image

Deni la Penzi

DENI LA MAPENZI Badisiku ambayo niliamua niuze vitu vya ndani kwangu ili nilipe madeni ya watu, ndipo yule binti akatokea tena.

Deni la Penzi

DENI LA MAPENZI
Badisiku ambayo niliamua niuze vitu vya ndani kwangu ili nilipe madeni ya watu, ndipo yule binti akatokea tena. Ilikuwa kama bahati vile akanikabidhi pesa ndefu nikalipa madeni na haikubakia hata kidogo. Siku hiyo alikaa karibu nami na kuanza kuzungumza hapa na pale. Nilimuomba niione sura yake kwa ukaribu zaidi, alimuita mjakazi wake mmoja na kumwambia akae karibu naye, kisha akafunua kitambaa kilichoziba uso wake.Nilipata kujiridhisha baada ya kukutana na nyusi ndefu zilizolala vyema, zilizo nyeusi sana, silizonyooka kama mwezi mwandamo. Macho ya duara yaliyo meupe. Nywele nyembamba, zilizoshuka kukaribia masikio. Hakuwa mweupe sana kama mwarabu wa Sham. Sikupata kujuwa nini amepaka kwenye midomo yake, maana alikuwa anameremeta. Sikutaka zaidi kumuangalia, niliamini itakuwa ni makosa. Kwakuwa nilikuwa naangalia uso, iliniridhisha kukubali uwepo wake.Hatimaye nikatamk maneno kumweleza, kama kuna dawa umenipa. Mwenzio zilali kutwa kucha kukuwaza. Siwachi kufukiri sura yako machoni mwangu. Nakiri kwa ulimi wangu, penzi lako nahitaji. Nilijikuta nabwabwanya maneno yasiyo mpangilio, yasiyo na vina vya mashairi, wala weledi wa mazungumzo. Niliamini kubwabwanya kwangu kutakuwa kumeelewaka japo kidogo. Hakuweza kunijibu kitu chochote, ila alinieleza kuwa atanijibu kwa barua. Lakini aliniomba kuwa nimkopee tena bidhaa kama za siku ile.Hata sikuwahi kufikiri, nikaingia kwenye maduka ya wenzangu na kumchukulia bidhaa zake. Kwa haraka akawaagiza vijakazi wake, wakafunga mzigo na kupotelea mtaani. Baada tu ya kuondoka nikaanza kujiuliza, hivi inamaana utajiri wote alionao yule binti ndo anashindwa kuwa na pesa ya kununulia bidhaa hizi?, ama hii ni mbinu ya matajiri kunyonya wanyonge. Sikuweza kuwaza sana maana kila nikikumbuka sura yake, na kimna ambavyo moyo wangu kwake, hata deni pia nalisahau.Sasa nikawa na mambo mawili ya kusubiria, kwanza barua na pili ni pesa ya watu. Sikumoja mapema asubuhi nikapokea barua kutoka kwa mtu asiyejulikana. Barua iliandikwa kwa maandishi meusi, kutokana na wino wa ngisi uliochanganywa na manukato. Imeandikwa kwenye karatasi nzuri. Kwa shauku nilikata kamba na kufungua barua ile. Maneno machache yaliandikwa:Salam, kipenzi, natumai upo salama. Nashukuru kwa nguo ulionichagulia siku ile imenitosha sawa. Ujumbe wa barua hii utaletewa ifikapo jioni, na pesa yako pia. Basi ilipofika jioni akaja moja kati ya wale wajakazi wake. Akanipatia pesa yangu kisha akaanza kusimulia:-“.….. toka alipoondoka hapa siku ile hakuweza kulala kwa kukuwaza wewe. Anakupenda na amenituma nije nikwambie hivyo. Kama upo tayari anakutaka wende ukaonekane kwao.” kwani anaitwa nani na kwao ni wapi? Huu ni mzigo wa maswali nilio mjibu. Anaitwa Shaniat bint ‘Aziz mkwe wa sultani Harun Rashid. Mmh sasa nitafikaje kwao?” nilimuulliza. “…. kuna mtihani umepewa na mke wa mfalme, uende kwa siri, ukifanikiwa atafanya taratibu zote za harusi yetu badala ya kuridhishwa nawe atakapo kuona, na kama ukifeli ukakamatwa, basi utapoteza maisha” haya ndiyo maneno aliyonijibu.Sikujuwa ni kwa nini ameamuwa kunipa mtihani huu. Lakini nilijuwa kuwa kama nisipoweza kumuona ka masiku mengi zaidi huwenda nikawa kichaa ama punguani. Niliamini ni bora nijaribu kwenda kwa siri nikifa nife kiume, kuliko kubakia hapa na kujiwazia naishia kukumbatia ukuta. Nikamjibu kuwa nimekubali. Basi akanielekeza kuwa kesho mida ya jioni niende kwenye bostani lililopo karibu na ikulu na hapo nitakutana nae.

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 282


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Hadithi ya kinyozi
Soma Zaidi...

Hadithi ya tabibu
HADITHI ILIYOSIMULIWA NA TABIBU: Tambua ewe Sultani mwadilifu kuwa mimi nimezaliwa katika familia ya wachamungu waabuduji wanaofata mila za kiyahudi. Soma Zaidi...

JARIBU LA PILI LA ALADINI
Soma Zaidi...

Nani muuaji?
Posti hii inakwenda kukusimulia kuhusu muuaji wa mtoa burudani wa sultan Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa tano wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

UGENI WA DHATI
Soma Zaidi...

NANI MUUAJI?
Download kitabu Hiki Bofya hapa NANI MUUWAJI? Soma Zaidi...

Hadithi iliyosimuliwa na tabibu
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

HADITHI YA KAKA WA SITA WA KINYOZI
Soma Zaidi...

hatima ya kinyozi
Soma Zaidi...

Hadithi ya kinyozi yeye mwenyew
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

MSHENGA WA ALADINI MBELE YA MFALME KWA MARA YA PILI
Soma Zaidi...