image

CSS - somo la 2: Jinsi ya ku weka code za css kwenye HTML

katika somo hili utajifunza jinsi ya ku install css kwenye ukurasa wa html

Utangulizi

Css ni kifupisho cha maneno cascading style sheet. Hii ni moja katika lugha za kompyuta ambazo hutumika katika kuboresha mtindo kwenye ukurasa wa wavuti. Hutumika kwenye HTML na XML. css ni style sheet angauage, hata hivyo haipo pekee kwenye kundi hili. Lugha nyingine za style ni kama:

 

Css ilianzishwa miaka ya 1990 na kuendelea. Historia a css imeanza punde tu baada ya tovuti ya kwnza kuchapishwa na watu wakaanza kutengeneza tovuti mbalimbali. Hivyo ikaonekana kunahitajika kuwepo na ubireshwaji wa muonekano.

 

Mwaka 1994 ndipo css ilianzishwa rasmi na Håkon Wium Lie na Bert Bos. Kutokea hapo css iliweza kukuw kwa kasi. Na kuanza kupata u maarufu. Mpaka sasa tupo toleo la 4 la css.

 

Kama nilivyotangulua kusema kuwa css hutumiaka kwenye HTML na xml katika course hii tutakwenda kujifunza kutumia css kwenye html. Tutajifunza kutumia style sheet kwneye xml kwenye course ya xml.

 

JINSI YA KU INSTALL CSS

Hakuna uhitaji wa ku install css ili uweze kuitumia kama zilivyo lugha nyingne. Unachotakiwa kufanya ni kuitumia moja kwa moja kwenye ukurasa wako wa wavuti kwenye html. Kuna njia kadhaa ambazo hutumika katika kutumia css kwenye faili la HTML. Njia hizo ni kama:-

  1. In line css: Hapa tuna andika css ndani ya mstari katika  faili la html.
  2. Internal css Hapa tutatumia css ndani ya faili la html.
  3. External css Hapa tunaandika css kwenye faili lingine kisha tuna iunganisha moja kwa moja
  4. Kwa kutumia javascript Katika njia hii tunanaitumia css kenye code za javascript.

 

Katika course hii tutakwenda kutumia njia hizo tatu za kwanza. Njia ya nne tutatjifunza kwenye course ya javascript level 1 na level 2.

 

In line css

Njia hii utakuwa na uzoefu nayo kwani tumesha itumia mara kadhaa kwenye course yetu ya html level  1 na level 2. Njia hii ni ile ya kutumia tag za css kwenye fali la html. Tag yenye we ni ile ya <style>. Kwa  kutumia tag hii ndani ya html itakuwezesha kuweza kuandika code za css na zikaweza kufanya kazi.

 

Katika inline css tutaandika css ndani ya tag ya html kw akuanza na neno style likifatiwa na attribute zake. Tutakwenda kutumia code hizi kwenye mfano huu:-

<html>

<head>

    <title>Bongoclass</title>

</head>

<body>

<p>Karibu bongoclass</p>

</body>

</html>


 

Mfano 1:

Tunataka kubadili nano karibu bongoclass kuwa na rangi ya buluu. Tutafanya hivi kwa kutumia in line css. Unachotakiwa kufanya ni kuweka style ndani ya tag ya <p>, ikifuatiwa na alama ya = kisha utaweka hizo attribute za css kwenye alama za kunukuu ().

 

Uandishi wa attribute utakuwa hivi, kwanza utaweka jina la property likifuatiliwa na nukta pacha (:) ama colon, Kisha utaandika value. Mfano ikitaka rangi iwe ya buluu utaweka style="color:blue" katika mfano huo hapo neno color ndio property na neno blue ndio value.

 

Hivyo tag ya html <p>itasomeka hivi <p style ="color:blue">Karibu bongoclass</p>

 

Pia unaweza kuweka style zaidi ya Moja kwenye inline css. Kufanya hivyo utatenganisha style Moja na nyingine kwa kutumia alama ya semicolon yaani  (;).

 

Mfano 2:

Katika mfano wetu huu tunataka kufanya maadhishi yawe makubwa kwa asilimia 200%. Kufanya hivi tutatumia property ya font-size kwa kuwa tunayo property ya color basi tutatenganisha kwa semicolon

 

<p style ="color:blue; fon">...



Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 398


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

CSS - somo la 4: Aina za css selecto
Katika somo hili uatkwenda kujifunza aina za css selectors Soma Zaidi...

CSS - somo la 1: Maana ya CSS, kazi zake na historia yake
Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya CSS, pia nitakujulisha kazi zake. Mwisho utatambuwa historia ya CSS toka kuanzishwa. Soma Zaidi...

CSS - somo la 3: syntax za css yaani sheria za uandishi wa css
Katika somo hili utakwenda kujifunza sheria za uandish wa css yaani syntax za css Soma Zaidi...

CSS - somo la 2: Jinsi ya ku weka code za css kwenye HTML
katika somo hili utajifunza jinsi ya ku install css kwenye ukurasa wa html Soma Zaidi...

CSS - somo la 5: Njia tano zinazotumika kuweka rangi kwenye css
Katika somo hili utajifunza aina tano za kuweka rangi kw akutumia css Soma Zaidi...