Ugonjwa wa Dondakoo na namna unavyoweza kuenea
Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa Dondakoo na namna unavyoweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.
Ugonjwa wa Dondakoo na namna unavyoweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.
1. Dondakoo ni ugonjwa unaosababishwa na sumu ya bakteria ambaye kwa kitaalamu huitwa corynebacterium diphtheria, bakteria huyu ushambulia sehemu za pua, koo na wakati mwingine maumivu kwenye masikio hali hii upelekea mgonjwa kushindwa kupumua na wakati mwingine kushindwa kumeza, kwa sababu ugonjwa huu usababishwa na bakteria kuna dawa mbalimbali za antibiotics zinaweza kuponya ugonjwa huu, antibiotics hizo ni kama vile penicillin au erythromycin.
2. Ugonjwa huu ushambulia hasa watoto na unaweza kusambaa kutoka kwa mtu mwingine kwa njia zifuatazo kama vile mtu akipiga chagua yale maji maji yakimgusa mtu mwingine hasa kinywani mtu huyo anaweza akapata, kwa hiyo wakati wa kupiga chafya tunapaswa kuwa makini au tunapopiga chafya tunapaswa kupigia kwenye vitambaa ili kuepuka kusambaza ugonjwa kutoka sehemu moja kwenda kwa mwingine, au kama mama au mlezi wa watoto wadogo wanapaswa kuwa makini sana wasije kuambukiza watoto.
3. Ugonjwa huu pia unaweza kusambaa kwa njia ya kutumia vitu vyenye bakteria kama vile kunywea maji kwenye kikombe au glass ya mtu mwenye Maambukizi, au kutumia kijiko bila kuosha kutoka kwa mtu mwenye Maambukizi kwa hiyo bakteria usambaa kutoka kwa mwenye Maambukizi kwenda kwa hasiye na Maambukizi, kwa hiyo kila mtu anapaswa kutumia vifaa vyake hasa hasa vile vinavyoongozwa moja kwa moja kinywani au ni vizuri kuosha vyombo kwa maji moto ili kuweza kuua wadudu wanaosambaza na Kuleta madhara.
4. Pia hawa wadudu wanaweza kusambaa kutoka kwa mtu mwingine kwa kutumia vitu kwa pamoja kama vile taulo na nguo zenye jasho kutoka kwa mtu mwenye Maambukizi na vile vile watu wanaokula peni, penseli na vfutio ambavyo vimetumbukizwa kinywani na mtu mwenye maambukizi na ambaye hana Maambukizi naye akija kutumia na kuweka mdomoni anaweza kupata, kwa hiyo kila mtu anapaswa kutumia vifaa vyake hasa kwa watoto ambao wako chekechekea wanapaswa kuangaliwa kwa makini ili kuepuka kuongeza kwa Maambukizi.
5. Kwa hiyo jamii nzima inapaswa kujua kuwa ugonjwa huu upo kwenye jamii na usipotibiwa mapema unaweza kuleta madhara makubwa kwa hiyo tunapaswa kuwapeleka watoto watoto wapewe chanjo mapema ili kuweza kuepuka madhara mbalimbali ambayo yanaweza kutokea pia jamii inapaswa kujua Dalili zote za ugonjwa huu ili kuweza kuwahi mapema kwenda hospitalini na pia watu wajifunze kujua jinsi ugonjwa huu unavyoenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 kitabu cha Simulizi 👉2 Dua za Mitume na Manabii 👉3 Madrasa kiganjani 👉4 ai web app 👉5 Kitabu cha Afya 👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
Matibabu ya vidonda vya kinywa (Canker sores) na nini cha kula.
Vidonda vya kinywa, vinavyojulikana kitaalamu kama aphthous ulcers au canker sores, ni changamoto ya kawaida inayoweza kusababisha maumivu makali na usumbufu wakati wa kula au kuzungumza. Blogu hii inatoa mwongozo wa kina kuhusu mbinu bora za matibabu, vyakula vya kuepuka ili kupunguza maumivu, na vyakula bora vya kuimarisha kinga ili kusaidia uponyaji wa
Soma Zaidi...Ni Nini husababisha kinjwaa kutoa harufu mbaya?
Posti hii inaelezea kuhusiana na sababu zinazosababisha kinjwa au mdomo kutoa harufu mbaya?
Soma Zaidi...Vidonda vya tumbo husababishwa na nini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu visababishi vya vidonda vya tumbo
Soma Zaidi...Namna ya kuzuia ugonjwa wa Homa ya inni.
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia ugonjwa wa Homa ya inni, ni njia ambazo utumiwa Ili kuepuka kusambaa kwa ugonjwa wa Homa ya inni kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine,
Soma Zaidi...Namna ya kumsaidia mtoto mwenye UTI
Post hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia mtoto akiwa na ugonjwa wa UTI.
Soma Zaidi...