Chemsha bongo 22

imageimage
4.Punda Mjinga
Ni kwa nini Punda alichelewa kufika?
Kijana mmoja kwa jina la malikutwa alikuwa na punda wake. Alikuwa akimmbebesha mizigo na alipendelea kumpitisha kwenye njia ambayo huwa anavuka kamto kama maji. Hakika punda huyu alifurahia sana njia hii. Alikuwa akimbebesha chumvi. Punda yule alikuwa akifika kwenye mto huwa anajitotesha maji ama huoga kisha khuendelea na safari.

Siku moja alimbebesha mzigo wa sufi ala baada ya kuvuka mto kwa mwendo kama wa dakika 10, Punda alikuwa ameshoka sana, na alikuwa akitembea kidogo kidogo. Kwa hakika siku ile walifika usiku.

Unadhani ni kwa nini punda alichoka sana. Unafikiri ni kwa nini punda alipenda kuoga akifika mtoni?

Jibu.
Punda aligundua kuwa anapojitotesha mzigo wa chumvi hutota hivyo chumvi humung’unyikia kwenye maji. Hatimaye mzigo hupungua. Ila hakujuwa kuwa sio kila mzigo humung’unyika kwenye maji. Leo amebeba sufi ambayo hunywa maji, hivyo huongeza uzito wa mzigo.