(iii) Adhabu ya Uzinifu
Katika Sheria ya Kiislamu mtu haadhibiwi mpaka atende kwa uwazi matendo yenye kuvuruga utaratibu na amani ya jamii. Mtu hataadhibiwa mpaka upatikane ushahidi wa wazi na wakutosha. Kwa upande mmoja, Sheria ya Kiislamu imeweka masharti magumu sana ya ushahidi wa makosa ya jinai, bali ushahidi wa kosa Ia zinaa ni mgumu zaidi. Ambapo mashahidi wa makosa yote ya jinai ni wawili, mashahidi wa zinaa ni wanne walioshuhudia kwa macho yao wakati kitendo kinafanyika.


Ushahidi katika sheria ya Kiislamu umewekewa masharti magumu iii kuwaokoa watu na hatia ya kuadhibiwa kwa makosa. Imesimuliwa na Aysha (La) kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Walindeni Waislamu kwa kila iwezekanavyo na matumizi ya Sheria dhidi yao. Mwacheni mkosaji atoke katika hatia kama atakuwa na haki ya kutoka. Kwa kiongozi kufanya kosa ?a kumsamehe mtu a?iye na hatia ni bora ku?iko kukosea kumuadhibu mtu asiye na hatia. (A t - Tirmidh).


Kwa upande mwingine, mara tu ushahidi wa kutosha utakapopatikana dhidi ya mkosaji, Sheria ya Kiislamu itatoa adhabu kalli sana ambayo haitamzuia tu muhalifu na kuendelea na kosa hilo, bali itawazuilia maelfu ya watu wengine ambao wangaliendea kosa hilo. Lengo Ia sheria ya adhabu katika Uislamu ni kuitakasa jamii na maovu na wala si kuwashawishi watu wafanye kosa na kuendelea kuwaadhibu tena na tena.Zinaa ni kitendo kiovu chenye kuathiri mno jamii. Mtu anayefanya kosa hili anauhakikishia ulimwengu kuwa unyama wake umemtawala kwa kiasi kwamba hastahiki kuishi katika jamii ya binadamu. Jamii ya wazinifu ni jamii duni kuliko jamii ya hayawani kimaadili. Kwa mtazamo huu, Sheria ya Kiislamu imetoa adhabu kali kwa wazinifu kama inavyobainishwa katika Qur'an:


Mzinfu mwanamke na mzinfu mwanamume mpigeni kila mmoja katika wao mj/eledi (bakora) mia. Wala isiwashikeni kwa ajili y 'ao huruma katika (kupitisha) hukumu hii ya Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na lishuhudie adhabu yao hii kundi ?a Waislam. (24:2).
Adhabu hii kulingana na Hadith ni kwa wale ambao hawajawahi kuoa au kuolewa. Baada ya kuchapwa viboko mia hutengwa na miji yao kwa muda wa mwaka mmoja kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:Ubadah bin Swamit ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Nisikilizeni, nisikilizeni. Hakika Allah ametoa adhabu kwa mzinfu mwanamke ambaye hajapata kuolewa na mzinfu mwanamume ambaye hajapata kuoa ni viboko 100 na kuhamishwa mjini kwa mwaka mmoja. Na adhabu ya mzinfu aliyeoa na aliyeolewa ni viboko 100 na kupigwa mawe mpaka kufa. (Muslim).Hadith hii pia imetufahamisha kuwa adhabu ya mzinifu mwanamke aliyeolowa au aliyewahi kuolewa au mzinifu mwanamume aliyeoa au aliyewahi kuoa ni kifo kwa kupigwa mawe. Katika Hadith nyingine tunajifunza kuwa Mtume (s.a.w) na Makhalifa wake walitoa adhabu hii kwa watu mbali mbali waliofanya kitendo hiki cha kinyama kidhalilishacho jamii. Miongoni mwa Hadith hizo ni hii ifuatayo:Ibn Abbas ameeleza kuwa Ma 'z bin Malik alikuja kwa Mtume (s.a.w) akasema kuwa amezini. Mtume (s.a.w) akamwambia: Labda umebusu, au umeshika au umeangalia tu. Akajibu (Ma 'z): 'Hapana, Ewe Mtume wa Allah ". Akamuuliza tena Mtume: Umezini na yeye? Akajibu; 'Ndio ". Kisha Mtume alitoa amri apigwe mpaka afe. (Bukhari)Sheria ya Kiislam ya adhabu ya mzinifu inatofautiana mno na sheria za jamii nyingine. Kwa mfano sheria ya Uingereza (British Law) ambayo ndiyo iliyorithiwa na nchi zote zilizotawaliwa na Uingereza na nchi yetu hii ikiwemo, haichukulii kitendo cha uzinifu chenyewe kama kilivyo kuwa ni kosa, bali kosa linapatikana pale kitendo hicho kitakapo fanywa kwa kumshika mwanamke kwa nguvu (ubakaji) au kitakapofanywa na mke wa mtu bila ya ridhaa yake au kwa hapa kwetu kitakaposababisha mimba kwa mtoto wa shule. Kwa maana nyingine katika sheria ya nchi uzinifu sio kitendo kiovu bali kina kuwa kiovu tu pale kitakapofanywa kwa nguvu au kitakapoathiri haki za wengine.


