picha

MAZINGIRZ

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

MAZINGIRZ

2.MAZINGIA
Mazingira yamekuwa leo ni sababu ya kupata maradhi mengi sana. Maradhi mengi yanayotupata kutokana na mazingira yetu yanaweza kusababishwa na uchafu wa mazingira. Ijapokuwa mazingira yanaweza kuwa safi na pia yakasababisha maradhi. Mazingira pia yanaweza kuwa msaada kwetu kwa kuweza kulinda na kuimarisha afya zetu. Ila kwa ufupi hapa tutazungumzia tuu mazingira yanavyoathizi afya zetu kuwa dhoofu.

Mfano mzuri ni maradhi ya malaria ambayo leo yamekuwa yakipelekea mamilioni ya vifo duniani hususani watoto waliopo chini ya umri wa miaka mitano. Malaria yanaenezwa na mbu aina ya anofelesi na mbu huyu ni jike. Mbu hawa wanazaliana sehemu zenye majimaji. Mbu hawa hawahitaji maji mengi sana, hapana hata tone moja linamtosha yeye kutaga na kutoa watoto. Mbu hawa wamekuwa wakipatikana kwenye mazingira yetu. Wataalamu wa afya wanaeleza usafi wa mazingira kama kufyeka nyasi na kufukia madimbwi ni katika njia za kupambana na maradhi haya.

Mfano mwingine ni m aradhi ya kipindupindu, haya yamekuwa yakisababishwa na bakteria ambao wanaingia mwilini kwa njia ya chakula. Mazingira yanaweza kuwa njia ya kuenezxa maradhi haya kama usafi wa mazingira hautazingatiwa. Nzi wanaweza kubeba vijidudu vya maradhi na kuvipeleka kwingine katika mazingira yasiyokuwa safi.

Maradhi ya mafua yamekuwa ji kawaida sana kwa nchi zilizopo kwenye tropic. Maradhi yaya yanaweza kupatikana sana kwenye mazingira yenye vumbi sana. Pia kupitia hewa kutoka mgonjwa kwenda mtu mzima. Hivyo tunaweza sema mafua yanaenezwa sana kwenye mazingira kupitia hewa.

--> Wataalamu wa afya wanaeleza maradhi mengi sana ambayo hupatikana kwenye mazingira yetu yakila siku. Mazingira haya yanaweza kuwa kwenye maji kama maradh ya kichocho, kwenye hewa kama kifua kikuu na mafua au mazingira ya chini kama vile maradhi ya kipindupindu.


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Jiunge nasi WhatsApp
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF Views 864

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 ai web app    

Post zinazofanana:

Dondoo za afya 41-60

Somo Hili linakwenda kukuletea dondoo mbalimbali za afya

Soma Zaidi...
DARASA LA AFYA, AFYA YA UZAZI, MARADHI NA LISHE BORA

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
TAHADHARI KWENYE VYAKULA ILI KULINDA AFYA YAKO

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
KITABU CHA MATUNDA

Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho

Soma Zaidi...
kitabu cha afya

Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho

Soma Zaidi...