Navigation Menu



image

NANI MUUAJI?

Download kitabu Hiki Bofya hapa NANI MUUWAJI?

NANI MUUAJI?

pic
Download kitabu Hiki Bofya hapa

NANI MUUWAJI?

Mfalme alipoamka alitaka kumuona kijana wake lakini asimuone. Akauliza habari za kijana yule na akaelezwa kuwa amefariki lakini muuwaji hajulikani, mpaka sasa kuna wauwaji wanne na kila mmoja anadai yeye ndio muuwaji halisi. Mfalme akaamrisha wote waitwe na waje mbele yake na amtafute muuwaji halisi wa kijana wake yeye mwenyewe.

Mfalme aliogopa sana asije fanya kosa kama lile alolifanya kwenye kesi ya kifo cha mtoto kwenye ndoo ya maji ambapo mtu asiye na hatia aliuliwa. Walinzi wa mfalme wakamuuliza kwani ni kitu gani kilitokea kuhusu kesi ya mtoto huyu. Akawasimulia kwa ufupi habari hii kuwa alikiwepo mama mmoja aliyekuwa na mtoto anayeanza kusimama dede. Pale ndani palikuwepo na mfanya kazi wao. Mtoto yule alizoeshwa kuogeshwa kwenye ndoo ya maji na mama yake a alikuwa akifurahia sana anapotiwa kwenye ndoo ya maji.

Siku moja mama yule alipata safari ya ghafla na kumuacha mtoto wake kwa jirani maana mfanyakazi hakuwepo alikwenda kuchota maji mbali kidogo. Mtoto yule akiwa kwa jirani alitoroka na kyurudi kwao. Na kwa kuwa milango ilikuwa wazi aliingia ndani na kukuta ndoo za maji zipo wazi. Mtoto yule akaingia kwenye ndoo zile na kupitiwa na usingizi. Dada mchota maji alipokuja hakuangalia vizuri kwenye ndoo akajaza maji na kuondoka kwa haraka ili akawahi foleni ya maji.

Mtoto mule kwenye ndoo alipiga kelele na kayanywa maji zaidi na hatimaye akapoteza maisha. Akaja dada wa kazi na kujaza ndoo ile kisha akaifung bila ya kuangalia nddani. Akazipandanisha ndoo kama tatu. Mama aliporudi alimtafuta mtoto kwa jirani bila ya mafanikio. Juhudi za kumtafuta ziliendelea ndani ya siku tatu bila hata kufanikiwa. Majirani wakamuonea huruma mwenzao na wakaamua kumpikia apate kula, wengine wakaanza kufua nguo zake na kudeki nyumba maana ndani ya siku tatu hakukuwa kukipikwa wala kufagiliwa wala kudekiwa.

Maji yalipobakia ndoo moja wakamkuta mtoto amshakufa kwenye maji. Mama yule kwa hasira alimpeleka mfanyakazi wa hakimu na hatimaye mfanyakazi akauliwa kwa kosa la kumuuwa mtoto kwenye maji na kumficha na ndoo. Kumbe mfanya kazi hana hatia maana ni mama aliyemzoesha mwanae kuingia kwenye ndoo na nikosa la jirani kutomuangalia vizuri mtoto. Kosa la mfanyakazi kuweka maji bila ya uangalifu. Hivyo nahofia kesi hii isijekuwa na mfanano na hii. Basi kwa haraka akaagiza waletwe wat wote wanaohusika mbele yake.

Watu wote wakapelekwa kwa mfalme pamoja na maiti wao. Falme akaanza kuuliza mmoja mmoja ataje amemuuwa vipi. Hapo mlevi akasema namna ambavyo tukio limetokea, kisha muuza nyama akaeleza tukio lilivyotokea kwa upande wake kisha tabibu kisha mshona nguo. Baada ya kiusikia maelezo ya kushangaza mfalme akaamuru habari hii iandikwe kwa wino wa dhahabu na iwekwe kwenye kumbukumbu za kifalme. Kisaha mfalme akauliza je kuna mwenye hadithi inayoshangaza zaidi ya hii ya kijana wangu huyu? Hapo mlevi akasema yeye ana hadithi ya kushangaza zaidi ya hii. Na akaanza kusimulia kama ifuatavyo;-


                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela2 Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1036


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Siri ya wageni wale
SIRI YA WAGENI WALE INAFICHUKA Tambua ewe kijana changu, mimi na baba yako tulikutana zamani sana. Soma Zaidi...

KIFO CHA AJABU
Download kitabu Hiki Bofya hapa KIFO CHA MTOA BURUDANI WA SULTAN. Soma Zaidi...

Mrembo mtoto wa tajiri
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Viatu vya ajabu
VIATU VYA AJABU VYAONDOKA NA MKONO WANGU Aliponieleza sifa za viatu anavyotaka nikamsogelea kwa ukaribu na kumkazia macho kama nataka kumpiga vile kisha nikamuuliza “wewe ni nani, na ni nani amekutuma, vina nini hasa viatu hivi” alibakia kimya ... Soma Zaidi...

BINTI MZURI ASIYETAMBULIKA
BINTI HUYU NI NANI? Soma Zaidi...

UJUMBE WA SIRI KWENYE KITABU CHA AJABU
Soma Zaidi...

Hadithi iliyosimuliwa na kijakazi wa sultani
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Ndoa ya siri
NDOA YA SIRI YAFANYIKA Hatimaye siku ya ijumaa ikafika na mimi nikaoga nyema na kuchukuwa kanzu iliyo nadhifu zaidi. Soma Zaidi...

Hadithi ya aladini na taa ya mshumaa wa ajabu
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi ya aladini na taa ya mshumaa wa ajabu Soma Zaidi...

Deni la Penzi
DENI LA MAPENZI Badisiku ambayo niliamua niuze vitu vya ndani kwangu ili nilipe madeni ya watu, ndipo yule binti akatokea tena. Soma Zaidi...

Kwanini dirisha moja?
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Hadithi ya kilema, mtanashati asiye na mkono
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi ya kilema, mtanashati asiye na mkono Soma Zaidi...