Baada ya Quraish kufeli mbinu zao za mateso, sasa wanaanza mbinu za diplomasi, wanajaribu kumshawishi Mtume kwa kumpa mali nauongozi
Mazungumzo ya Utbah bin Rabi'a na Mtume Muhammad (SAW)
Baada ya kusilimu kwa mashujaa wawili wenye nguvu, Hamzah bin Abdul-Muttalib na Umar bin Al-Khattab, mateso dhidi ya Waislamu yalianza kupungua. Watu wa Makkah walitambua kuwa kuendelea kuwatesa hakutawafanya Waislamu waache imani yao. Kwa hiyo, wakaanza kubuni njia mpya ya kushawishi. Wakuu wa Makkah walimshauri Utbah bin Rabi'a kumwendea Mtume Muhammad (SAW) na kumshawishi kwa ahadi za mali, cheo, na hata ufalme, mradi tu aache kuhubiri Uislamu.
Utbah alikutana na Mtume (SAW) na kusema: “Hakuna mwingine aliyewaletea watu wa Arabia msiba mkubwa kama wewe. Umeikashifu dini yetu, miungu yetu, na mababu zetu. Kama unataka mali, tutakupa utajiri mkubwa kuliko mtu yeyote wa Quraish; kama unataka kuwa kiongozi, tutakufanya mkuu wetu; na kama unahitaji matibabu, tutakuletea waganga wazuri."
Mtume Muhammad (SAW) alijibu kwa utulivu kwa kumsomea Utbah maneno ya Qur’an kutoka Surah Fussilat (41:1-5), akianza na:
"Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu. Hâ-Mîm. Ufunuo kutoka kwa Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu. Kitabu ambacho aya zake zimeelezwa kwa kina…"
Mtume (SAW) alisoma sura hiyo huku Utbah akisikiliza kwa makini, mpaka alipofika kwenye aya inayohitaji kusujudu, Mtume akasujudu. Kisha akamwambia Utbah: “Ewe Abu Al-Waleed, umesikia jibu langu, sasa unaweza kufanya utakavyo.” Utbah alirudi kwa viongozi wenzake wa Makkah na kuwaambia: "Sijawahi kusikia maneno kama hayo; hayana mashiko ya ushairi, uchawi, au uaguzi. Naomba msimwonee, mwacheni afanye atakavyo."
Hata hivyo, viongozi wa Quraish hawakushawishika. Walimcheka Utbah na kusema kuwa Mtume (SAW) alikuwa amemroga.
Katika simulizi nyingine, Utbah aliendelea kusikiliza maneno ya Mtume (SAW) hadi alipofika aya isemayo:
"Lakini kama wakigeuka, waambie: ‘Nimewaonya kuhusu Sa’iqa (kilio kikubwa, adhabu kali, radi) kama ile iliyoipata kaumu ya ‘Ad na Thamûd." [41:13]
Utbah, akiwa na hofu kubwa, alisimama na kumwomba Mtume (SAW) aache ili watu wa Quraish wasije wakaangukiwa na adhabu hiyo. Alirudi haraka kwa watu wake na kuwaambia yale aliyoyasikia, lakini walikataa kumsikiliza.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Katika somo hili utakwend akujifunz akuhusu Ndoa Mtume Muhammad baada ya Bi Khadija alimuoa Sauda kisha Aisha
Soma Zaidi...Baada ya mbinu nyingi za Maquraish kufeli sasa wanaamuwa bora tu wamuuwe Muhammad ili kukomesha kuendelea mafundishio bya dini mpya.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunz akuhusu miaka mitatu ya kulingania dini kwa siri na mambo yaliyojitokeza.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza historia fupi ya Abu Lahab
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza mchango mkubwa wa nyumba ya Arqam Ibn Abi AL Arqam katika historia nzima ya Uislamu
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza historia fupi ya Abadallah baba wa Mtume Muhammad ﷺ
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunz akuhusu habari ya kifo cha Bi Amina ambaye ni mama yake Mtume MUhammad ﷺ
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujfunz akuhusu historia ya Bi Khada mke wa kwanz awa Mtume Muhammad ﷺ
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunz akuhusu amri ya kulingania dini bila ya kificho, baada ya kulingania kwa siri kwa miaka mitatu
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu namna ambavyo wito wa ulingano ulipoenea na kuwafikia maquraish na washirikina
Soma Zaidi...