Mirathi katika jamii za kijahiliKatika jamii nyingi za kijahili kama vile jamii ya Waarabu kabla ya Mtume Muhammad (s.
Mirathi katika jamii za kijahili
Katika jamii nyingi za kijahili kama vile jamii ya Waarabu kabla ya Mtume Muhammad (s.a.w), watoto wadogo ambao hawajafikia baleghe, walemavu na wazee ambao hawakuwa na uwezo wa kupigana vita katika kuihami heshima ya familia na kabila kwa ujumla, hawakupata chochote katika mirathi. Aghalabu katika jamii zote za kijahili mwanamke akiwa binti au mke, au mama au katika uhusiano wowote ule kwa marehemu, hakuwa na haki yoyote ile katika urithi.
Badala yake wanawake wenyewe walifanywa mali ya kurithiwa kwa nguvu na ndugu wa marehemu au mtoto mkubwa wa kiume wa marehemu ambaye hakuzaliwa na huyo mama anayerithiwa. Waliwarithi kama wake au vinginevyo waliwaoza kwa wanaume wengine kwa nguvu kinyume cha ridhaa ya wajane hao. Kwa namna hii wanawake walirithiwa kama sehemu ya mali ya marehemu na waliuzwa na kununuliwa kama bidhaa. Uislamu umepiga marufuku tabia hii katika aya ifuautayo:
Enyi mlioamini! Si halali kwenu kurithi wanawake kwa jeuri. Wala msiwazuie (kuolewa na wanaume wengine) iii mpate kuwanyang 'anya baadhi ya vile mliiyowapa(Hapana ruhusa haya) isipokuwa wawe wamefanya uovu ulio wazi nakaeni nao kwawema " (4:19).
Wala msiwaoe wake waliowaoa baba zenu, ispokuwa yale yaliyokwisha pita. Bila shakajambo hili ni uovu na chukizo na ni njia mbaya. (4:22).
Umeionaje Makala hii.. ?
Hapa tunakwenda kuona jinsi ya kuzitathmini swala zetu.
Soma Zaidi...Fahamu darsa mbalimbali za fiqh kama swala, twahara, zaka pamoja na funga. Zijuwe sharti za swala, funga na zaka.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu,umuhimu na msisitizowa zakat na sadaqat katika uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Hizi ndio haki kuu tano unazopasa kumpatia Muislamu mwenzio.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza taratibu za kumkafini maiti wa kiislamu. Yaani kushona sanda yake na kumvisha.
Soma Zaidi...Uchumi wa uislamu umeweka taratibu mbalimbali katika kuchuma mali.
Soma Zaidi...Mtume amemfundisha kuwa watoto wafundishwe kuswali wakiwa na miaka saba na waadhibiwe wakiacha wakiwa na miaka 10
Soma Zaidi...