fangasi wa kwenye Mdomo na koo
- Fangasi hawa wa kwenye mdomo watambulikao kama thrush ama oropharyngeal candidiasis wanaweza kuishi kwenye koo na tundu zima la koo kuelekea kwenye tumbo na hawa wanajulikana kama esophageal candidiasis ama candida esophagitis. Fangasi hawa ni maarufu sana kwa watu wanaoishi na HIV ana UKIMWI.
Dalili za fangasi hawa
- Kuwa na madoa meupe kwenye sehemu ya ndani ya shavu, ulimi, sehemu ya juu ya mdomo, na koo.
- Unahisi kama kuna pambai kwenye mdomo
- Kupetea kwa ladha ya unachokila
- Maumivu wakati wa kula ama kumeza
- Kupasuka na kuwa wekundu kwenye kona za mdomo
Walio hatarini kupata fangasi hawa:
Fangasi hawa si kawaida sana kuwapata watu wenye afya madhubuti. Ijapokuwa wapo watu ambao wapo hatarini sana kupata fangasi hawa kama watoto chini ya umri wa mwaka mmoja, na watu wenye matatizo ya kiafya kam wenye:-
- Watu wanaotumia meno bandia
- Watu wenye kisukari
- Watu wenye saratani
- Watu wenye HIV ama UKIMWI
- Watu wanaotumia dawa amazo zinakausha mdomo
- Watu wanaovuta sigara.
- Watu wanaotumia dawa za kupulizia za pumu
Njia ya kupambana na fangasi hawa:
Wengi wanaopata fangasi hawa ni wale ambao mfumo wao wa kinga umeathirika hivyo miili yao haiwezi kupambana vyema na mashambulizi. Hivyo kupambana na fangasi hawa hakikisha unaweka mwili wako katika hali njema ya kiafya. Muone daktari akuelekeze namna ya kuboresha afya yako. Pia piga mswaki kila unapotumia dawa ya kupulizia ya pumu. Wacha kuvuta sigara.