Navigation Menu



Historia ya Nabii Ismail katika quran

KKatika somohili utakwenda kujifunzahistoriaya Mtume Ismail Mtoto wa Nabii Ibrahim

HISTORIA YA NABII ISMAIL(A.S)

 

Ismail(a.s) ni mtoto wa kwanza wa Mtume Ibrahim(a.s.). Alizaliwa wakati uzee umekwishamfikia Ibrahim(a.s). Kama Qur’an inavyobainisha, katika umri huo wa uzeeni, MtumeIbrahiim(a.s) alimuomba Mola wake ampe mtoto mwema atakaendeleza harakati za Kiislamu.


 

“Ee Mola wangu! Nipe (mtoto awe) miongoni mwa watenda mema.” Ndipo tukampa habari njema ya (kuwa atapata) mtoto mpole. (Basi akapata. Naye ndiye Nabii Ismail).” (37:100-101).


 

Mtume Ibrahim(a.s.) aliletewa mitihani migumu miwili juu ya mtoto huyu. Mosi ni kule kuamriwa kumwacha yeye pamoja na mama yake katika bonde kavu lisilo na watu wala maji. Hilo lilikuwa bonde la Makka. Maji ya kisima zamzam yaliyo katika Msikiti wa Makka, aliyabubujisha Allah(s.w) kwa ajili ya Ismail na mama yake. Chem-chem hiyo imedumu hadi leo. Aidha, vilima vya Safa na Marwa vimepata umaarufu na kuwa miongoni mwa alama muhimu katika Uislamu, kutokana na kitendo cha mama yake Ismail Hajirah, kukimbia baina ya vilima hivyo katika jitihada za kumtafutia mwanae Ismail maji.


 

Mtihani mwingine alioupata MtumeIbrahiim(a.s) juu ya Ismail(a.s) ni kule kuamrishwa amchinje. Huu haukuwa ni mtihani kwa baba tu, lakini pia mtoto Ismail(a.s). Hebu fikiri ungekuwa katika hali gani, kama ungekuwa mahali pa Ismail(a.s). Baba yako anakwambia ameamrishwa na Allah(s.w.) akuchinje! Hakika ni mtihani mgumu ila kwa wale wanaonyenyekea kikweli kweli kwa Muumba wao.


 

Qur’an yatufahamisha kuwa Ismail alikuwa mpole na mnyenyekevu kwa Mola wake. Kwa hiyo hakusita kutoa nafsi yake kwa ajili ya Muumba wake. Bali alimhimiza baba yake amchinje kama Allah(s.w) alivyomuamrisha.


 

Basi alipofikia (makamu ya) kwenda na kurudi pamoja naye akamwambia: “Ee mwanangu! Hakika nimeona katika ndoto ya kwamba ninakuchinja. (Na ndoto ya Mitume ni Wahayi). Basi fikiri,waonaje?”Akasema:“Ee baba yangu! Fanya unayoamrish wa, utanikuta Inshallah miongoni mwa wanaosubiri”.(37:102).


 

Utii na unyenyekevu huu wa Nabii Ismail(a.s) ni kielelezo muhimu kwetu. Kwamba, amri ya Allah(s.w) ni lazima itiiwe kwa gharama yoyote ile ikiwa ni pamoja na roho zetu.

 

Kuinua Kuta za Ka’bah.

 

Kama tulivyoona katika maisha ya Mtume Ibrahim(a.s.), Nabii Ismail (a.s.) alishirikiana na baba yake kuinua kuta za Ka’abah ambayo ndiyo nyumba kongwe ya kufanyia Ibada na kituo kikuu cha kwanza cha harakati za Kiislamu duniani.


“...........Na tulimwusia Ibrahim na Ismail (tukawaambia): Itakaseni nyumba yangu kwa ajili ya wale wanaoyoizunguka kwa ajili ya kutufu na wanaokaa hapo na (kwa ajili ya) wanaorukuu na kusujudu hapo pia” (2:125).


 

“Na (kumbukeni khabari hii) Ibrahim alipoinua kuta za nyumba (hii ya Al-Ka’bah) na Ismail (pia) (wakaomba, wakasema): “Ee Mola wetu! Tutakabalie (amali yetu hii ya kujenga huu msikiti). Hakika wewe ndiwe Mwenye kusikia, na Mwenye kujua”. (2:127).


 

Ismail(a.s) na Taifa la Waarabu

 

Nabii Ismail(a.s) ndiye chimhuko la kabila la Quraysh. Baada ya kuachwa katika bonde la Makka lililokavu, Allah(s.w) alijaalia kupatikana maji na hatimaye watu kuhamia pale. Uhai wa mji ukaanza na kutokana na kizazi cha Ismail(a.s) wakapatikana Waarabu wa Hijaz (Saudi Arabia) ambao hufahamika kwa jina mashuhuri Banu Quraysh. Qur’an imemtaja Ismail(a.s) kuwa alikuwa Mtume mkweli wa ahadi aliyewausia watu wake swala na zakat.


