picha

Tembo ni katika wanyama wenye kushangaza sana.

Tembo wana maajabu makubwa kama utazingatia kwa umakini umbo lake zuri.

Tembo anaweza kufika urefu wa mita tatu (3) mpaka mita 4 yaani fkuanzia futi 10 mpaka 13. Tembo anaweza kufika uzito wa kilo elfu saba (kg 7000) yaani tani saba. Mimba ya tembo inaweza kuchukuwa miezi 20 mpaka 22 yaani miaka miwili kasoro miezi miwili.

 

Tembo mtoto ananyonya mpaka kufikia miaka mitatu mpaka minne. Tembo mtoto akiwa na umri wa miaka 10 uzito wake unaweza kufika kilo 900 mpaka 1,300. Tembo anaweza kuishi zaidi ya miaka 60.Inakadiriwa kuwa idadi ya tembo wote waliopo duniani leo ni kati ya laki nne mpaka tano (400,000 - 500,000).

 

Tembo anaweza kufundishwa na kutumika kwa shughuli kama kunyanyua mizigo ama usafiri. Tembo ana uwezo wa kusikia kwa umbali mrefu sana. Tembo hutumia mkonga wake wa ajili ya kuzungumza na wezie, kuwaonya na kuita mkutano. Pia hutumia mkonga wake kwa ajili ya kulia chakula, kuhifadhi maji ama kuoga. Tembo hutumia meno yake yaani mapembe kwa ajili ya kujilinda na kulinda familia yake dhidi ya wanyama walao nyama.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Mengineyo Main: Post File: Download PDF Views 1988

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Dua za Mitume na Manabii     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 web hosting     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zinazofanana:

The fastest (anakwenda mbio zaidi)

Posti hii inakwenda kukuletea sifa za mnyama anayekwenda mbio zaidi

Soma Zaidi...
Subscribe

Ingiza taarifa zako hapo chini uweze kupata Update zetu.

Soma Zaidi...
Historia fupi ya kuingia kwa wakoloni Tanzania

Hapa utakwenda kujifunza namna ambavyo ukoloni uliingia Tanzania na vipindi vyake. Utajifunza hatuwa ambazo ukoloni uliweza kupiti na hatimay kuitawala Tanzania

Soma Zaidi...