image

Kwa nini vidole vimekatwa

HADITHI YA ALIYEKATWA VIDOLE GUMBA Mimi nilikuwa mfanyabiashara mdogo sana, katika mji wa Baghdad.

Kwa nini vidole vimekatwa

HADITHI YA ALIYEKATWA VIDOLE GUMBA
Mimi nilikuwa mfanyabiashara mdogo sana, katika mji wa Baghdad. Nilikuwa ni muuzaji wa kofia na mikanda pamoja na nguo za ndani za wanawake. Ijapokuwa biashara yangu ilikuwa ni ndogo lakini ilikuwa ikinitosheleza kupata rizki . sikupata kuwa na mke wakati huo. Katika sehemu tulipokuwa tukiuza mimi ndiye niliyekuwaga mgogo pekee, nikiwa na miaka 21, huku sharubu ndio zilikuwa zikianza kuota.Siku moja akaja msichana mmoja wa kitajiri sana, niligundua hilo baada ya kumuona amepanda farasi mzuri aliyekuwa na matandiko mazuri yenye mapambo ya kupendeza zaidi. Pia alikuwa ameongozana na wajakazi wawili. Alipokuja alionekana kushangaa sana pindi lipokuwa akitazama upande tulipokuwa tumekaa mimi na mwenzangu. Basi alinagiza wajakazi wake wanunue vitu alivyotaka na walipokamilisha waliondoka, huku akiwa anatuangalia. Sikuweza kuioa sura yake wala kusikia sauti yake. Alikuwa ni mrefu wa wstani mwembamba wa kawaida. Mwenye nywele ndefu. Niligundua hilo baada ya kumuangalia vyema pindi alipogeuka.Sikuwa na umakini naye maana hata hakuwa mteja wangu. Wiki ilipita hatimaye siku ya jumamosi nikamuona tene, siku hii alikuja kwenye biashara yangu na kuulizia mikanda ya wanawake pamoja na ngua za ndani. Akataka nimchagulie nguo ya ndani inayomuenea vyama. Nilistaajabu sana maana katu sijapata mteja aliyewahi kunieleza maneno haya ya kipuuzi. Lakini pia nilistaajabu sana niliposikia sauti yake. Sauti laini, iliyo na mikwaro, nikajikuta moyo unaenda mbio na joto la mwili wangu linaongezeka. Jasho la kwenye makwapa linaanza kunichuruzika. Kwa hakika sijapatapo kusikia sauti tamu kama hii katika maisha yangu yote.Nilitamani azungumze nami maneno mengine, nipate kuthaminisha zaidi sauti ya binti huyu. Nilipogundua kuwa si mtu wa maneno mengi nikamuuliza, “unava saizi gani” hakunijibu swali langi, alifikiri zaidi ndipo akanijibu “niangalie kwa ukaribu vizuri utajuwa saizi yangu”. mmmmmhhh haya. Hapo nikapata fursa ya kuthaminisha ngombe kwenye gunia. Nilistaajabu sana baada ya kuona mapigo ya moyo yanaongezeka na jasho la kwapa ninanitoka.Nikaanza kumchagulia niliyoona inamtosha, nikampatia kisha kimpatia na mkanda. Wakati naendelea kuchaguwa alikuwa akiniangalia sana usoni. Alikuwa amefunika sura yake lakini niligundua kuwa alikuwa ananikonyeza. Sikupata kuiona sura yake, lakini niliamini huenda ni mrmbo kama sauti yake. Nilianza kuvutiwa na mteja wangu. Alipomaliza vitu vyake akaondoka bila hata kujuwa anapokaa.Niliwaza kuwa pindia akija tena nimuulize maswali kadhaa nipate kujuwa nitamkuta wapi pindi nikimtafuta. Hali haikuwa kama nilivyotaka, muda mrefu ulipita bila hata ya kumuona. Baada ya wiki kama mbili akaja tena siku hii akadai kuwa amesahau pesa hivyo anaomba nimkopee atakweda kuniletea pesa siku nyingine. Kwa kuwa nilishaanza kulewa nikakubali kumkopea.Alichukuwa karatasi na kuanza kutaja bishaa anazotaka. Nikaenda kumkopea vitu vile nikiwa mimi ndiye dhamana. Ilikuwa ni siku ya kipupwe, nilipokuwa ninarudi ghafla nguo aliyoifunika sura yake (nikabu) ikapeperuka, na hapo nikapata kuona sura iliyobandikwa kwenye paji lake. Nilitamani awe ni sanamu liwe nyumbani kwangu. Nilipata kuvutiwa ghafla na urembo wa binti huyu. Niligundua hakuwa na mkunjo hata mmoja kwenye uso wake. Nilizidi kulewa na kupenda.Nikamletea bidhaa na nikapata kusikia neno ahsante kutoka kwenye kinywa chake. Niligundua anatabasamu pana na la kuvutia. Matukio yote haya yalitokea kwa muda mchache sana. Alichukuwa bidhaa zile na kutokomea mtaani. Nilishikwa na butwaa na nikasahau kumuuliza ni lini ataleta pesa ya watu. Nilipata kugundua kuwa kumbe unaweza kupenda hata kwa siku moja.. sikuweza kula, kulala wala kusinzia, kana kwamba sira yake ilikuwa ipo ukutani.Niliamaka usiku nikakamata nguzo na kushika ukuta huku nikiufananisha ndiye yeye. Hatimaye nikapitiwa na usingizi paleplae. Asubuhi nilijikuta nipo chini, nikakumbuka hasa nini kilitokea. Wii moja, mbili na hatimaye mwezi ukapita bila ya kutokea, na huku ninadeni lake. Wenye mali zao walikuwa wakinitaka nilipe pesa yako. Mikawa nawwhidi kuwa nitawalpa kesho.

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 205


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Harusi ya aladini na binti sultani
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

HADITHI YA TUNDA EPO
Soma Zaidi...

Deni la Penzi
DENI LA MAPENZI Badisiku ambayo niliamua niuze vitu vya ndani kwangu ili nilipe madeni ya watu, ndipo yule binti akatokea tena. Soma Zaidi...

Mrembo mtoto wa tajiri
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Aladini na binti wa mfalme
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya mshumaa wa ajabu Soma Zaidi...

Jaribio la pili la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Hadithi ya mjakazi wa Mfalme
HADITHI ILIYOSIMULIWA NA MJAKAZI WA SULTANI Mtukufu sultani, nakwenda kukusimulia tukio lililotokea leo hii wakati tulipokuwa tunaburudika. Soma Zaidi...

Ujumbe wa Siri kwenye kitabu cha ajabu
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Mshenga wa aladini mbele ya mfalme kwa mara ya pili
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Wagen wa Ajabu
UJIO WA WAGENI WA BARAKA. Soma Zaidi...

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA KITABU CHA PILI
Soma Zaidi...

NDANI YA JUMBA LA ALADINI
Soma Zaidi...