Somo hili linakwenda kukueleza jinsi ya kumfanyia huduma ya Kwanza kwa mtu aloanguka kifafa
HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEANGUKA KIFAFA
Kifafa kinaweza kumpata mtu muda wowte. Tafiti zinaonyesha kuwa kati ya watu 10 mmoja anaweza kupata kifafa katika umri wake japo ni mara moja.mara nyingi kifafa ninatokea ndi ya muda mchache. Kikawaida ndani yasekunde kadhaa mpaka dakika 4 na hakizidi dakika 5.
Sio lazima kumpeleka mgonjwa hospitali ama kuhitaji msaada wa daktari. Kifafa kinaweza kuondoka chenyewe. Kumbuka hapa hatuzungumzii kifafa cha mimba. Taka msaada wa daktari ama mgonjwa apelekwe hospitali kama:
1.Hajawahi kuwa na kifafa toka azaliwe
2.Anashindwa kuhema ama kutembea baada ya kifafa kuondoka
3.Kifafa kimeendelea kwa muda zaidi ya dakika tano
4.Mtu amepata kifafa kingine punde tu baada ya kurejea hali ya kawaida kutoka kwenye kifafa
5.Mtu ameumia wakati alipopata kifafa
6.Kama kifafa kimetokea akiwa kwenye maji
7.Mtu ana magonjwa ya kisukari, maradhi ya moyo ama ana ujauzito
Ili kumsaidia aliyepata kifafa unaweza kumpa huduma ya kwanza kwa kutumia njia kama:-
A.Mlaze mgonjwa chini palipo safi
B.Mlaze mgonjwa upande mmoja
C.Safisha eneo alilopo mgonjwa hakikisha hakuna vitu vyenye ncha kali ama chochote cha kumdhuru
D.Weka kitu kilaini kwenye kicha chake kama mto ama nguo
E.Kama amevaa miwani ivue, vua na tai ana legeza
F.Kama kifafa kitaendelea zaidi ya dakika 5 mpeleke kituo cha afya kilicho karibu.
Usifanye haya kwa mtu aliyeanguka kifafa
1.Ukimkamate ama kumzuia miguu na mikono eti asihangaike
2. Usiweke chochote kwenye mdomo wake
3.Usijaribu kumfanyia CPR
4.Usimpe kitu chochote cha kula ama kunywa
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Post hii inahusu zaidi njia za kuenea kwa ugonjwa wa Ukimwi. Ukimwi ni upungufu wa kinga mwilini.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi umuhimu wa uterusi, ni mfuko unayosaidia kumtunza mtoto akiwa tumboni mwa mama yake.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mbinu ambazo hutumika kuponyesha majeraha kwa haraka zaidi,tunajua majereha utokana na kupona kwa vile vidonda au kupona kwa sehemu ambayo imekuwa na majeraha kwa hiyo ili kuponyesha majeraha hayo tunapaswa kufanya yafuatayo.
Soma Zaidi...Huduma ya kwanza ni huduma anayopewa mgonjwa au mtu yeyote aliyepata ajali kabla ya kumpeleka hospitalini
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa asidi iliyo kwenye tumbo kwa kitaalamu huitwa HCL, ni asidi inayofanya kazi nyingi hasa wakati wa kumengenya chakula.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Aina ya choo kisichokuwa cha kawaida, ni dalili za choo ambacho siyo Cha kawaida, Ina maana ukiona dalili za choo Cha Aina hii ni vizuri kwenda hospitalini Ili kupata matibabu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi ratiba ya chanjo ya kuzuia Nimonia, hii ni chanjo inayozuia hasa hasa Magonjwa ya mfumo wa hewa kwa hiyo nayo upewa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea mambo ambayo hayawezi kuambukiza UKIMWI
Soma Zaidi...Posti hii inahusu njia mbalimbali ambazo utumika kupitisha chanjo, njia hizo utegemea na kazi ya chanjo kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...