viapo
20.
20.Kujiepusha na Viapo
Waislamu tumekatazwa kuapa apa ovyo ovyo. Kiapo kinakubalika tu pale inapobidi kutolewa mbele ya Kadhi kama ushahidi. Mara nyingi mtu anayeapa apa ovyo ovyo ni muongo. Anaapa ili ahalalishe uwongo. Anahisi kuwa akisema bila kuapa watu hawatamuamini. Kuapa apa ovyo ni tabia ya kinafiki. Tunafahamishwa katika Qur-an kuwa wanafiki wakati wa Mtume (s.a.w) walikuwa wakificha ubaya wao dhidi ya Uislamu na Waislamu kwa kutoa viapo mbele ya Mtume (s.a.w). Lakini Allah (s.w) alimfahamisha Mtume wake kuwa asiamini viapo vyao kwani wao ni waongo.
21.Kujiheshimu na kuwaheshimu wengine
Katika Uislamu kila mtu anayo haki ya kuheshimiwa. Heshima ni haki ya mwanaadamu aliyozaliwa nayo. Miongoni mwa mambo ya msingi aliyousia Mtume (s.a.w) katika khutuba yake ya kuaga aliyoitoa katika uwanja wa Arafa 9 Dhul-Hijjah 10A.H, ni kulinda heshima ya kila mtu. Aliusia:
“Enyi watu hakika damu yenu (yaani uhai wenu), mali zetu na heshima yenu ni vitu vitakatifu kamwe visiharibiwe hadi mtakaposimamishw a mbele ya Mola w enu, kw a utukufu w a vitu hivyo ni kama ulivyo Utukufu wa siku hii, na mwezi huu na mji huu. Kwa hakika mtakutana na Mola wenu na atakuulizeni juu ya vitendo vyema. Je, nimefikisha ujumbe? Ee! Allah shuhudia ”.
Kutokanana usia huu kila Muumini analazimika kuwaheshimu wanaadamu wenzake wakubwa na wadogo. Aseme nao kwa uzuri, asiwadharau, asiwadhalilishe, asiwafedheheshe na asiwavunjie heshima kwa namna yoyote ile. Awatii wazazi, wenye mamlaka juu yake na walio wakubwa kwake katika mambo yote yanayowafikiana na Qur-an na Sunnah, awahurumie na kuwasikiliza walio chini yake au wadogo zake. Kwani Mtume (s.a.w) amesema:
“Si katika sisi yule ambaye hamheshimu mkubwa wetu na kumhurumia mdogo wetu ”.
Kuwaheshimu watu kama ilivyosisitizwa katika Qur-an ni pamoja
Kuzungumza na watu kwa kauli nzuri, kwa upole na huruma. Qur-an inatuamrisha:
“... Na semeni na watu kwa wema...” (2:83).
(ii) Kuwatii wazazi, kuwahurumia na kusema nao kwa vizuri:
~ ~ ~
“... Na sema nao (wazazi) kwa msemo wa heshima (kabisa)”. (17:23).
“Na wanapofika wale wanaoamini aya zetu wambie “Assalaam alaykum” (yaani amani iwe juu yenu)...” (6:54)
(iv)Kurudishia saalam kwa ucheshi baada ya kusalimiwa:
“Na mnapoamkiwa kwa maamkio yoyote yale; basi itikieni kwa yaliyo bora kuliko hayo, au rejesheni hayo hayo. (4:86)
(v)Kuwaheshimu watu wa dini nyingine kwa kutowabughudhi, kutowadharau au kutowadhalilisha kwa namna yoyote ile:
“Wala msiwatukane ambao wanaabudu kinyume cha Allah, was ije wakamtukana Allah kwa jeuri zao bila kujua....” (6:108).
“Waite (watu) katika njia ya Mola wako kw a hekima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako ndiye anayemjua aliyepotea katika njia yake.. (16:125).
(vi)Kuwakaribisha wageni na kuwapisha kwenye viti au nafasi ya kukaa:
“Enyi mlioamini mnapoambiw a (katika mikutano): “Wafanyieni w asaa wenzenu katika (nafasi za) kukaa”, wafanyieni nafasi. Na Mwenyezi Mungu atakufanyieni nafasi (Duniani na Akhera). Na (hata) ikisemwa, “Simameni”, (ondokeni muw apishe w enzenu), basi ondekeni. Mwenyezi Mungu atawainua wale walioamini miongoni mwenu, waliopewa elimu watapata daraja zaidi. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda ”. (58:11)
Ili mtu aheshimiwe hana budi kujiheshimu yeye mwenyewe na kuwaheshimu wengine.Mtu asiyejiheshimu hujidharaulisha yeye mwenyewe kwa wanaadamu wenzake. Muheshimiwa zaidi mbele ya Allah ni yule anayemheshimu na kumtii Allah (s.w) na Mtume wake.
“... Hakika aheshimiw aye sana miongoni mwenu mbele ya Allah ni yule amchaye Allah zaidi katika nyinyi. Kwa yakini Allah ni Mjuzi Mwenye habari(za mambo yote).” (49:13)
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉3 Bongolite - Game zone - Play free game 👉4 web hosting 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 ai web app
Post zinazofanana:
Utaratibu wa lishe kwa wazee
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu utaratibu wa lishe kwa wazee
Soma Zaidi...Hizi ni kazi za mapafu mwilini
Makala hii itakwenda kukufundisha kazi 5 za maafu mwilimi. Wengi tunajuwa tu kuwa mapafu yanafanya kazi ya kupumuwa. ila si hivyo tu yapo mengi zaidi.
Soma Zaidi...huduma ya kwanza kwa mtu aliyeingiwa na uchafu sikioni
Post hii inahusu huduma ya kwanza kwa mtu aliyeingiwa na uchafu au kitu chochote sikioni. Sikio ni mojawapo ya milango ya fahamu ambapo hutumika kusikia, Kuna wakati vitu uingia ndani yake na kuleta madhara
Soma Zaidi...Upungufu wa vyakula na madhara yake
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya upungufu wa vyakula
Soma Zaidi...Huduma kwa wenye ugonjwa wa herpes simplex au vipele kwenye midomo na sehemu za siri
Post hii inahusu zaidi tiba na huduma kwa wenye ugonjwa wa herpes simplex au vipele kwenye midomo na sehemu za siri.
Soma Zaidi...Utaratibu wa maisha kwa aliye athirika
Somo hili linakwenda kukuletea utaratibu wa maisha kwa aliye athirika
Soma Zaidi...