Menu



Dalili na ishara za shambulio la moyo

Posti hii inazungumzia kuhusiana na Dalili na ishara za shambulio la moyo. Shambulio la moyo huzuia damu yenye oksijeni kufika kwenye moyo hivyo hupelekea tishu kufa. Na Ugonjwa huu mtu akicheleweshewa matibabu huweza kupata mshtuko wa moyo mpaka kifo.

DALILI 

Daliliza na ishara za kawaida za Shambulio la Moyo ni pamoja na:

1. Shinikizo, kujaa au maumivu ya kufinya katikati ya kifua ambayo hudumu kwa zaidi ya dakika chache

2. Maumivu yanayoenea zaidi ya kifua chako hadi kwenye bega lako, mkono, mgongo, au hata kwenye meno na taya yako

3. Kuongezeka kwa vipindi vya Maumivu ya Kifua

4. Maumivu ya muda mrefu kwenye tumbo la juu

5 Upungufu wa pumzi

6. Kutokwa na jasho kwa wingi sana

7. Kuzimia na kupoteza fahamu.

8. Kichefuchefu na kutapika.

9.kuhisi mapigo ya moyo yanaenda haraka.

10.maumivu ya kichwa.

11.maumivu ya kifua

 

Namna ya Kuzuia

Hatua za kujikinga na  kuzuia shambulizi la moyo

1.Kuacha kuvuta sigara

2.Kufanya mazoezi ya mara kwa mara

3.Kupunguza unywaji wa pombe

4.Kubadilisha aina ya mlo. Kupunguza mafuta katika mlo na chumvi.

5.Kutumia mafuta ya samaki (omega-3 fatty acids)

6.Kuna utafiti unaosema kuwa uchangiaji damu hupunguza hatari ya magonjwa ya moyo hasa kwa wanaume.

 

Mambo ya hatari

Madhara ya shambulizi la moyo Ni Kama Yafuatayo

1.Moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure)

2.Matatizo katika mfumo wa mapigo ya moyo ambayo hatimaye hupelekea kifo

3.Shambulizi la moyo kurudia mara ya pili

4.Kifo cha ghafla.

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea

Ndio     Hapana     Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Views 1855

Share On:

Facebook WhatsApp

Post zinazofanana:

Dalili za vidonda vya tumbo

Vidonda vya tumbo no tatizo linalotokea baada ya kuta za tumbo au utumbo mdogo kuwa na vidonda,hutokea baada ya ukuta wenye ute unaozuia kemikali za kuyeyusha chakula unaitwa mucus kuharibika. Vidonda vya tumbo (peptic ulcers) imegawanyika katika ma

Soma Zaidi...
Minyoo na athari zao kiafya

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu minyoo na athari zao kiafya

Soma Zaidi...
Dalili za VVU

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za VVU

Soma Zaidi...
Dalili za moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure)

post inaonyesha dalili mbalimbali za Kushindwa kwa moyo, wakati mwingine hujulikana kama kutofaulu kwa moyo, hutokea wakati misuli ya moyo wako haisukuma damu kama inavyopaswa. Hali fulani, kama vile ateri nyembamba katika moyo wako (Ugonjwa wa ateri y

Soma Zaidi...
Matibabu ya fangasi

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu matibabu ya fangasi

Soma Zaidi...
Namna ya kuzuia Ugonjwa wa ini

Posti hii inaelezea namna na jinsi ya kujikinga au kuzuia Ugonjwa wa ini.

Soma Zaidi...
Njia za kupambana na fangasi

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kupambana na fangasi

Soma Zaidi...
Dalili za malaria

Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na mdudu kwa kitaalamu anaitwa Anopheles.na anasambazwa na mbu jike pale anapotafuta chakula hasa wakati akiwa na mimba. Mbu hawa hupenda kuishi kwenye mnyasi, madibwi haswa kwenye maji yaliyo simama.

Soma Zaidi...
Kiungulia na tiba zake kwa wajawazito.

Posti hii inahusu kiungulia kwa wanawake wajawazito na tiba yake, ni ugonjwa au hali inayowapata wajawazito walio wengi kwa sababu ya kuwepo kwa mabadiliko ya homoni wakati wa ujauzito.

Soma Zaidi...