HADITHI YA. 28 NAKUUSIENI KUMCHA ALLAAH NA TABIA NJEMA

HADITHI YA. 28 NAKUUSIENI KUMCHA ALLAAH NA TABIA NJEMA

Hadithi Ya 28: Nakuusieni Kumcha Allaah Na Tabia Njema

الحديث الثامن والعشرون

"أوصيكم بتقوى الله وحسن الخلق"

عن أبي نَجيحٍ الْعِرْباضِ بنِ سارِيَةَ رضي اللهِ عنه قال: وَعَظَنَا رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم مَوْعِظَةً وَجِلَتْ مِنها الْقُلُوبُ، وذَرَفَتْ منها الْعُيُونُ، فَقُلْنا: يا رسول اللهِ، كأَنَّهَا مَوْعِظَةُ مُوَدِّعٍ، فأَوْصِنا. قال:

((أُوصِيكُمْ بِتَقْوَى اللهِ عَزَّ وَجَلَّ، والسَّمْعِ والطَّاعَةِ، وإن تَأَمَّرَ عَلَيْكُمْ عَبْدٌ، فإنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ فَسَيَرَى اخْتِلافاً كَثِيراً، فَعَليْكُمْ بِسُنَّتي وسُنَّةِ الخُلفَاءِ الرَّاشِدِينَ المَهْدِيِّينَ، عَضُّوا عَلَيْها بالنَّواجِذِ، وإيَّاكُمْ ومُحْدَثاتِ الأُمُورِ، فإنَّ كلَّ مُحْدَثَةٍ  بِدْعَةٌ وَ كُلَّ  بِدْعَةٍ ضَلاَلَةٌ  وَكُلَّ ضَلاَلَةٍ فِي النَّارِ))  

رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ. 

 


HADITHI YA. 28 NAKUUSIENI KUMCHA ALLAAH NA TABIA NJEMA

Kutoka kwa Abu Najiih Al 'Irbaadh Ibn Saariyah رضي الله عنه  ambaye alisema kwamba:

Mtume صلى الله عليه وسلم  alituhutubia  hutuba ambayo nyoyo zetu zilijaa hofu na macho yetu yalitutoka machozi.  Tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu!, inaonyesha kama kwamba hii ni hutuba  ya kuaga, kwa hivyo tuusie.  Akasema (Mtume صلى الله عليه وسلم  )  nakuusieni kumcha Allaah سبحانه وتعالى  na kumtii kiongozi wenu hata akiwa mtumwa.  Yule atakayeishi (muda mrefu) ataona ikhtilaaf nyingi (migongano), kwa hivyo fuateni mwendo wangu (Sunnah) na mwendo wa Makhalifa walioongoka (Makhalifa wanne). Shikamaneni nazo kwa magego (kwa nguvu).  Na tahadharini na mambo mapya yanayozuliwa kwani kila jambo jipya ni uzushi, na kila uzushi ni upotofu, na  kila upotofu unapeleka motoni.

 

Imesimuliwa na Abu Dawuud na At Tirmidhi na wamesema ni Hadithi Hasan na Sahihi.



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sunnah Main: Dini File: Download PDF Views 1134

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 Kitau cha Fiqh    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Simulizi za Hadithi Audio    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Dua za kuwaombea wazazi

Kwenye Quran kuna duaambazo Allah ametufundisha tuziombe kwa ajili ya wazazi, familia na kwa ajili yetu wenyewe.

Soma Zaidi...
kuwa muaminifu na kuchunga Amana

Uaminifu ni uchungaji wa amana.

Soma Zaidi...
Nafasi ya Elimu na wenye elimu katika Uislamu

Nafasi ya elimu na mwenye elimu katika uislamu inaonkana katika maeneo yafuatayo: Kwanza, Elimu ndio takrima ya kwanza aliyokirimiwa mwanaadamu na Mola wake.

Soma Zaidi...
Dua za wakati wa shida na taabu

Hizi ni Dua ambazo unatakiwa uziombe wakati wa shida na taabu

Soma Zaidi...
MASHARTI YA KUKUBALIWA KWA DUA

MASHART YA KUKUBALIWA KWA DUA.

Soma Zaidi...