HADITHI YA KAKA WA TANO WA KINYOZI

HADITHI YA KAKA WA TANO WA KINYOZI

HADITHI YA KAKA WA TANO WA KINYOZIBaba yete alikuwa ni mfanya biashara. Alijaaliwa na kuwa na umri mrefu tunaweza kukadiria kuwa alipatapo kuishi miaka isiyopungua 90. alipofariki aliacha kiasi cha pesa kilicho kingi. Vipande vya dhahabu , fedha na almasi. Tulugawana urithi kawa kwa sawa. Kila mmoja kati ya sisi alitumia oesa yake kwa namna aliyoitaka. Hata mimi nilitumia pesa ile. Haikupita muda mrefu hakuna aliyebakiwa na pesa ile ila ni kwa uchache. Hakuna aliyefaninikiwa kufanya jambo kubwa lenye kuonekana mbele za watu. Hakika sikuachkujilaumu kwa uzembe wa matumizi nilioufanya. Kaka yangu wa tano naye hakuacha kujilaumu kwa kosa alilifanya.


Baada ya kukusanya mawazo kaka aliamuwa kufanya biashara kwa hicho kiasi kidogo alichonacho.alikusanya mawazo yake na kujiridhisha kuwa biashara ya vioo itaweza kumtosha kwa kiasi alichonacho ataweza kupata mwanzo. Kaka akaenda duka la jumla na kukusanya mzigowa vioo vilivyo katika ukubwa na maumbile tofautitofauti. Kisha akafungua duka lake karibu na njia yenye panda. Kaka alipamba vyema duka lake na kuliweka manukato. Alitambuwa kuwa wateja wake watakuwa ni wanawake na watu wa hadhi za juu. Hivyo kuweka manukato kweenye duka kutafutia watu wa aina hizo.


Ilikuwa siku ya ijumaa, kaka hakuwenda kufanya ibada siku hiyo. Alipikuwa amekaa kwenye duka lake akiwa ameegeme kiti akapata wazo kupanga vii vyake kwa nje ili kuvutia zaidi watej. Kaka akatoa robo tatu ya vioo vyote vilivyopo ndani na kuvipangilia vyema. Alivipandanisha katika mpangilioulio bra sana mbele ya macho ya mtazamaji. Kisha akaketi kwenye kiti karibu na viio huku ameegemea nguzo kubwa. Katika hali kama hiyo akaanza kuona sura za watu na warembo zikipita. Kwa kutumia vii aliweza kuona vyema sura za wadada hata bila ya kuwaangalia moja kwa moja. Mara akaona sura ya bint mrembo sana mtoto wa waziri mkuu.


Kaka alianza kupata mawazo ya hapa na pale. Mawao yaliendelea kujengeka katika fikra zake hata ikawa kama ndo uhalisia. Kaka alizidi kuwaza hata akatoka kabisa katika eneo lile na akabakia mwili tu. Katika mawazo yake kaka aliwaza kuwa 'Dah'.!!! kwa vioo vyaku hivi kama biashara ikinikalia sawa nitaweza kupata faida kubwa. Kama mzigo huu ukiisha nitakwenda kununua mzigo mwingine. Bila shaka faida yake itakuwa ni mara nne ya mtaji wangu. Nitanunuwa mzigo mwengine na mwengine na mwengine. Na kama duka hili ndio halitoshi nitafunguwa maduka mengimengi mjini hapa.


Nitajenga majumba matatu ya kifahari katika eneo moja. Ukuta mrefu uliozungukwa na uzio wa mawe ya thamani utazunguka majumba yangu. Nitanunuwa vijakazi wa kike na wakiume wengi kwangu. Mambostani ya matunda na mauwa ya kuvutia nitaweka. Nitanunuwa wanawae wa kutoa burudani na vitu vingi. Baada ya kujiridhisha utajiri wangu nitakwenda kwa waziri mkuu kwenda kumposa mtotot wake. Kwa kuwa waziri mkuu hanijuwi na hatakuwa anajuwa utajiri wangu atanikatalia. Akifanya hivi nitamchukuwa mtoto wake kwa nguvu. Sitamwambia kitu kuwa mimi ni anai na nini ninamiliki.


Nitakwenda naye mtoto wa waizri hadi nyumbani kwangu. Sitamgusa hata kidogo siku itakayofata nitachukuwa msafara wa vijakazi wakike na kiume wasiopunguwa 20. farasi wawili watapambwa kwa matandiko ya hariri yaliyochovywa kwenye dhahabu nyekundu. Viatu vya farasi vilivyotengenezwa kwa madini ya almasi. Farasi wawili watakuwa wanangaa na kuumiza macho ya watazamaji. Farasi mmoja nitampanda mimi na mwingine atapanda mtoto wa waziri. Katika msafara kila kijakazi atakuwa amebeba vipande 100 vya dhahabu na fedha. Mizigo yote itakuwa kwenye ngamia wawili.


