Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu utaratibu wa lishe kwa wajawazito na wanaonyonyesha
8.UTARATIBU WA LISHE KWA WAJAWAZITO NA WANAONYONYESHA.Wamama wajawazito na wanaonyonyesha. Wanaonyonyesha na wajawazito wanahitaji kupata vyakula vyenye viinilishe vya kutosha ili kuwezesha ukuaji wa mtoto tumboni , utengenezwaji wa maziwa na kwa ajili ya afya zao wenyewe.Vyakula vya protini vinahitajika kwa mkiwango kikubwa ili kuwezesha mwili wa mama kujenga misuli vizuri , tishu katika mwili wake na mwili wa mtoto aliye tumboni. Utengenezwaji wa maziwa , usafirishwaji wa damu na ukuaji wa viungo vya mama na mtoto unahitaji protini. Hivyo wamama hawa wapewe protini kwa wingi.Vyakila vya folic asid na vitamini B vinahitajika kwa ajili ya kuwezesha kupunguza tatizo la kushindwa kujifunguwa kwa njia ya kawaida. Vyakula vya madini ya kashiam(calcium) ni muhimu kwa ukuwji wa mifupa ya mtoto aliye tumboni na kuimarika mwili wa mama pia. Kwani mjamzito asipopewa madini haya mtoto atatumia madini yaliyomo kwa mama na kumfanya mama awe na mifupa dhaifu katika kipindi hiki.Madini ya chuma ni muhimu katika utengenezwaji wa damu, halikadhalika mtoto anahitaji madini haya ili ayatumie katika wiki ya kwanza ya kuzaliwa. Madini ya zink ni muhimu katika kuwezesha kujifunguwa.(progression of labour) na ukuaji salama wa mtoto aliyoko tumboni.Wamama wajawazito wapewe vyakula vyenye kambakamba (dietary fiber}. Hivi vitamuwezesha kutopata tatizo la kukosa choo.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi imani potofu juu ya ugonjwa wa Ukimwi,ni Imani walizonazo watu wengi kuhusiana na ugonjwa wa Ukimwi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa asidi iliyo kwenye tumbo kwa kitaalamu huitwa HCL, ni asidi inayofanya kazi nyingi hasa wakati wa kumengenya chakula.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi hatari zilizopo kwa mtu mwenye uzito mkubwa,kwa sababu ya kuwepo kwa uzito mkubwa na pia unene usio wa kawaida usababisha mtu kuwa na matatizo mbalimbali hasa saratani za kila sehemu kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi mabadiliko katika umri wa kubarehe kwa wsichana, ni kipindi ambacho watoto huelekea ujana, utokea Kati ya miaka kuanzia Kumi na kuendelea.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi sababu za michubuko kwa watoto wanaozaliwa,ni sababu ambazo uweza kuchangia kuwepo kwa michubuko kwa watoto wanaozaliwa.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi namna ya kutoa huduma ya kwanza kwa watu waliopata ajali. Ajali ni tukio lisilotarajiwa ambalo kinaweza kumkuta mtu yeyote, tunapotoa huduma ya kwanza tnazingatia rangi ambazo huwakilisha jinsi watu walivyoumia.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sehemu ambazo zinapaswa kudungwa chanjo, hizi ni sehemu zile zilizopendekezwa kwa ajili ya kuchoma chanjo kwa kadiri ya kazi ya chanjo.
Soma Zaidi...