Katika somo hili, utajifunza jinsi ya kudhibiti muonekano wa sehemu ya nyuma (background) ya HTML element kwa kutumia CSS. Utaweza kuongeza rangi, picha, kuweka picha zisirudiwarudiwe, na hata kusogeza picha kwenye maeneo tofauti ya ukurasa.
Inatumika kuweka rangi ya nyuma ya element.
div {
background-color: lightblue;
}
Inatumika kuweka picha kama background ya element.
body {
background-image: url("picha.jpg");
}
Kwa kawaida picha ya background hurudiwa (repeat). Kama hutaki irudiwe, tumia:
body {
background-image: url("picha.jpg");
background-repeat: no-repeat;
}
Chaguo zingine:
repeat-x: Rudiwa upande wa mlalo
repeat-y: Rudiwa upande wa wima
repeat: Rudiwa pande zote (default)
no-repeat: Haijirudii
Inaelekeza picha iwekwe wapi. Mfano:
body {
background-image: url("picha.jpg");
background-position: center;
}
Chaguzi maarufu: top, bottom, left, right, center, au vipimo: 50px 100px
Inadhibiti ukubwa wa picha ya background.
body {
background-image: url("picha.jpg");
background-size: cover;
}
Chaguzi:
auto
cover: picha inajaza eneo lote
contain: picha inaingia yote ndani ya eneo
px/percentage kama 100px 200px
Inadhibiti kama background inabaki palepale au inasogea pamoja na ukurasa.
...
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili, tutajifunza kuhusu CSS Variables, au Custom Properties. Utajifunza jinsi ya kuunda, kuitumia, na faida za kutumia variables katika CSS ili kuweka msimamizi mzuri wa rangi, ukubwa, na mitindo mingine ya kurudia-rudia.
Soma Zaidi...Mfano wa kitu kinachoweza kumaba mtoto kooni ni kama chagula kigumu, pesa ya sarafu, kijiwe na mengineyo. Endapo hili litataokea msaada wa haraka unahitajika kwa ulazima.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ya kutumia float ili kupanga elementi upande wa kushoto (left) au kulia (right). Pia utajifunza jinsi ya kutumia clear kuondoa athari za float na kuhakikisha layout yako inabaki thabiti.
Soma Zaidi...Katika somo hili, tutajifunza kuhusu CSS functions muhimu zinazotumika kufanya mahesabu, kuweka vipimo vya kisasa vinavyobadilika kulingana na hali ya kifaa, na kutumia variables. Tutazingatia functions kama: calc(), clamp(), var(), min(), max(), na mwishoni tutajifunza jinsi ya kutengeneza custom function kwa kutumia variables.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza aina tano za kuweka rangi kw akutumia css
Soma Zaidi...Katika somo hili tutajifunza kwa kina kuhusu CSS Shorthand Properties — ni nini, jinsi zinavyofanya kazi, faida zake, na mifano mbalimbali ya kutumia shorthand kuandika CSS kwa njia fupi na bora zaidi.
Soma Zaidi...Katika somo hili, tutajifunza kuhusu @import — amri inayotumika kuingiza faili moja la CSS ndani ya jingine. Tutaona namna ya kuitumia, faida zake, hasara zake, na tofauti kati yake na njia mbadala ya <link> ndani ya HTML.
Soma Zaidi...Katika somo hili uatkwenda kujifunza aina za css selectors
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza kuhusu property muhimu ya CSS inayoitwa display, ambayo huamua jinsi element inavyoonyeshwa kwenye ukurasa. Tutachambua aina kuu za display: block, inline, inline-block, na none.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutajifunza kuhusu z-index, ambayo hutumika kudhibiti ni elementi ipi ionekane juu au chini wakati kuna elementi nyingi zinazofunika sehemu moja. Pia tutajifunza kuhusu stacking context, yaani jinsi vivinjari vinavyopanga
Soma Zaidi...