Pisti hii inahusu zaidi dalili za mtoto mwenye Maambukizi ya ugonjwa wa Dondakoo, tunajua wazi kuwa ugonjwa huu uwashambulia hasa watoto wadogo ambao wako chini ya miaka mitano, kwa hiyo zifuatazo ni baadhi ya Dalili zinazoweza kujitokeza kwa watoto hawa.
Dalili za ugonjwa wa Dondakoo.
1. Kukoroma wakati wa kuingiza hewa.
Hii ni mojawapo ya Dalili ya kuwepo kwa ugonjwa wa Dondakoo kwa mtoto ambapo mtoto anapokuwa anaingiza hewa ndan huwa anakoroma hali hii utokea kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi kwenye koo, kwa hiyo walezi wa watoto wadogo wanapaswa kutambua Dalili hii mapema na kuchukua hatua, ingawa kukoroma kunaweza kufanana na mafua ya kawa ila kukoroma kwa maambukizi ya Dondakoo utokea pale hewa inapokuwa inaingia ndani .
2. Kiwango cha mapigo ya moyo kuongezeka.
Hii nayo ni mojawapo ya Dalili ya kuwepo kwa Maambukizi kwenye koo yanayosababishwa na bakteria kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi hasa ya mda mrefu na sehemu mbalimbali za moyo ushambuliwa ambazo ufanya mapigo ya moyo kwenda mbio na wakati mwingine kwa sababu ya kuwepo kwa homa pia usababisha mapigo ya moyo kuongezeka, kwa hiyo tunapaswa kutibu ugonjwa huu mapema ili kuepuka kuwepo kwa matatizo mengine.
3. Kuvimba kwa sehemu ya juu ya tezi.
Dalili hii ujitokeza kwa mtoto hasa hasa kama Ugonjwa umesbaa sana, matezi yanaanza kuvimba kwa sehemu ya juu, hali hii tunapaswa kuitafautisha na tonslis ambapo matezi ya chini ndo uvimba kwa hiyo tukiona tu matezi ya juu yamevimba na mtoto anashindwa kimeza vizuri moja kwa moja tunapaswa kutambua kuwa ni ugonjwa wa Dondakoo na kutafuta matibabu mara moja.
4. Vidonda kwenye koo na sauti kubwa nzito.
Kwa sababu ya Maambukizi kwenye koo, hali ya kooni ushambuliwa na kusababisha madonda ambayo uleta maumivu kwa mtoto kwa hiyo mtoto kushindwa kumeza na wakati mwingine kama ananyonya ushindwa kabisa kwa hiyo hali hii upelekea kuwepo kwa madonda ambayo usababisha sauti kubwa nzito, kama mtoto haongei utagundua pale anapolia ambapo sauti yake ibadilika kabisa, kwa hiyo walezi wanapaswa kugundua dalili hii mara moja na kupata matibabu.
5. Kupumua kwa shida na wakati mwingine kupumua haraka haraka.
Hii ni mojawapo ya Dalili ya kuwepo kwa Maambukizi kwenye koo ambapo koo linakuwa limearibiwa na bakteria na Maambukizi yanakuwa yameenea kwenye kifua ambapo kusababisha matatizo kwenye upumuaji na pengine mtoto upumua kwa haraka haraka.kwa hiyo tunapaswa kutofautisha kupumua kwa mafua ya kawaida na kupumua kwa sababu ya Maambukizi ya Dondakoo.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za presha ya kushuka
Soma Zaidi...Coma ni hali ya kupoteza fahamu kwa muda mrefu ambayo inaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali Jeraha la kichwa , Kiharusi, Tumor ya ubongo, ulevi wa dawa za kulevya au pombe, au hata ugonjwa wa msingi, kama vile Kisukari au maambukizi.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na mifuko midogo midogo, iliyobubujika ambayo inaweza kuunda kwenye utando wa mfumo wako wa usagaji chakula. Wao hupatikana mara nyingi katika sehemu ya chini ya utumbo mkubwa (koloni). Hali hiyo inajulikana kama Divert
Soma Zaidi...Makala hii itakwenda kukupa elimu juu ya maradhi haya ya ukimwi, dalili zake, tiba na kinga zake na mengineyo zaidi.
Soma Zaidi...Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na dalili za minyoo ya tumbo ambapo minyoo hawa husababishwa na mtu kula vyakula vichafu ambavyo havijaiva vizuri au maji machafu pia au bacteria.
Soma Zaidi...Hapa nitakueleza namna ambavyounaweza kupunguza hatari ya kupata maradhi ya ini. Kwa njia hizi unaweza kujikina wewe na wengineo na maradhi haya hatari ya ini.
Soma Zaidi...Homa ya ini yenye sumu ni kuvimba kwa ini lako kutokana na kuathiriwa na vitu fulani ambavyo umeathiriwa navyo. Homa ya ini yenye sumu inaweza kusababishwa na pombe, kemikali, dawa za kulevya au viongeza vya lishe.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi maambukizi kwenye nephroni, uweza kutokea kwenye figo Moja au zote mbili.
Soma Zaidi...