MAAJABU NA NGUZU ZA TEMBO
TEMBO Tembo ni katika wanyama wa porini na ndiye mnyama mkubwa kuliko wote.
TEMBO
Tembo ni katika wanyama wa porini na ndiye mnyama mkubwa kuliko wote.Tembo anaweza kufika urefu wa mita tatu (3) mpaka mita 4 yaani fkuanzia futi 10 mpaka 13. Tembo anaweza kufika uzito wa kilo elfu saba (kg 7000) yaani tani saba. Mimba ya tembo inaweza kuchukuwa miezi 20 mpaka 22 yaani miaka miwili kasoro miezi miwili.
Tembo mtoto ananyonya mpaka kufikia miaka mitatu mpaka minne. Tembo mtoto akiwa na umri wa miaka 10 uzito wake unaweza kufika kilo 900 mpaka 1,300. Tembo anaweza kuishi zaidi ya miaka 60.Inakadiriwa kuwa idadi ya tembo wote waliopo duniani leo ni kati ya laki nne mpaka tano (400,000 - 500,000). Tembo majike huwa wanaishi kwenye makundi. Kundi hili la tembo lina watoto na wakee wanawake pamoja na mashangazi. Kiongozi wa kundi hili la tembo ni yule mkubwa kuliko wote. Watoto wa kiume wa tembo wanapofika umri wa miaka 6 hujitenga na kundi hili na kutembea pekee. Tembo majike hukutana na tembo matume unapofika muda wa kupata watoto.
Tembo ni katika wanyama wenye nguvu kwani anauwezo wa kuweza kung’oa mti pamoja na mizizi yake. Wataalamu wa sayansi wanashangazwa na uwezo wa nguvu za tembo. Kwani anauwezo wa kunyanyua vitu vikubwa na pia kwa mkinga wake anaweza kunyanyua vitu vyepesi kama tunda au majani. Wataalamu wa sayansi wametengeneza vifaa kama magreda kwa kuiga nguvu za tembo lakini bado vifaa vyao ijapokuwa vinanyanyua vitu vizito lakini havina uwezo wa kunyanyua vitu vyepesi.
Tembo anaweza kufundishwa na kutumika kwa shughuli kama kunyanyua mizigo ama usafiri. Tembo ana uwezo wa kusikia kwa umbali mrefu sana. Tembo hutumia mkonga wake wa ajili ya kuzungumza na wezie, kuwaonya na kuita mkutano. Pia hutumia mkonga wake kwa ajili ya kulia chakula, kuhifadhi maji ama kuoga. Tembo hutumia meno yake yaani mapembe kwa ajili ya kujilinda na kulinda familia yake dhidi ya wanyama walao nyama.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 ai web app 👉2 Simulizi za Hadithi Audio 👉3 Kitabu cha Afya 👉4 Kitau cha Fiqh 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Kitabu Cha ayansi ya viumbe
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.
Soma Zaidi...Njia za Kutatua Migogoro Katika Ndoa
igogoro katika ndoa ni jambo lisiloepukika kutokana na ukweli kuwa wanandoa wawili ni watu tofauti wenye malezi, fikra, na matarajio tofauti. Hata hivyo, tofauti kati ya ndoa zinazostawi na zile zinazoshindwa si ukosefu wa migogoro, bali ni jinsi wanandoa wanavyoitatua. Makala hii inaangazia mbinu za kivitendo za kutatua migogoro ili kudumisha upendo na heshima.
Soma Zaidi...