HADITHI YA 17

عَنْ أَبِي يَعْلَى شَدَّادِ بْنِ أَوْسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم قَالَ: "إنَّ اللَّهَ كَتَبَ الْإِحْسَانَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ، فَإِذَا قَتَلْتُمْ فَأَحْسِنُوا الْقِتْلَةَ، وَإِذَا ذَبَحْتُمْ فَأَحْسِنُوا الذِّبْحَةَ، وَلْيُحِدَّ أَحَدُكُمْ شَفْرَتَهُ، وَلْيُرِحْ ذَبِيحَتَهُ".
[رَوَاهُ مُسْلِمٌ].

Kwa mapokezi ya Abu Ya'la Shaddad bin Aws (Mwenyezi Mungu apendezwe naye), kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (amani na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema:

Hakika Mwenyezi Mungu ameamuru ihsan (ustadi, ukamilifu) katika vitu vyote. Kwa hivyo ikiwa mnaua basi uueni vizuri; na ikiwa mnachinja, basi chinjen vizuri. Na anoe (vyema) mmoja wenu kichinjio chake (kisu) na na asimpe mateso mnyama anayemchinja ”
[Muslim]