HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ALIYEZIMIA (CARDIOPULMONARYRESUSCITATION) AU CPR


Kuzimia ni hali ya kupoteza fahamu ambako kunaendana na kutokuhema. Ukikutana na mtu huyu usimkimbie. Kwanza msogelee karibu kisha hakikisha kama yupo hai ama laa. Kama yupo hai, kwanza angalia kama utaweza kupiga simu kituo cha afya, ama mtaalamu wa afya. Hakikisha maamuzi haya na utekelezwaji unafanyika haraka bila ya kuathiri hali ya mgojwa.



Baada ya kujiridhisha na maamuzi uliyochukuwa unaweza kuanza huduma ya kwanza, ya kumsaidia mgonjwa asiyepumua aweze kupumua. Hapa tutafanya huduma ya kwanza itambulikayo kama CPR. Hii ni huduma ya kwanza inayohitaji umkini wa hali ya juu. Lakini kwa ambaye hafahamu chochote kuna namna anavyotakiwa kufanya



1.mlaze mgonjwa kichalichali juu ya sehemu iliyo ngumu, isiwe sehemu inayobonyea kama kitandani


2.Punguza nguo zilizopo kifuani kwake, na kama ni mwanaume unaweza kumvua shati kabisa.


3.Bidua kidogo kichwa cake


4.Weke mkono wako wa mmoja juu ya mwengine, kisha iweka katikati ya chuchu za mgonjwa.


5.Anza kumbonyeza kifua chake kwa wastani wa mibonyezo 100 paka 120 kwa dakika moja. Yaani karibia mibonyezo miwili kwa sekunde.


6.Hakikisha unabonyeza kwa nguvu mpaka uone kifua cha mgonjwa kinapanda na kuchuka kutokana na mibonyezo yako.


7.Usizidishe nguvu kupitiliza ukavunja mifupa ya mgonjwa.


8.Enelea kufanya hivi mpaka utakapoona mgonjwa anweza kupumua.


9.Muwahishe mgonjwa kituo cha afya baada ya kuanza kupumua.