 


“Na mtaje katika kitabu (hiki) Ismail. Bila shaka yeye alikuwa mkweli wa ahadi, na alikuwa Mtume, Nabii. Na alikuwa akiwaamrisha watu wake Sala na Zakat na alikuwa mridhiwa mbele ya Mola wake”. (19:54-55).


 

Qur’an hapa haimtaji Ismail kwa wema kwa vile alikuwa mtoto wa Mtume Ibrahim(a.s.), bali kwa vile alikuwa mtumishi wa Allah aliye mkweli, muamrisha mema na mkataza maovu. Nasaba hapa haikutajwa kabisa.


 

Baada ya MtumeIbrahiim(a.s) na mwanae Ismail kujenga upya Ka’bah na kutangaza Hija, walimwomba Allah(s.w) alete Mtume atokanaye na kizazi chao ambaye ataendeleza harakati za Kiislamu kama walivyofanya wao. Aidha walikiombea kizazi chao kiwe ni cha watu wanyenyekevu:


 


“Ee, Mola wetu! Utufanye tuwe wanyenyekevu kwako. Na miongoni mwa kizazi chetu (pia ufanye) umma mnyenyekevu

kwako. na utuonyeshe njia ya Ibada yetu na utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu.(2:128)


 


“Ee, Mola wetu! Waletee Mtume anayetokana na wao, awasomee Aya zako, na kuwafundisha kitabu (chako) na hikma na awafundishe kujitakasa (na kila mabaya). Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu Mwenye hikima” (2:129).


 

Dua hii ilikuwa kabuili. Ilipofika zama za kuletwa Mtume wa mwisho, Allah(s.w.) akamleta kupitia kizazi cha Bani Quraysh ambao wanatokana na Ismail(a.s). Ndiye Mtume wetu Muhammad (s.a.w.).

 

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Ismail(a.s)

 

Kutokana na Historia ya Nabii Ismail(a.r) tunajifunza yafuatayo:

(i) Kila Muislamu anatakiwa kumuomba Allah(s.w) amruzuku mtoto mwema atakayesaidia kupeleka mbele harakati za kuhuisha na kusimamisha Uislamu katika jamii.


 

(ii) Mtoto mwema anayependwa na Allah(s.w) ni yule anayewatii wazazi wake katika mambo ya kheri.


 

(iii) Mtoto mwema hujitahidi kushiriki katika harakati za kuusimamisha Uislamu katika jamii.


 

(iv) Amri ya pili ya Allah(s.w) inayotukabili baada ya ile ya kusoma(kutafuta elimu) ni kusimamisha swala na kutoa katika vile Allah(s.w) alivyoturuzuku, kisha kuamrisha familia zetu na jamaa zetu wa karibu kufanya hivyo kisha tuilinganie jamii nzima kufanya hivyo.


 

(v) Kusema kweli na kutekeleza ahadi ni katika tabia njema anayoiridhia Allah(s.w).


 

(vi) Inatupasa kumuomba Allah(s.w) atupe yaliyo mema katika kila jambo tunalolikusudia kufanya.


 

(vii) Kuwa tayari kutoa nafsi zetu kwa ajili ya Allah(s.w)kama alivyokuwa tayari Ismail(a.s) kuchinjwa na baba yake katika kutekeleza amri ya Allah(s.w)

Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-06-26 11:55:49 Topic: visa vya Mitume Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 284


Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

hHistoria ya Nabii Dhul-kifl
Katika makala hii tutakwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Dhul-kifl Soma Zaidi...

Hstora ya Nabii Yahya
Katika somo hili uatkwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Yahya Soma Zaidi...

Histora ya Nabi Zakariya
Katika somo hili utakwenda ujfunza kuhusu hslistoria ya Nabi Zakariya Soma Zaidi...

Historia ya Nabii Nuhu katika Quran
Katika somo hili utakwenda kujifunza historia ya Mtume Nuhu kulingana na melezo yaliyo kwenye Quran Soma Zaidi...

Hstoria ya Nabii Yusuf
Katika makala hii utakwenda ujfunzakuhusu historiaya Nabii Yufuf katika Quran Soma Zaidi...

Historia ya Nabii Idrisa
Katika somohili utakwenda kujifunza historia ya Nabii Idrisa (amani iwe juu yake) Soma Zaidi...

Historia ya Mtume Muhammad (s.a.w) wa ufup
Huu n ufupisho wa Historia ya Mtume Muhammad s.a.w. Tumekuandalia histori hii kwa urefu zaidi kwenye Makala zetu zinazofuata Soma Zaidi...

Historia ya Nabii Shu'aib
atika makala hii utakwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Shu'aib katika Quran Soma Zaidi...

Historia ya Mtume Lut
Katika somo hili utakwenda kujifunza historia yaMtume Lut kutoka katika Quran Soma Zaidi...

Historia ya Mtume Al-yasa’a
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu historia ya Mtume Al-yasa'a Soma Zaidi...