Fahamu dawa ya kutibu kikohozi inayoitwa expectorant
Post hii inahusu zaidi dawa aina ya expectorant katika matibabu ya kikohozi,ni dawa ambayo usaidia au uzuia kikohozi kuendelea kutokea.
Dawa ya kutibu kikohozi.
1. Kama tunavyojua kwamba kikohozi ni ugonjwa ambao uwapata watu wengi na uleta usumbufu sana hasa kwa watoto na wazee, basi kwa kutumia dawa ya expectorant inaweza kutibu kikohozi kwa sababu dawa hii ufanya kazi kwa kuhakikisha makohozi na material yote yaliyomo kwenye mapafu yanatolewa na kufanya mapafu,koo kuwa huru.
2. Pia dawa hii inapoingia kwenye mwili uhakikisha kwamba sehemu ya kwenye mfumo wa hewa ambayo kwa kitaalamu huitwa bronchial inakuwa safi bila makohozi na inafanya makohozi yaliyozalishwa yanakuwa mepesi na kwa hiyo hata mgonjwa anapokohoa hapati shida zaidi na pia kwa kutumia dawa hii ya expectorant usaidia maumivu kupungua na matibabu yanaweza kuwa mepesi zaidi.
3. Dawa hizi ya expectorant ina maudhui madogo madogo kama vile kichefuchefu na kutapika na pia kwa mara nyingine mgonjwa anaweza kuhisi kubwa na usingizi au mwili kulegea wakati akiwa anatumia dawa hii kwa hiyo ni vizuri kabisa na kujua kwamba hizi ni dalili za kawaida kwa mgonjwa mwenye kutumia dawa hii.
4. Pia dawa hizi utumiwa na watu mbalimbali ambao wana kikohozi na kwa wale wenye shida au aleji na dawa hizi hawapaswi kuitumia kwa sababu wanaweza kupata matatizo yatokanayo na kutoelewana kati ya mtumiaji na dawa yenyewe.
5. Katika matumizi ya dawa hii ni kufuata utaratibu wa wataalamu wa afya dawa hizi haitumiki kiholela ila kabla ya kuanza kutumia ni vizuri kujua namna unavyopaswa kutumia, uitumia mara ngapi na kazi yake ni nini baada ya kujua hayo unaweza kuitumia na matokeo natumaini yatakuwa mazuri zaidi.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 ai web app 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 Dua za Mitume na Manabii 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 Kitabu cha Afya 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
dawa ya kutibu infection kwenye kizazi nisaidie doctor
Je unasumbuliwa na maambukizi na mashambulizi ya virusi na bakteria kwenye sehemu za siri ama via vya uzazi?. Posti hii inakwenda kuupa ushauri.
Soma Zaidi...dawa ya minyoo, dalili za minyoo na sababu na vyanzo vya minyoo
MWISHO Mwisho tunapenda kusema kuwa unapohisi una minyoo kutokana na dalili ambazo tumezitaja humu, nenda kituo cha afya ukapate ushauri zaidi.
Soma Zaidi...Ijue Dawa ya lignocaine
Posti hii inahusu zaidi dawa ya lignocaine kama mojawapo ya Dawa ambayo utumika wakati wa upasuaji.
Soma Zaidi...Dawa za mitishamba za kutibu meno
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za mitishamba za kutibu meno
Soma Zaidi...Dawa za Anesthesia katika kutuliza maumivu.
Unapotaka kufanyiwa baadhi ya matibabu unatakiwa kupewa ganzi ama nusu kaput ili kulifanyia usihisi maumivu. Dawa hizi zinajulikana na Anesthesia.
Soma Zaidi...