Dalili Kubwa za kukaribia Siku ya kiama
Dalili Kubwa za kukaribia Siku ya kiama
Mtume (s.a.w) pia ametutajia dalili kubwa za kukaribia kwa siku ya Mwisho. Dalili hizo zinapatikana katika Qur’an na Hadith kama inavyobainishwa hapa chini:“Na kitakapokaribia Kiyama, tutawatolea mnyama kutoka ardhini atawaeleza (watu) kwa kuwa watu walikuwa hawaziamini aya zetu” (27:82)“Mpaka watakapofunguliwa Ya’juj na Ma’juj nao wataporomoka kwa kasi, na ikakaribia ahadi ya kweli kufunguliwa, hesabu na malipo, basi wakati huo macho ya makafiriyatatokeza mno juu ” (21:96 – 97)
Katika hadith aliyoipokea Imam Ahmad, na kusimuliwa na Khudhaifa Ibn Usaid Al – Ghifaar (r.a) amesema; Alitutokea Mtume (s.aw) kutoka chumbani kwake na sisi tukikumbushana jambo la kiyama, Mtume (s.a.w) akasema: Hakitosimama Kiyama mpaka muone alama kumi,
1. Kuchomoza jua Magharibi
2. Kutokea moshi mkubwa utakaochafua mazingira (pollution)
3. Mnyama atatokeza na kuwasemesha watu (27:82)
4. Kufunguliwa Ya’juj na Ma’juj (21:96 97)
5. Kurudi kwa Issa mwana wa Maryam
6.Kuja kwa Masih Dajal (False Messayah)
7.Kutoka Moto (Volcano) katika pango la Aden ukiwaendesha watu
8.Dunia kugawika mapande matatu (Three Blocks); Pande la Mashariki (Eastern Block)
9.Pande la Magharibi na (western block)
10.Bara Arab (Mashariki ya kati - Middle East)
Kwa hakika Qur’an imetaja dalili nyingi mno, Rejea Suratul qiyaamah (75:6 – 9) na nyinginezo nyingi zilizotajwa katika hadith mbali mbali.
Kuamini siku ya mwisho ni kuamini kuwa kuna maisha ya milele baada ya maisha haya ya hapa duniani. Kwa mujibu wa mafundisho ya Qur-an, maisha hayo yatakuwa na hatua kuu nne zifu atazo:
(i)kutokwa na roho
(ii)Maisha ya kaburini - Barzakh.
(iii)Kufufuka na kuhudhurishwa mbele ya Allah (s.w) na kuhesabiwa.
(iv)Maisha ya kukaa Peponi milele kwa watu wema au kukaa motoni kwa watu waovu.Aidha kwa kuzingatia matukio yatakayotokea katika hatua nne za maisha yajayo,
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Bongolite - Game zone - Play free game 👉5 Dua za Mitume na Manabii 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Kujiepusha na kukaribia zinaa
Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa.
Soma Zaidi...Himizo la kuwasamehe waliotukosea
“Na wasiape wale wakarimu na wenye wasaa miongoni mwenu, kujizuia kuwasaidia jamaa zao, maskini na wale waliohama kwa ajili ya Dini ya Allah; na wasamehe na waachilie mbali (wapuuze yaliyopita).
Soma Zaidi...Ni lipi lengo la Elimu katika yislamu?
Ni lipi lengo kuu la Elimu katika uislamu (Edk form 1 Dhanaya Elimu)
Soma Zaidi...Nafsi ya mwanadamu inavyothinitisha uwepo wa Allah
Mwanadamu ukifikiria vyema. Kuhusu nafsi yako, hakika utapatabfikra yabuwepp wa Mwenyezi Mungu
Soma Zaidi...