye mafinzi, kuchelewa kupona kwa majeraha, maumivu ya viungo na kudhoofu kwa mishipa ya damu hasa kwenye ngozi.


6.Upungufu wa vitamin D husababisha kuleta matege.


7.Upungufu wa vitamin k husababisha kuchelewa kuganda kwa damu kwenye jeraha


UPUNGUFU WA MAJI
Maji yakipungua mwilini yanaweza kuleta madhara makubwa hata kifo. Hali hii ikitokea kuwa maji yamepunguwa kwa kiasi kikubwa sana kwa haraka mgonjwa ataongezewa maji. Hili linajulukana sana. Ila nataka kuongezea maarifa hapa kuhusu kupunguwa kwa kawaida nini adhari zake kwenye mwili. Endapo maji yakipungua kwa hali hya kawaida mtua ataanza kuhisi kiu.


Pia maji yanaweza kusababisha maumivu ya kichwa. Choo kuwa kigumu na hatimaye kutoka na damu kwa sababu ya kuchubua kuta za haja kubwa. Mkojo kuwa mchache na kutokwa na jasho kwa kiasi kidogo sana. Mtu anaweza kuhisi kuchanganyikiwa na kuhisi kama kichwa chaje ni chepesi sana. Pia athari nyingine unaweza kuziona kwenye ngozi pale ngozi inapopoteza uhalisia wake wa kujikunja na kusinyaa. Ngozi inakuwa ngumu na imekauka.


UPUNGUFU WA PROTIN
Ugonjwa wa kwashiakoo ni katika yanayoletwa na upungufu wa protini. Pia ukuaji hafifu wa mtoto na kupelekea kudumaa ni katika upungufu wa vyakula hivi. Kiriba tumbo hasa kinachotokea kwa sbabu ya kuvimba kwa ini. Hii huweza kupelekea ini kushindwa kufanya kazi. Misuli na nyama za mwili kushindwa kujaa kwa ufasaha. Wataalamu wanahusisha uimarikaji wa mifupa kuwa unategemea pia vyakula hivi. Hivyo upungufu wa protini huweza kusababisha udhaifu wa mifupa.


UPUNGUFU WA FATI
Kama hautapata fat ya kutosha kuweza kutengeneza omega-3 fat acid unaweza kupata upungufu wa vitamin A, D, E na K hivyo magonjwa yanayohusiana na upungufu wa madini haya hayatakuwa mbali nawe. Vyakula vya fati vina saidia katika kuiweka ngozi kuwa katika afya njema. Kama utakosa fati ya kutosha ngozi yako itashindwa kupata majimaji ya kutosha na hivyo kupelekea afya dhaifu ya ngozi.


Omega-3 fat acid ipo katik aina kuu mbili ambazo ni eicosapentaenoic acid na docosahexaenoic acid hizi husaidia katika ukuaji na maendeleo mazuri ya ubongo. Pindi ukikosa aina hizi za fat acid unaweza kupata matatizo ya kusahau na ukuaji hafifu wa ubongo. Omega-3 fat acid inaweza kupatikana kwenye samaki, nyama na vyakula vingine lakini si kwenye matunda wala mboga a majani. Fat acidi inasaidia katika kutengebezwa kwa pigment rhodopsin hizi husaidia katika kuboresha afya ya macho. Husaidia katika kuufanya ubongo uweze kutafasiri mwanga kuwa kitu unachokiona. Husaidia sana kwa wazee dhidi ya matatizo ya kutokuona.



Pata kitabu Chetu Bofya hapa





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1238


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

MAZINGIRA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

darasa la lishe
Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe Soma Zaidi...

Dondoo za afya 21-40
Somo Hili linakwenda kukuletea dondoo mbalimbali za afya Soma Zaidi...

Habari za uzima,nimesoma makala yako tumbo linaniuma upande wa kulia Ila sisikii Sana yenyewe Ila nikibonyeza na mkono ndio inauma yaani ni Kama nimegongwa sehem flani alafu Kuna maumivu lakini ni mpaka upaguse ndio una experience maumivu Kama Kuna namna
Kama unasumbuliwana tumbo upande wa kulia, kushoto, kitomvuni ama kuoande wa kuliavkwachini, basi muulizaji huyu atakupa uelewa. Soma Zaidi...

KIJUWE KISUKARI CHANZO CHAKE, DALILI ZAKE NA KUKABILIANA NACHO
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

UPUNGUFU WA PROTINI NA FATI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Safari ya damu kwa Kila siku
Posti hii inakwenda kukuletea mfumo wa damu mwilini na safari zake za Kila siku Soma Zaidi...

Kitabu cha Afya 01
Soma kitabu hiki cha afya sehemu ya kwanza upate kuijua afya yako. Soma Zaidi...

Zijuwe faida za kiafya za kula Zabibu
Kula zabibubkina faida nyingi kwa afya yako. Soma Zaidi...

dondoo 100 za afya
Soma Zaidi...

kitabu cha matunda
Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho Soma Zaidi...

Vyumba vidogo vidogo kwenye chumba cha upasuaji
Post hii inahusu zaidi juu ya vyumba vidogo vidogo ambavyo Vimo kwenye chumba cha upasuaji, ingawa chumba cha upasuaji ni kimoja ila kuna vyumba vingine vidogo ambavyo vinatumika kwa kazi mbalimbali kama tutakavyoona. Soma Zaidi...