Hadithi Ya 27: Uadilifu Ni Tabia Nzuri
Hadithi Ya 27: Uadilifu Ni Tabia Nzuri
الحديث السابع والعشرون
"البر حسن الخلق"
عن النّوَّاسِ بْنِ سَمْعَانَ رضيَ اللهُ عَنْهُ عن النَّبي صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((الْبِرُّ حُسْنُ الْخُلُقِ، وَالإِثْمُ مَا حاكَ في نَفْسِكَ وَكَرِهْتَ أَنْ يَطَّلِعَ عَلَيْهِ النَّاسُ))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ .
وعن وَابصَةَ بْنِ مَعْبَدٍ رضي اللهُ عَنْهُ قالَ: قالَ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ((جِئْتَ تَسأَلُ عَنِ الْبِرِّ؟)) . قُلْتُ: نَعَمْ. قَالَ: ((اسْتَفْتِ قَلْبَكَ، الْبِرُّ مَا اطْمَأَنَّتْ إلَيْهِ النَّفْسُ وَاطْمَأَنَّ إلَيْهِ الْقَلْبُ، وَالإِثْمُ مَا حاكَ في النَّفْسِ وَتَردَّدَ في الصَّدْرِ وَإنْ أَفْتَاكَ النّاسُ وَأَفْتَوْكَ))
حَدِيثٌ حَسَنٌ، رَوَيْنَاهُ في مُسْنَدَي الْإِمَامَيْنِ أَحْمَدَ بْنِ حَنْبَلٍ وَالدَّارِمِيّ بِإِسْنَادٍ حَسَنٍ.
HADITHI YA 27 UADILIFU NI TABIA NZURI
Kutoka kwa An-Nawwaas Ibn Sam'aan رضي الله عنه ambaye alisema kuwa Mtume صلى الله عليه وسلم kasema:
Uadilifu ni tabia nzuri na udhalimu ni kile kitu ambacho huyumbayumba (chenye mashaka) katika nafsi yako na hupendelei watu kukitambua.
Imesimuliwa na Muslim
Na kutoka kwa Waabisah Ibn Ma'abad رضي الله عنه ambaye alisema:
Nilikuja kwa Mtume صلى الله عليه وسلم naye akasema:
Umekuja kuuliza juu uadilifu? Nikasema: Ndio . Akasema: Ushaurishe moyo wako. Uadilifu ni kile ambacho nafsi yako inakihisi shwari na moyo wako pia unahisi shwari, na udhalimu ni kile kinachoyumbayumba katika nafsi na kwenda na kurudi kifuani ijapokuwa watu wamekupa shauri lao la kisheria (kukipendelea).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 kitabu cha Simulizi 👉3 ai web app 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 web hosting 👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Wajbu wa wazazi kwa watoto wao
Wajibu wa Wazazi kwa Watoto Wazazi wanawajibu kwa watoto wao.
Soma Zaidi...Ni siku zipo huitwa Aiyami tashriq?
Aiyami ni wingi wa neno yaumi kwa maana siku. Kwenye uislamu Kuna masimu matukufu kama vile masimu ya tashriq. Je ni yapi hayo? Endelea na makala hii.
Soma Zaidi...Utofauti wa dua ya kafiri na dua ya muislamu katika kujibiwa
Posti hii inakwenda kukufundisha ni kwa nini dua ya kafiri inawwza kujibiwa wakati ya muumini haijibiwi.
Soma Zaidi...Al-Arba'uwn An-Nawawiyyah hadithi ya 1: Nia
huu ni mwanzo wa kitabu hiki cha Matn arbaina Naway
Soma Zaidi...Hatari ya kumshika mwanamke asiye halali yako.
Hpa utajifunza umuhimu wa kujilinda dhidi ya mambo yanayoweza kupelekea fitna na maasi. Uislamu umeweka mipaka ya heshima kati ya mwanaume na mwanamke ili kulinda moyo, tabia na maadili ya jamii.
Soma Zaidi...