Kuamini Malaika ni imani ambayo pindi ikithibiti vema moyoni, huleta taathira kubwa sana katika maisha ya kila siku na hivyo kubadili kabisa tabia na mwenendo wa Muumini.
Kuamini Malaika ni imani ambayo pindi ikithibiti vema moyoni, huleta taathira kubwa sana katika maisha ya kila siku na hivyo kubadili kabisa tabia na mwenendo wa Muumini. Hii ni kwa sababu:
1.Imani ya kweli juu ya Malaika humuepusha Muumini na kumshirikisha Allah (s.w) na viumbe vyake, hasa vile visivyoonekana, miongoni mwa hivyo ni Malaika na Majini.
2.Muislamu anaamini kuwa Malaika ni viumbe watukufu ambao wametakasika na dhambi na kila aina ya uchafu, lakini binaadamu amepewa daraja ya juu zaidi pindi atakapotimiza wajibu wake kama Khalifa wa Allah (s.w) hapa duniani. Imani hii humpelekea mtu kujitahidi upeo wa uwezo wake kuishi maisha yanayolingana na cheo hiki kikubwa, cheo ambacho Malaika walikitamani (Rejea Qur-an, 2:30)..
3.Muislam anaamini kuwa kila wakati na kila alipo yu pamoja na Malaika watukufu. Imani hii peke yake inatosha kumfanya mtu abadili tabia yake. Hii ni kwa sababu binaadamu ameumbwa na haya, kwa hiyo huhuzunika akifanya mambo maovu mbele ya watu na hasa mbele ya watu anaowaheshimu.
4.Muislamu anaamini kuwa Malaika hao sio tu kuwa wapo naye daima bali wanahudhurisha mbele ya Allah (s.w) kila anachokitenda. Imani hii ikithibiti moyoni humfanya Muislam ajitahidi kufanya mambo mema na ajitahidi kuepuka maovu.
5.Muislamu anajua kuwa Malaika sio tu hupendezwa na mema, bali pia humuombea mtu huyo anayefanya mema, maghfira kwa Allah (s.w) jambo ambalo humzidishia Muislamu hima ya kutenda mema daima na kujiepusha na maovu hata akiwa peke yake.
Umeionaje Makala hii.. ?
Malaika wamepewa kazi ya kumtumikia Allah(SW) kwa kumtukuza na kumtakasa, kama wanavyosema wenyewe:Hakuna yoyote miongoni mwetu ila anapo mahali pake mahususi.
Soma Zaidi...Ninichanzo cha Elimu? (EDK form 1 Dhanaya Elimu)
Soma Zaidi...Ni lipi lengo kuu la Elimu katika uislamu (Edk form 1 Dhanaya Elimu)
Soma Zaidi...Nabii Musa na Mama yake nabii Isa bi Mariam waliweza kuwasiliana na Allah nyuma ya pazia.
Soma Zaidi...Elimu ndiyo zana aliyotunukiwa mwanadamu ili aitumie kutekeleza majukumu yake kama Khalifa wa Allah (s.
Soma Zaidi...Mwanadamu hawezi kuishi bila dini, kwani dini imekusanya mfumo mzima wa maisha yake.
Soma Zaidi...(i) Kutiishiwa Upepo Qur'an inatufahamisha kuwa Nabii Sulaiman alitiishiwa upepo akaweza kuutumia apendavyo kwa amri yake.
Soma Zaidi...“Na wasiape wale wakarimu na wenye wasaa miongoni mwenu, kujizuia kuwasaidia jamaa zao, maskini na wale waliohama kwa ajili ya Dini ya Allah; na wasamehe na waachilie mbali (wapuuze yaliyopita).
Soma Zaidi...