Je na wewe ni katika ambao wanahitaji kujuwa dalili za mimba ndani ya wiki moja? kama ndio makala hii ni kwa ajili yako. Utakwenda kuona dalili za mwanzo sana za ujauzito toka siku za mwanzoni.
Mimba huweza kutungwa baada ya mbegu ya kiume kukutana na yai na kulirutubisha. Mchakato huu kiasili hufanyika katika tumbo la uzazi katika mirija ya falopia ya mama. Siku hizi teknolojia imekuwa, mimba inaweza kutungishwa nje na baadaye yai kurudishwa kwa mama na tayari kukuwa kama mtoto. Watu wengi wamekuwa wakisumbuka na kutafuta ujauzito. Makala hii itakuwa na maada katika nyanja hii ya afya ya uzazi.
Dalili za mimba maana yake ni kuona mabadiliko katika mwili wa mwanamke baada ya kushiriki tendo la ndoa. Mabadiliko haya yawe yamesababishwa na kutungishwa kwa yai. Mabadiliko ya homoni katika mwili wa mwanamke huweza kuzungumza mabo mengi kuhusu afya ya mwanamke huyo. Miongoni mwa dalili za mwanzoni za ujauzito ni mabadiliko ya homoni. Mabadilko haya ndiyo baadaye yanasababisha kichefuchefu, kupata harufu, na mengineyo.
JE NI ZIPI DALILI ZA UJAUZITO NDANI YA WIKI MOJA?
Mwanamke anaweza kupatwa na mabadiliko ndani ya wiki moja ya ujauzito. Mabadiliko haya anaweza asiyahisi kwani yamekuwa yakifanana na hali za kawaida. Hii husababisha mwanamke ajegunduwa kuwa ana ujauzito hadi pale atakapokosa siku zake. Hapa nitakuletea baadhi ya mabadiliko ambayo huweza kuonekana mwanzoni sana mwa ujauzito ambayo huweza kuashiria dalili za mimba changa ndani ya wiki moja.
1.Kuona damu kidogo yneye rangi hafifu. Damu hii inaweza kuwa ni kitone ama mabadiliko ya rangi kwenye nguo ya ndani. Huwenda pia asigundue damu hii hadi wakati anapojisafisha. Damu hii kitaalamu hufahamika kama implantation bleeding. Kwa baadhi ya wanawake wanaweza kuiona damu hii mwanzoni kabisa katika wiki ya kwanza.
2.Maumivu ya tumbo. Maumivu haya yanafanana na tumbo la chango. Yanaweza kuuma kwamuda kama unachomwa kisha yanakata. Yanaweza kufanya hivikwa siku kadhaa kisha yanapotea. Kwa wanwake wengine yanaweza kuchukuwa muda mfupi sana hata kwa siku moja ama mbili hivi, ila wengine hata wiki.
3.Kichwa kuwa chepesi na kuwa na maumivu ya hapa na pale. Mwanamke anaweza kuhisi kizunguzungu yaani kichwa kinakuwa chepesi sana. Hali hii huweza kuambatana na maumivu ya kichwa ama joto la mwili kuongezeka.
4.Kuhisi uchovu. Uchovu ni hali za kawaida ambapo kila mtu anaweza kuihisi hali hii. Kuna sababu nyingi za kuwa na uchovu.lakni kwa mwanamke mwenye mimba hana sababu maalumu. Yaani ghafla anaweza kuhisi uchovu ambao hauna chanzo.
5.Tumbo kujaa gesi na kujaa nakuwa gumu. Hali hii inaweza kuambatana na kupungua kwa hamu ya kula na kukosa choo. Mwanamke atahisi tumbo kuwa limejaa, akila kidogo ameshiba hii ni kwa sababu ya gesi. Gesi hii hutokea kutokana na mabadiliko ya homoni aliyonayo.
Kwa ufupi hizo ni baadhi tu ya dalili za mwanzo sana za ujauzito. Mabadiliko haya pia yanaweza kuwa si ujauzito hivyo kuashiria shida nyingine za kiafya kwa mfano. Kuna baadhi ya maradhi yenyewe yanaweza kuwa na baadhi ya dalili za ujauzito kama:-
1.Mabadiliko ya homoni
2.UTI
3.PID
4.Fangasi
5.Shida kwenye kizazi
Je ni siku ipi ya kushiriki tendo la ndoa upate ujauzito?
Ujauzito huweza kupatikana katika siku chache sana zisizozidi 10 katika mzunguko wa siku za mwanamke. Siku hizi zipo ambazo nimujarabu sana kutafuta ujauzito na nyingine sio sana. Hivyo kama unataka kutafuta ujauzito zinagtia yafuatayo:
1.Shiriki tendo la ndoa katika siku hatari zote ama ruka kwa mojamoja
2.Shiriki tendo la ndoa siku ambayo una hamu sanna
3.Shiriki tendo la ndoa utakapoona majimaji ya ukeni yameongezeka
4.Shiriki tendo la ndoa utakapoona joto la mwili wako limeongezeka, si kwa sababu unahoama ama ulilala n.k.
Umeionaje Makala hii.. ?
Upasuaji ni kundi la ki medical linalohusu kutoa kiungo kisichohitajika kwenye mwili.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi aina mbili za kifua kikuu, aina ya kwanza ni ile ya kawaida ambayo ushambulia mapafu na aina ya pili ni ile ambayo ushambulia sehemu mbalimbali za mwili kama vile kwenye limfu node, kwenye sehemu za moyo, kwenye uti wa mgongo, kwen
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za maumivu ya jino
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ya Tiba homoni, ni madhara- ambayo utokea kwa mgonjwa anayetumia homoni kama Tiba kwenye kutibu saratani.
Soma Zaidi...post hii inahusu zaidi ugonjwa wa kuishiwa damu kwa kitaalamu huitwa(Anemia) ni ugonjwa wa kuishiwa na damu mwilini na kusababisha maisha ya mtu kuwa hatarini
Soma Zaidi...Jipu la jino ni mfuko wa usaha unaosababishwa na maambukizi ya bakteria.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kujibu swali linalosema je ni bakteria aina gani husababisha igonjwa wa pumu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi tatizo la kushindwa kushuka kwa makende kutoka kwenye tumbo kwenda kwenye skolatumu(scrotum).
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na Magonjwa yanayosababisha madhara kwenye mapafu na kitaalamu hujulikana Ugonjwa wa Acute Respiratory Distress Syndrome (ARDS) hutokea wakati Majimaji yanapojaa kwenye vifuko vidogo vya hewa nyororo (alveoli) kwenye mapafu
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mfumo wa mwili ambao huhusika na kusafirisha damu ,virutubisho na takamwili.mfumo huu unajumuisha damu,mishipa ya damu na moyo.moyo husukuma damu kupitia mishipa ya damu na kufika maeneo yote ya mwili.
Soma Zaidi...