Mimi na mtoto wa waziri tukifuatwa na vijakazi tutaelekea mjini kufurahisha macho na kujionesha kuwa kuna tajiri mwingine pembeni kidogo ya mji anaingia katikati ya mji. Nitashuka kwenye farasi na kutembea kwa mguu. Mavazi yangu yatakuwa yanang'aa na kuwaka kama mbalamwezi. Zitankia nguo zangu hata wadada wote wanifuate na kunikumbatia. Watatka kunibusu, na hapo ndipo nitamshika mkono mtoto wa waziri. Pindi wakimuona wataogopa. Nitaelekea kwa waziri ambaye atakuwa ndiye baba mkwe. Kwa kuwa mwanzo alinikatalia na nikamchukuwa mwanaye kingivu leo nataka akanipongeze.


Nikifika kwa waziri hataamini kama ni mimi. Yeye mwenyewe atasimama kunisalimia na kunitengea sehemu ya kukaa. Kwa dharau sitakaa hata niumpatie kwanza Fedha na dhahabu kutoka kwa kijakazi mmoja. Waziri hataamini kama mimi ndiye yule aliyenikatalia. Mtoto wa waziri atafurahi kumuona baba yake kwa mara nyingine. Waziri na mkewe wataingia ndani kujadili kitu. Wakitoka watakubaliana kuwa nimuoe biti yao. Nitakubali na kuwapatia vipande vya dhahabu na fedha nyingi. Nitakaa kwa waziri kwa juma moja kisha nitaelekea kwangu na mkewangu.


Nikifika kwangu nitajifanya ni mtu mwenye majigambo kidogo. Endapo mke wangu ataniletea maji ya kunywa nitakataa kunywa kwa kigezo kuwa maji ni machafu. Akiniletea chakula nitakipiga teke pu'! kwa kigezo kuwa sahani chafu' basi kaka alipofanya kama anapiga teke sahani la chakula ndipo alipopiga teke vioo. Na kwa kuwa vioo vilijipanga vyema ndipo vikaanza kuanguka na kuvunjiaka vyote hakuna kilichobakia salama. Kaka alilia sana, alibaiwa na vioo kidogo sana ndani. Watu wakakusanyika kujuwa kilichotokea. Kaka aliwaeleza kuwa ilikuwa ni bahati mbaya kwa mawazoa liyonayo alipiga teke. Watu walimpa pole na kuanza kuondoka.


Kaka aliendelea kulia kwa muda, wakati kaka anaendelea kulia mara si ndio akapita binti mwingine, mzuri sana zaidi ya mtoto wa waziri. Binti yule akaulizia kilichotokea. Akaeezwa na kwa huruma akampatika akaka fedha na vipande mia tano vya dhahabu. Pesa hii ilikuwa ni mara tatu ya mtaji alioanzia biashara. Kilio kilikata kwa furaha kaka akarukaruka sana. Bila hata ya kumuangalia vyema binti aliyempatia msaada, wapia anatoka na anafanya nini pale mjini. Kaka akasafisha eneo lile na kuingia ndani. Ghafla mlango ukagonjwa na bibi kizee akaingia. Bibi alitaka maji ya kutawadha ili aswali.


Kaka hakuwa anamfahamu bibi huyo. Akampatia maji na alipomaliza kuswali kaka akatowa vipande viwili vya dhahabu. Bibi alikataa na kusema 'ni vyema ungekwenda kumpatia shukrani aliyekupa fedha hiyo' kwani anakaa wapi 'kama una muda nifate nikupeleke' haya yalikuwa ni mazungumzo kati ya kaka na bibi. Kisha wakafuatana kuelekea kumuona. Bibi akamueleza kaka kuwa 'huyo binti ameolewa, ila kwa muda huu ume hayupo. Hivyo kuwa makini sana usije kutwa na kufikiriwa vibaya' bibi aliendelea kusema na kuongoza njia. Walipofika kwenye geti kubwa, geti jeusi bib akagonga na mdada wa makamo akaja kufunguwa geti. Bibi ana kaka wakaingia ndani. Loo!!! binti mrmbo sana alitokea akiwa na hereni zinazo meremeta kama kio kilichoakisi mwanga. Mashavu yaliyojazia na pua ndefu yenye vitone vya jasho kwa juu. Alikuwa akitembea kwa madaha kama kinyonga. Hakika alikuwa ni mzuri na wa kupendeza.


Hakuwa amejifunika sura ila hakuweza kuonekana viungo vyake ila vile ambavyo ni halali kuonekana kwa mujibu wa dini ya kiislamu. Kaka alitamani asingekuja maana ilikuwa I fitina kubwa kumuona mke wa mtu. Kaka alieleza shida yake kuwa amekuja kutoa shukrani. Binti akamwambia kaka amfate. Kaka amamfuata binti yule hadi katika chumba kingine. Chumba kilikuwa na kitamnda kilichowekwa katikati ya chumba. Zuria la rangi nyekundu na njano lililopamwa vye ma kwa maandishi ya kiajemi na kirumi. Meza kubwa yenye vikombe vya dhahabu na vinywaji vya kuvutia macho. Kaka alishangazwa sana na uzuri ulioje wa chumba kile.


