Ni viumbe watiifu wasiomuasi Allah(SW)
Malaika ni viumbe watiifu kwa Allah(SW). Wakipewa amri ya kumuadhibu mtu muovu, hawagomi wala kumuonea huruma mtu huyo.Enyi mlioamini! Ziokoeni nafsi zenu na nafsi za watu wenu na moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Juu yake kuna Malaika w akali wenye nguvu.Haw amuasi Allah(SW) katika yale anayowaamuru, na wanatekeleza vile walivyoamrishwa.(66:6)
Wana elimu ya kutosha kutekeleza majukumu yao
Malaika wana elimu inayowawezesha kutekeleza majukumu yao bila ya kubabaisha. Elimu waliyopewa malaika ni sehemu ndogo sana katika ujuzi wa Allah(SW). Na wenyewe walikiri mbele ya Allah(SW)Wakasema: Utukufu ni wako! Hatuna elimu ila ile uliyotufundisha, bila shaka wewe ndiye mjuzi na mwenye hekima(2:32)
Malaika hawana jinsia ya kike wala ya kiume. Qur’an inawakosoa watu wanaodhani kuwa malaika ni wanawake. In a h oji:
Na wamewafanya malaika ambao ni waja wa Mwingi wa Rehma kuwa ni wanawake. Je wameshuhudia kuumbwa kwao(43:19).
Ni viumbe wenye mbawa
“Sifa zote njema ni za Allah, Muumba wa mbingu na ardhi. Aliyewafanya malaika kuwa wajumbe wenye mbawa mbili-mbili, na tatu tatu, na nne nne. Huzid is ha katika kuumba apendavyo. Bila shaka Allah ni mwenye uweza juu ya kila kitu”. (35:1)
Huweza kujimithilisha umbile la mwanadamu
Malaika huweza kujimithilisha kuwa kama wanadamu. Hufanya hivyo pale wanapotumwa na Allah(SW)kuleta ujumbe kwa watu maalumu. Kwa mfano, Bibi Maryam, mama yake nabii Isa(a.s), alijiwa na malaika katika umbo mithili ya mwanaume.Na mtaje katika kitabu, Maryam, alipojitenga na watu wake katika upande wa mashariki.
Tukampelekea Muhuisha sharia Yetu(Jibril) akajimithilisha kwake kwa sura ya binaadamu aliye kamilifu. (19:16-1 7)
Lengo la kuumbwa malaika
Lengo la kuumbwa malaika ni kumtumikia Allah(SW). Katika kutekeleza lengo la kuumbwa kwao, malaika hawana hiyari katika kutekeleza amri za Allah(SW), hufanya mambo yote vile anavyotaka Allah(SW).
..Hawamuasi Allah(SW) katika yale anayowaamuru, na w anatekeleza vile w alivyoamrishw a.(66:6)