Hii ni historia ya Imamu Bukhary pamoja na kitabu chake cha sahihul Bukhari.
Kwa majina anaitwa Muhammad bin Isma'il Abu 'Abdallah al'Ju'fi anayejulikana kwa jina la "Imamu al-Bukhari." Alizaliwa 13 Shawwal, 194 A.H./21 Julai, 810 A.D. katika mji wa Bukhara huko Urusi, na alifariki 30 Ramadhan, 256 A.H./31 Agosti 870 .D. Hamu yake ya kuhifadhi Hadith aliipata bado akiwa mtoto wa umri wa miaka kumi na moja.
Alipofikia umri wa miaka kumi na sita alikwenda kuhiji Makka na kubakia humo humo kujifunza Hadith kwa wanazuoni mbali mbali. Baada ya kutoka Makka alikwenda Misr kisha Basra na sehemu nyingine za Asia ambapo alitembea huku na huku katika kujifunza na kukusanya Hadith kwa muda wa miaka kumi na sita.
Kazi yake ya miaka kumi na sita inaonekana katika kitabu chake mashuhuri kijulikanacho kwa jina la "Al-Jami'u al-Sahihi au Sahihi al-Bukhari".Kitabu hiki ndio kitabu cha kwanza cha Hadith kinachotemgemewa na Umma wa Waislamu baada ya Qur-an, kwa sababu ya uangalifu mkubwa uliochukuliwa na Imamu Bukhari katika ukusanyaji na uchambuaji wa Hadith zake.
Jumla ya Hadith alizokusanya ni 600,000 na katika hizo alihifadhi Hadith 200,000. Lakini kutokana na uangalifu na tahadhari kubwa aliyoichukua katika kuhakiki usahihi wa Hadith alizozipokea, ni Hadith 7,275 tu zilizotokea katika kitabu cha sahihi al-Bukhari. Kabla hajaikubali Hadith kuwa ni sahihi, ilibidi kwanza achunguze historia ya maisha ya kila mpokeaji wa Hadith hiyo kutokea kwa Mtume (s.a.w) mpaka kumfikia.
Imamu Bukhari amezipanga Hadith katika kitabu chake kufuatana na mada za fiq-h. Ameigawanya kazi yake katika juzuu tisini na saba na katika milango (sura) 3,450.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Kama tunavyojifunza katika surat ‘Alaq (96:4-5), chanzo cha elimu au mkufunzi wa binadamu ni Allah (s.
Soma Zaidi...عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم "مِنْ حُسْنِ إسْلَامِ الْمَرْءِ تَرْكُهُ مَ?...
Soma Zaidi...DUA ZA KUONDOA MAUMIVU MWILINI Katika uislamu Allah amejaalia dawa katika kufuata sunnah.
Soma Zaidi...hii ni orodha ya dua mbalimbali kutoka kwenye quran. Unaweza kuzitumia dua hizi kujipendekeza kwa Allah na kupata msamaha, neema na mengineyo.
Soma Zaidi...Zijue fadhila za kuomba dua, tambua umuhimu na mahimizo juu ya kuomba dua?
Soma Zaidi...