Kulikuwa na masofa mawili yaliyopamwa kwa magodoro ya harori na sufi iliyo nyepesi. Masofa yalikuwa yakiangaliana. Kaka akakaa na yule binti akaa pembeni na kunena kuwa 'bibi atakuwa amekuambia kuwa mimi nimeolewa, ukwel ni kuwa sikuolewa'. kaka nafsi ikatulia na kuanza kufurahi. Waliendelea kuzungumza na baadaye binti akamwambia kaka nisurbiri hapa hapa usiondoke. Binti akatoka na baada ya muda wa dakika kama 10 akaja kijana mmoja wa kiafrika shupavu na aliye mweusi sana. Alishika upanga na kusema kuwa yeye ndiye mume wa binti na amemkamata kaka kuwa anazini na me wake. Kijana akamkata mapanga kaka na akaka akapotez afahamu kabisa. Kijana akadhani kaka amekufa.


Kijana akaita 'almellah njoo' yule binti aliyefunguwa mlangoa akaja na bakuli la chumvi. Wakampaka kaka katika majeraha yake' kisha wakamburuza na kumpeleka katika chumba kingine. Kaka alipata fahamu na kujiburuza hadi akatoka nje kwa lango wa nyuma. Aka alirufi mjini na kutibu majeraha yake. Alipopona akavaa nguo za kigeni na kupaka mekapu hata akabadilika sura na akawa kama mtu mgeni. Alikaa kumvizia yule bibi. Baada ya muda akampata yule bibi na akachukuwa upanga wake vyema. Kama kawaida yule bibi akamlebulebu ili aendenaye. Alipofika yule binti alifanya kama alivyofanya mwanzo.


Alipokuja kijana kaka akamuwahi kwa kumkata upanga kisha akamuita almellah na kamkata upanga. Akamfuata bibi bia akamkata upanga. Akamkamata yule binti. Binti akajitetea kuwa yeye huwa anafanya kwa kulazimishwa. Binti akamwambia kaka nenda kate watu tuje tuhamishe mali za hapa tukaishi mbali, kwani mimi nakupenda unioe. Kaka alitoka haraka kwend akuita watu. Kaka alichofanya ni kwenda kuchukuwa mkokoteni. Alipofika pale hakukuta kitu ila pesa chache na vipande vichache vya dhahabu. Kaka akachukuwa pesa ile na baadhi ya dhamani za ndani. Kaka akavipeleka kwake. Asubuhi akashangaa kuna askari mlangoni. Askari waliingia ndani na kuchukuwa baadhi ya vitu na kumtaka atoe maelezo alipovipata.


Kaka alizungumza kila kilichotokea. Kaka akaambiwa wewe ni mwizi na ni muuwaji. Ila cha kukusaidia ondoka hapa mjini na tafuta sehemu ya kuishi vinginevyo habari zikimfikia kadhi utauliwa. Kaka alijifunganya ili kesho asubuhi aondoke. Ukusi ule waliinga wezi na katika kuminyana wakamkata kaka sikio na kuondoka na baadhi ya mali. Nilipozipata habari za kaka nilikwend kumchukuwa kisisrisiri. Kinyozi akamaliza kwa kusema hii ndio hadithi ya kaka yangu wa tano. Kisha akaendelea kuhadithiahadithi ya kaka wake wa sita kama ifuatavyo:-

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 139


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

KUTOKA KWENYE KISIMA MPAKA KUWA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa KUTOKA KWENYE KISIMA MPAKA KUWA MFALME. Soma Zaidi...

MAAJABU NA UWEZO WA CHEETAH
5. Soma Zaidi...

Utajiri wa Baba na kifo chake
UTAJIRI WA BABA NA KIFO CHAKE. Soma Zaidi...

Kitabu Cha hadithi ya Chongo
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

HADITHI YA CHONGO WA PILI MTOTO WA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA CHONGO WA PILI MTOTO WA MFALME. Soma Zaidi...

SAFARI YA MAJIBU JUU YA MASWALI MAWILI
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA MAJIBU JUU YA MASWALI MAWILI. Soma Zaidi...

HADITHI YA MZEE WA PILI NA MBWA
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MZEE WA PILI NA MBWA WAWILI WEUSI. Soma Zaidi...

Kitabu Cha Hadithi ya mvuvi
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

NDOTO YA MGONJWA MTOTO WA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa NDOTO YA MGONJWA BINTI WA MFALME. Soma Zaidi...

SIRI
Kutoka kwenye usingizi mzito unaamka, Haujui nini kimetokea (uenda ukawa umepoteza kumbukumba). Soma Zaidi...

HADITHI YA BINTI WA KWANZA NA MBWA
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA BINTI WA KWANZA NA MBWA. Soma Zaidi...

HADITHI YA KAKA WA TANO WA KINYOZI
Soma Zaidi...