Kutokana na mtazamo huu sheria ya adhabu ya uzinifu ya nehi . ni lazima itofautiane sana na sheria ya Kiislamu dhidi ya kosa hili katika sheria ya nchi, adhabu ya ubakaji ni kifungo cha miaka thelathini (30), adhabu ya kukamatwa ugoni ni kumlipa fidia yule mume aliyeziniwa mkewe na adhabu ya kumtia mtoto wa shule mimba ni kumuoa au kumlea mtoto mpaka aweze kujitegemea. Adhabu kama hizi haziwezi kamwe kukomesha uzinifu bali huzidi kuupalilia. Kwa mfano, ukimtaka mke wa mtu ni kiasi cha kumuendea na kuwa tayari kumlipa mumewe fidia. Ni katika mtizamo huu zinaa imekuwa ni mtindo wa maisha na kitendo cha maendeleo katika jamii zetu hizi. Sera za kudhibiti uzazi zimewekwa katika jamii mbali mbali ili zinaa iendelee pasina kutokea mimba zisizohitajika.


Kinyume na mtazamo wanchi juu ya zinaa, katika maadili ya Kiislamu zinaa ni kitendo kiovu mno kinachoidhalilisha jamii na kuivuruga. Ni katika mtizamo huu, sheria ya Kiislamu imetoa adhabu kali sana kwa wazinifu iii iwe onyo kali kwa wakosaji na kwa jamii nzima kwa ujumla. Ndio maana katika nchi zinazosimamisha sheria hii huoni uzinifu kuwa mtindo wa maisha na hupati watu wanaougua magonjwa ya zinaa kama huu ugonjwa wa UKIMWI (AIDS). Utakuta ugonjwa wa UKIMWI umejizatiti katika maeneo yale ambayo zinaa imefanywa mtindo wa maisha.Adhabu kwa Wenye Kuwasingizia Wanawake Watahirifu kuwa Wamezini.
Kitendo chakuwasingizia wanawake watwaharifu kuwa wameZlnl nacho ni kitendo kiovu mno chenye kuivuruga jamii, kwani kumsingizia mwanamke uzinifu hakuishii tu kwenye kumvunjia he shima na hadhi yake bali huwahusu wazazi, ndugu, jamaa na marafiki. Wotc wanaomuhusu huvurugikiwa na mawazo na imani yao juu yake hupungua na unyumba huvunjika. Tunajifunza katika Qur'an na Hadith kuwa jamii ya Mtume (s.a.w) ilivurugikiwa na kuyumba wakati mke wa Mtume, Aisha (r.a), aliposingiziwa kuwa amezini na swahaba mmoja. Maonyo makali na makemeo kwa jamii kutoka kwa Allah (s. w) juu ya kitendo hiki kiovu tunayapata katika Qur'an, sura ya 24 aya 10-20. Kutokana na ubaya wa kitendo hiki cha kuwasingizia wanawake wataharifu kuwa wamezini, Sheria ya Kiislamu inatoa adhabu kali sana kwa wahalifu kama inavyobainishwa katika aya ifuatayo:


Na wale wanaowasingizia wanawake watwaharfu (kuwa wamezini) kisha hawaleti mashahidi wanne basi wapigeni mj/eledi (bakora) thamanini na msiwakubalie ushahidi wao tena) na hao ndio mafasiki (24:4).