Katika somo hili tutajifunza kuhusu CSS Filters — mitindo inayotumika kuhariri mwonekano wa picha, video, au elementi nyingine kwa kuongeza athari kama blur, brightness, contrast, grayscale, na nyinginezo. Hii huifanya tovuti kuwa ya kisasa, ya kuvutia, na yenye mwingiliano mzuri.
Filters hutumika zaidi kwa ajili ya kuleta athari za kimuonekano kwenye elementi. Unaweza kuzitumia kwa:
Picha (<img>)
Divs au background zenye content
Text (kwa baadhi ya filters)
CSS filters zinafanya kazi kama “kamera” inayopita kwenye lenzi maalum kabla ya kuonyesha kitu kwa mtumiaji.
filterFilter huandikwa kwenye CSS kwa kutumia property ya filter.
.element {
filter: blur(5px);
}
Unaweza pia kuchanganya filters nyingi:
.element {
filter: brightness(0.9) contrast(120%) grayscale(50%);
}
blur(px)Hufanya elementi au picha ionekane iliyofifia au haijawa wazi.
filter: blur(3px);
brightness(%)Hutawala mwangaza wa picha. 100% ni kawaida, zaidi ya hapo ni mwangaza zaidi.
filter: brightness(150%);
contrast(%)Hudhibiti utofauti wa rangi. 100% ni kawaida. Chini ya hapo hufanya rangi kufifia.
filter: contrast(80%);
grayscale(%)Hubadilisha picha kuwa nyeusi na nyeupe. 100% ni black & white.
filter: grayscale(100%);
invert(%)Hubadilisha rangi kuwa kinyume chake. 100% ni full invert.
filter: invert(100%);
opacity(%)Hufanya kipengele kuwa na uwazi (transparent). 0% ni kutoonekana kabisa.
filter: opacity(60%);
saturate(%)Hudhibiti nguvu ya rangi. 100% ni kawaida, chini ya hapo hupunguza saturation.
filter: saturate(120%);
sepia(%)Hutoa athari ya rangi za kahawia (rangi za zamani/kale).
filter: sepia(100%);
hue-rotate(deg)Huzungusha rangi kama kwenye duara la HSL. 180deg hubadilisha rangi kikamilifu.
filter: hue-rotate(180deg);
img {
filter: grayscale(100%);
transition: filter 0.5s ease;
}
img:hover {
filter: grayscale(0%);
}
➡️ Hapa, picha itaonekana nyeusi na nyeupe, lakini ikipigwa hover itarudi kwenye rangi zake halisi.
CSS filters ni njia nzuri ya kubadilisha mwonekano wa picha au vipengele kwa haraka na bila kutumia programu ya picha. Ni muhimu kutumia filters kwa kiasi ili zisilete usumbufu kwa watumiaji.
@font-faceTutajifunza jinsi ya kutumia fonts tofauti kutoka kwenye Google Fonts au fonts zako mwenyewe kwa kutumia @font-face.
Kazi ya filter: blur(5px) ni ipi?
a) Kupunguza ukubwa wa maandishi
b) Kuongeza mwanga
c) Kufifisha muonekano
d) Kupunguza opacity
grayscale(100%) hufanya nini?
a) Huongeza rangi
b) Hufanya picha kuwa nyeusi na nyeupe
c) Huongeza contrast
d) Hupunguza mwanga
Filter ipi hubadilisha rangi kuwa kinyume chake?
a) sepia
b) grayscale
c) invert
d) saturate
Kipi kati ya hivi si filter halali ya CSS?
a) blur
b) zoom
c) contrast
d) brightness
Ili kutumia filters nyingi kwa kipengele kimoja, unafanyaje?
a) Unaandika mara mbili
b) Unaweka filter zote ndani ya bracket
c) Unaziandika kwa nafasi moja moja
d) Hutakiwi kuchanganya filters
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili, utajifunza msingi wa mfumo wa Flexbox unaotumika kupanga elementi kwa usahihi ndani ya kontena. Utajifunza kuhusu display: flex;, pamoja na properties muhimu kama justify-content, align-items, flex-direction, na gap.
Soma Zaidi...Mfano wa kitu kinachoweza kumaba mtoto kooni ni kama chagula kigumu, pesa ya sarafu, kijiwe na mengineyo. Endapo hili litataokea msaada wa haraka unahitajika kwa ulazima.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ya kudhibiti mwonekano wa maandishi kwa kutumia fonti kwenye CSS. Utajifunza jinsi ya kubadilisha aina ya fonti, ukubwa, mtindo, unene, na mpangilio wa maandishi ili yaweze kuonekana kwa mvuto na usomaji bora.
Soma Zaidi...Katika somo hili uatkwenda kujifunza aina za css selectors
Soma Zaidi...Katika somo hili, tutajifunza kuhusu @import — amri inayotumika kuingiza faili moja la CSS ndani ya jingine. Tutaona namna ya kuitumia, faida zake, hasara zake, na tofauti kati yake na njia mbadala ya <link> ndani ya HTML.
Soma Zaidi...Katika somo hili, utajifunza vipengele vya juu zaidi vya Flexbox: flex-wrap, flex-grow, flex-shrink, na flex-basis. Pia tutajifunza jinsi ya kujenga muundo wa safu (rows) na nguzo (columns) kwa kutumia Flexbox layout.
Soma Zaidi...Katika somo hili, utajifunza jinsi ya kudhibiti muonekano wa sehemu ya nyuma (background) ya HTML element kwa kutumia CSS. Utaweza kuongeza rangi, picha, kuweka picha zisirudiwarudiwe, na hata kusogeza picha kwenye maeneo tofauti ya ukurasa.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya CSS, pia nitakujulisha kazi zake. Mwisho utatambuwa historia ya CSS toka kuanzishwa.
Soma Zaidi...Katika somo hili, utajifunza jinsi ya kudhibiti upana (width) na urefu (height) wa elementi katika CSS. Pia utaelewa tofauti kati ya max-width, min-width, na jinsi overflow inavyodhibiti tabia ya content inayoizidi element.
Soma Zaidi...Katika somo hili, tutajifunza jinsi ya kuleta miondoko na harakati kwenye tovuti kwa kutumia CSS Transitions na Animations. Hii itasaidia kuboresha muonekano na matumizi ya tovuti.
Soma Zaidi...