Basi tambua haya;-
61.Vyakula vya mafuta huchangia kwa kiasi kikubwa kupata maradhi ya moyo hususani shinikizo la juu la damu yaani presha ya kupanda au shambulio la moyo yaani heart attack. Sababu kuu ni kuwa vyakula hivi husababisha mgando wa mafuta kwenye mishipa ya damu na kuifanya mishipa hii iwe na tundu nyembamba za kupitishia damu. Na hapa ndio panapoleta shinikizo la damu la kupanda. Wataalamu wa fizikia (physics) wanatambua kuwa eneo likiwa dogo basi presha huwa kubwa. Yaani kwakuwa tundu za mirija zimekuwa nyembamba basi damu huwa na presha kubwa.

62.Uvutaji wa sigara huweza kuathiri afya ya mvutaji na hili halina tabu kabisa maana imeandikwa kwenye maboksi ya sigara na sigara zenyewe kuwa UVUTAJI WA SIGARA NI HATARI KWA AFYA YAKO. Ila pia ijulukane kuwa hata mtu aliye pembeni ya mvutaji anaathirika kwa kiasi pia.

63.Ni vyema kunywa maji yamoto hususani asubuhi au ukiwa na unaumwa. Hii ni kwa sababu maji yamoto hayahitaji kupashwa joto tumboni. Pia wataalamu wa afya wanasisitiza sana kunywa maji yamoto hasa wakati wa asubuhi.

64.Si vyema kulala na mauwa ya makopo ndani. Yaani kama umepanda mauwa kwenye makopo si vyema ukalala nayo ndani. Kwani mimea wakati wa usiku huvuta hewa ya oksijeni ambayo wanadamu huvuta. Hivyo kitendo hiki kitasababisha mminyano wa kugombea hewa wewe na mmea. Hivyo hewa huenda isitoshe kuhudumia mmea na wewe pamoja.

65.Ijapokuwa kukari na chumvi ni muhumu kwenye maisha yetu, lakini inashauriwa tusitumie sukari nyingi au chumvi nyingi. halikadhalika kwa wadoto sio jambo jema sana kupenda kuwapa vitu vya sukari kwa wingi kama pipi, peremende n.k. Kwani huenda vikasababisha madhara katika meno yake.

66.Ulaji ulio salama ni kati ya kushiba na kuwa na njaa. Yaani mtu anatakiwa kiafya asishibe sana kiasi cha kushindwa kujimiliki kama kukimbia n.k hivyo ali kwa ukati nakati.

67.Mtu anatakiwa ale kwa wakati alojiekea. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa miongoni kwa sababu za vidonda vya tumbo ni kutokula kwa wakati. Mwili huwa unakawaida ya kujua wakati wa kula ambao huwa unakulaga. Hivyo unapofika wakati ule kuna majimaji yanazalishwa ili kuliandaa tumbo. Na kama majimaji haya yasipokutana na chakula yanaanza kukwagua kuta za tumbo na kuleta vidonda kama hali hii itaendelea kwa mud mrefu.

68.Unywaji wa maji ni jambo la umuhimu sana kwa afya. Wataalamu wa afya wanasisitiza sana, kwani maji yanaweza kupunguza hatari za ugonjwa wa UTI, maumivuya kichwa na kurekebisha migongeo ya chakula tumboni.

69.Mtu anatakiwa atumie muda katika kutafuna chakula. Wataalamu wa Afya wanaeleza kuwa mmeng’enyo wa chakula huanza rasmi mdomoni ambapo vyakula vya wanga huanza kumeng’enywa. Hivyo kama mlaji hatatafuna vizuri huenda asipate virutubisho kwa usahihi.

70.Unaweza ukadhibiti maradhi mbalimbali na mengi kwa kupangilia kula tu. Kwa msaada wa kanuni za afya unaweza kupambana na matatizo mengi ya kiafya kwa kurekebisha ulaji na kula kama inavyotakiwa.. Kwa mfano

A)kizazi yaani nguvu za kiume
B)Kisukari
C)Saratani
D)Vidonda vya tumbo.

71.Sio vizuri kulala ukiwa unajiko la mkaa likiwa linamoto. Wataalamu wa elimu za viumbe wanaeleza kuwa moto wa mkaa unatumia gesi ya okijeni kuwaka na badala yake hutoa gesi ya kabon monoksaid. Gesi hii huweza kuungana na oksijeni kutengeneza kabondaioksaid. Hivyo hali hii itapelekea matumizi makubwa ya gesi ya oksijen ambayo mwanadamu atakuwa anatumia. Kama yupo chumbani anawza kukosa hewa kabisa ikiwa chumba ni kidogo.

72.Si vyema kuvaa nguo nyingi na za kubana. Watu wengi leo wanasumbuliwa na fangasi sehemu za siri na hujikuna sana. Wadudu hawa wanapenda sana sehemu za majimaji hasa za siri. Hivyo nguo nyingi husababisha jasho sehemu za siri na kuwafanya wadudu hawa kupata mazingira mazuri.

73.Si jambo jema kuvaa nguo mbichi hasa sile za ndani. Jambo hili kiafya si jema kwani linaweza kuwafanya fangasi waliopo sehemu za siri kukuwa vizuri na kumfanya mtu ajikune kwa muwasho.

74.Unapojisikia haja ndogo au kubwa ni vizuri kuwahi haraka kwenda kuitoa. Haja kubwa au ndogo inaweza kupelekea matatizo ya kiafya kama haitatolewa kwa muda unaotakikana.

75.Kuwahi kutoa haja kubwa kunaweza kupunguza athari za UTI kwani unapokojoa unawatowa wadudu wa UTI.

76.Haja kubwa ikichelewa kutolewa inakuwa ngumu kwani mwili utaendelea kufyonza majimaji yaliyopo kwenye haja kubwa. Haja hii ikiwa ngumu inaweza kusababbisha mipasuko au michubuko kwenye njia na kusababisha damu.

77.Sio jambo jena kubana upeop (ushuzi). Kwani upepo huu unatakiwa utoke nje kwa muda ule. Halikadhalika kijamii sio vyema kujamba mbele za watu.

78.Pindi ukipata majeraha si vyema kuvyonza damu kwa mdomo. Kwani damu ile sio salama. Ni damu ambayo imekusanya vitu vingi kama urea, seli, plasma, homone n.k. Hivyo si vyema kuila damu hii.

79.Unaposikia maumivu ya kichwa kunywa maji mengi, huenda ni kutokana na upungufu wa maji.

80.Ni vyema kupiga mswaki zaidi ya mara moja kwa siku. Na huu ni ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya ya kinywa.