Presha ya kushuka (hypotension) dalili zake na njia ya kukabiliana nayo
Presha ya kushuka ama kitaalamu huitwa hypotension, presha ya kushuka ni hatari kwa afya kama ilivyo presha ya kupanda, maana mwili unakosa nguvu kabisa.
RPESHA YA KUSHUKA (HYPOTENION)
Presha ya kushuka ama kitaalamu huitwa hypotension, presha ya kushuka ni hatari kwa afya kama ilivyo presha ya kupanda, maana mwili unakosa nguvu kabisa. Kama ilivyo presha ya kushuka presha ya kupanda unaweza kuizuia ana kujilinda nayo kwa kula vyakula salama.
VYAKULA MUJARABU KWA MWENYE PRESHA YA KUSHUKA
1.Tumia chumvi zaidi; wataalamu wa afya wanahimiza sana kutumia chumvi zaidi kwani madini ya sodium yaliyomo kwenye chumvi husaidia katika kupandisha presha. Ila tambua kuwa kwa wazee kuzidi kula chumvu kunaweza kusababisha moyo kujashinwa kufanya kazi vyema.
2.Kunywa maji mengi ya kutosha: maji husaidia katika kuongeza hali ya umajimaji kwenye miili. Hii husaidia kukabilia na upungufu wa maji mwilini (dehydration) hali hizi ni muhimu kwa kukabiliana na presha ya kushuka.
3.Punguza ulaji wa vyakula vya wanga kwa zaidi. Kwa mfano viazi mbatata, mchele na mikate
4.Kunywa chai yenye caffein;
DALILI ZA PRESHA YA KUSHUKA
1.Kushundwa kuona vyema
2.Kuchanganyikiwa
3.Kizunguzungu
4.Kuzimia
5.Uchovu wa hali ya juu.
6.Kuhisi baridi
7.Kushindwa kufikiri kwa kina
8.Kichefuchefu
9.Kushindwa kuhema vyema
10.Kutokwa na jasho
NJIA ZA KUKABILIANA NA MRESHA YA KUSHUKA
1.Fanya mazoezi ya mwili na viungo walau kila siku kwa muda wa dakika 30 mpka 60
2.Kunywa maji mengi na ya kutosha
3.Unapokaa usikae mkao wa kukunja miguu
4.Punguza ulaji wa vyakula vya wanga kama viazi mbatata, mchele na mikate
5.Punguza ama wach kabisa uvutaji wa sigara
6.Punguza ama wacha kabisa unywaji wa pombe.
HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPATWA NA PRESHA YA KUSHUKA
1.Lala chini kwenye kitu kilicho flati.
2.Kunywa maji mengi
3.Tumia chumvi, unaweza kuilamba unaweza pia kukoroga chumvi kwenye kikombe na kunywa.
4.Kama hali inaendelea kuwa mbaya zaidi ni vyema kuwasiliana na kituo cha afya kilicho karibu nawe.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 Simulizi za Hadithi Audio 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 kitabu cha Simulizi 👉5 Bongolite - Game zone - Play free game 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Fahamu Magonjwa yanayowapata watoto chini ya miaka mitano
Posti hii inaelezea kuhusiana na Magonjwa mbalimbali ambayo watoto chini ya miaka wanaweza kuyapata kiurahi.
Soma Zaidi...Ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo
Posti hii inahusu zaidi Ugonjwa wa uti wa mgongo, ni ugonjwa unaoshambulia sehemu inayofunika ubongo na pia sehemu ya spinal cord
Soma Zaidi...Maambukizi kwenye mifupa
Posti hii inahusu zaidi Maambukizi kwenye mifupa ambayo kwa kitaalamu huitwa Osteomyelitis, ugonjwa huu uaribu zaidi kwenye mifupa na sehemu nyingine ambazo zinakaribia kwenye mifupa
Soma Zaidi...dalili za mwanzo za ukimwi kwa mwanamke
Katika makala hii utakwenda kuzijuwa baadhi ya dalili za ukimwi ama HIV kwa mwanamke
Soma Zaidi...Tatizo la Kikohozi Cha muda mrefu
Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili za Kikohozi cha muda mrefu ni zaidi ya kero. Kikohozi cha muda mrefu kinaweza kuharibu usingizi wako na kukuacha unahisi uchovu. Matukio makali ya kikohozi cha muda mrefu yanaweza kusababisha kutapika, kizunguz
Soma Zaidi...