Kujiepusha na Vishawishi vya Zinaa
Katika macho ya sheria kitendo cha zinaa kinahesabiwa pale wanapokutana kimwili mwanamume na mwanamke nje ya ndoa. Lakini katika maadili ya Kiislamu kitendo chochote kitakacho fanywa na mwanamume au mwanamke ambacho kitapelekea kuleta matamanio ya jimai nje ya ndoa, kinahesabiwa kuwa ni kitendo cha uzinifu wa ama yake. Kwa mfano mtu kumwangalia kwa matamanio mwanamke asiye kuwa mkewe, kufurahia tusi, uzuri wa sauti ya mwanamke asiyekuwa mkewe,kufurahia maongezi na mwanamke asiyekuwa mkewe au maharimu wake na kumtembelea mara kwa mara mwanamke asiyekuwa mkewe au maharimu wake atakuwa amefanya uzinifu kwa macho, masikio, ulimi na miguu yake.


Hapana sheria yoyote itakayomkamata kwa uzinifu, lakini muumini wa kweli atajihukumu mwenyewe na kujihesabu kuwa ni mkosaji mbele ya Allah (s.w). Hivyo atatubia kwa Mola wake na kujiepusha mbali na vishawishi hivi vya zinaa. Kuhusu zinaa ya viungo mbali mbali vya mwili Mtume (s.a.w) amesema:"Macho yanazini na uziniji wa macho ni mtazamo mbaya (kutizama kwa matamanio (evil look), mikono inazini na zinaa ya mikono ni kuvuruga amani (kufanya mabaya); miguu inazini na zinaa ya miguu ni kuendea maovu; uziniji wa ulimi ni maongezi mabaya au yasiyo maana; na uzinifu wa moyo (nafsi) ni matamanio mabaya. Hatimaye viungo vya sin vinathibitisha (kwa kuviunga mkono) au kuvikatalia.Mtazamo muovu ni hatari zaidi katika kuwapelekea watu katika kitendo cha zinaa. Katika Qur'an tunaamrishwa tujiepushe na mtazamo muovu katika aya zifuatazo: Waambie Waislam wanaume wainamishe macho yao (was it izame yaliyokatazwa), na wazilinde tupu zao, hili nitakaso kwao, bila shaka Mwenyezi Mungu anazo habari za yote wanayofanya Na waambie Waislam wanawake wainamishe macho yao, na walinde tupu zao (24:30-31).Utekelezaji wa amri hii umefafanuliwa katika Hadith mbali mbali za Mtume (s.a.w). Mtume (s.a.w) amesema: Mwana wa Adam! Mtazamo wako wa kwanza unasamehewa, lakini kuwa mwangalfu kuwa hutazami mara ya pili. (Al-Jassaas). Mtume (s.a.w) alimuusia Au (r.a):Ewe Au, usirudie mtazamo wa pili baada ya ule wa kwanza. Mtazamo wa kwanza unasamehewa lakini sio ule wa pili. (AbuDaud).
Jabir (r. a) alimuuliza Mtume kuwa atafanya nini endapo macho yake yatamwangukia mwanamke bila kudhamiria? Mtume (s.a. w) alimuelekeza kuwa ageuze macho yake pale pale. (Abu- Daud).Mwanamke kuonesha urembo wake na mapambo yake ni kitendo kiovu kinachoambatanishwa na mtazamo muovu. Hiki ni kishawishi kingine cha zinaa na wanawake wamekatazwa kufanya hivyo katika Qur'an: Wala wasidhihirishe viungo vyao isipokuwa vinavyodhihirika "(24:31). "Wala msionyeshe mapambo yenu kama walivyokua wakionyesha mapambo yao wanawake wa zama za ujahili (33:33).Sauti ya mwanamke ni kishawishi kingine cha zinaa endpao ataongea kwa kuilegeza. Hivyo wanawake Wakiislamu wanaonywa wasifanye hivyo: "... Kama mnamuogopa Mwenyezi Mungu, basi msilegeze sauti (zenu) mnaposema na wanaume) iii asitamani mtu mwenye ugonjwa moyoni mwake (kufanya mabaya na nyinyi) na semeni maneno mazuri' (33:32).Si sauti yake tu iliyokishawishi cha zinaa bali hata sauti ya mapambo ya mwanamke huwavutia wanaume na kuwapelekea kwenye fikra mbaya ya zinaa. Katika Qur'an wanawake wa Kiislamu wanakatazwa kudhihirisha sauti za mapambo yao:


Wala wasipige miguu yao (wasitingishe) iii yajulikane wanayoyaflcha katika mapambo yao (24:3 1). Manukato yenye harufu kali kwa wanawake pia ni kichocheo kingine cha zinaa. Mtume (s.a.w) kasema: Mwanamke anayetumia manukato na kupita mbele ya watu ni muovu. (At- Tirmidh). Uislamu umeweka tahadhari hizi na nyinginezo ambazo mtu binafsi, akizingatia inakuwa ni ngao madhubuti ya kuikinga jamii na uovu wa Zinaa.