Somo Hili linakwenda kukueleza sababu za kwanini mbu hawezi kuambukiza ukimwi
KWA NINI MBU HAWEZI KUAMBUKIZA HIV (UKIMWI)
? Tumekusha kuona na kujua kuwa mbu anaweza kuambukiza maradhi mengi na ya virusi kama zika. Na mradhi mengine kama malaria na homa ya bonde la ufa. Lakini kuna jambo linaumiza sana fikra za wasomaji. “kama mbu wanaweza kuambukiza maradhi hayo ya virusi, sasa ni kwa nini mbu hawezi kuambukiza HIV?”
? Kwa hakika swali hili linasumbua fikra za watu wengi sana. Tafiti nyingi za kisayansi zimefanywa ili kuthibitisha majibu sahihi na kuwaridhisha waulizaji. Ukweli ni kuwa mbu katu hawezi kueneza HIV. Na huu ni ukweli ambao haupingiki katu, lakini sasa ni kivipi?. katika makala hii nitakueleza jibu la swali hili katika namna tatu:-
? Mdomo wa mbu una sehemu kuu 6, katika hizo 6 nne hutumika kutoboa ngozi ya mwili wa kiumbe anachotaka kunyonya damu. Na sehemu 2 zilizobakia ni kwa ajili ya kunyonya damu. Katika sehemu 2 hizo mojawapo ni kunyonya damu na nyingine ni kupeleka mate kutoka kwenye mwili wa mbu na kuelekea kwenye mwili wa kiumbe kinachonyonywa damu. Mate haya hutumika kwa kuifanya damu isigande.
? Hivyo basi kitu ambacho kinatoka kwa mbu kwenda kwa kiumbe kinachonyonywa damu ni mate ya mbu tu, na si damu, kwani damu haiwezi kutoka kutoka kwa mbu kwenda kwa kiumbe kinachonyonywa. Tafiti zinaonesha kuwa mate kati hayawezi kuambukiza ukimwi, hata yawe ya mtu. Hivyo basi hata kama mate ya mbu yataingia kwa mbu kati hayawezi kuambukiza ukimwi kkama amebeba virusi.
? Virusi vya HIV vikifika mwilini mwa mbu vinaliwa na kupotea kabisa. Virusi vya HIV ili viendelee kuzaliana vinahitaji kupata T seli (T cell), lakini mbu hana seli aina hii. Hivyo virusi vinapofika kwa mbu, vinaliwa pamoja na damu na kupotea kabisa. Kwa sababu hii hakuna uwezekano wa virusi vya HIV kuingia kwenye mate ya mbu ambayo ndio huenda kwa kiumbe kinachonyonywa damu. Hii inaonyesha kuwa katu HIV haiwezi kusambazwa kwa mbu.
? hata kama virusi vya HIV vitaweza kuingia kutoka kwa mbu kwenda kwa kiume kinachonyonywa damu (japo jambo hili haliwezekani) hakua uwezekano wa kuambukiza HIV. Tafititi zinaonyesha kuwa ili damu ama mate ya mbu yasambaze HIV inahitajika ang’ate si chini ya mara milioni 10. Jambo hili kisayansi haliwezekani. Pia kummeza mbu aliyebeba HIV HAIWEZEKANI KUSAMBAZA HIV. Haka akipasukia kwenye jeraha la mtu katu damu yake haiwezi kuambukiza HIV.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi ratiba ya chanjo ya kuzuia Nimonia, hii ni chanjo inayozuia hasa hasa Magonjwa ya mfumo wa hewa kwa hiyo nayo upewa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu ya kuwepo kwa maumivu ya mwili kwa sababu tunaweza kuhisi maumivu kwenye sehemu za mwili kwa sababu mbalimbali kama tutakavyoona hapo chini
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea namna ambavyo mwili unapambana na maradhi
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi namna ya kutoa huduma ya kwanza kwa watu waliopata ajali. Ajali ni tukio lisilotarajiwa ambalo kinaweza kumkuta mtu yeyote, tunapotoa huduma ya kwanza tnazingatia rangi ambazo huwakilisha jinsi watu walivyoumia.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukujulisha njia za kushusha presha iliyopanda.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuchoma chanjo, ni njia ambazo utumika kutoa chanjo kwa watoto na watu wazima kwa utaratibu uliowekwa.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyezimia
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kazi ya chanjo ya Surua kwa watoto, ni Aina ya chanjo ambayo utolewa kwa watoto na kufanya kazi mbalimbali mwilini ambazo ni kumkinga mtoto asipatwe na magonjwa.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu namna ambavyo mwili unapambana na maradhi
Soma Zaidi...