(x)Wenye kuepuka lagh-wi

Waumini wa kweli waliofuzu hujiepusha na Lagh-wi. Lagh-wi ni mambo ya upuuzi yanayomsahaulisha mtu kumkumbuka Mola wake, yanayosababisha ugomvi au bughudha baina ya watu na yanayomsahaulisha mtu kusimamisha swala: Rejea Qur-an (5:91).


Mahala ambapo Allah (s.w) hakumbukwi, shetani huchukua nafasi. Michezo yote ni lagh-wi isipokuwa ile tu inayochezwa kwa kuchunga mipaka yote ya Allah (s.w) kwa lengo la kukuza ukakamavu na siha.