Tembo

Posti hii inakwenda kukupa sifa za mnyama tembo

TEMBO

 

picTembo ni katika wanyama wa porini na ndiye mnyama mkubwa kuliko wote.Tembo anaweza kufika urefu wa mita tatu (3) mpaka mita 4 yaani fkuanzia futi 10 mpaka 13. Tembo anaweza kufika uzito wa kilo elfu saba (kg 7000) yaani tani saba. Mimba ya tembo inaweza kuchukuwa miezi 20 mpaka 22 yaani miaka miwili kasoro miezi miwili.

 

Tembo mtoto ananyonya mpaka kufikia miaka mitatu mpaka minne. Tembo mtoto akiwa na umri wa miaka 10 uzito wake unaweza kufika kilo 900 mpaka 1,300. Tembo anaweza kuishi zaidi ya miaka 60.Inakadiriwa kuwa idadi ya tembo wote waliopo duniani leo ni kati ya laki nne mpaka tano (400,000 - 500,000). Tembo majike huwa wanaishi kwenye makundi. Kundi hili la tembo lina watoto na wakee wanawake pamoja na mashangazi. Kiongozi wa kundi hili la tembo ni yule mkubwa kuliko wote. Watoto wa kiume wa tembo wanapofika umri wa miaka 6 hujitenga na kundi hili na kutembea pekee. Tembo majike hukutana na tembo matume unapofika muda wa kupata watoto.

 

picTembo ni katika wanyama wenye nguvu kwani anauwezo wa kuweza kung’oa mti pamoja na mizizi yake. Wataalamu wa sayansi wanashangazwa na uwezo wa nguvu za tembo. Kwani anauwezo wa kunyanyua vitu vikubwa na pia kwa mkinga wake anaweza kunyanyua vitu vyepesi kama tunda au majani. Wataalamu wa sayansi wametengeneza vifaa kama magreda kwa kuiga nguvu za tembo lakini bado vifaa vyao ijapokuwa vinanyanyua vitu vizito lakini havina uwezo wa kunyanyua vitu vyepesi.

 

Tembo anaweza kufundishwa na kutumika kwa shughuli kama kunyanyua mizigo ama usafiri. Tembo ana uwezo wa kusikia kwa umbali mrefu sana. Tembo hutumia mkonga wake wa ajili ya kuzungumza na wezie, kuwaonya na kuita mkutano. Pia hutumia mkonga wake kwa ajili ya kulia chakula, kuhifadhi maji ama kuoga. Tembo hutumia meno yake yaani mapembe kwa ajili ya kujilinda na kulinda familia yake dhidi ya wanyama walao nyama.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Mengineyo Main: Jifunze File: Download PDF Views 2281

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 web hosting    👉5 kitabu cha Simulizi    👉6 Dua za Mitume na Manabii   

Post zinazofanana:

Historia fupi ya kuingia kwa wakoloni Tanzania

Hapa utakwenda kujifunza namna ambavyo ukoloni uliingia Tanzania na vipindi vyake. Utajifunza hatuwa ambazo ukoloni uliweza kupiti na hatimay kuitawala Tanzania

Soma Zaidi...
Fast

Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta..

Soma Zaidi...
What is Bongoclass

What is Bongoclass and what does it do to the individuals and whole community.

Soma Zaidi...
ABOUT BONGOCLASS

learn English Vocabulary

Soma Zaidi...
Promo

Kama wewe ni Muandishi mzuri za hadithi au makala za kutoa elimu kwa watu na unataka kazi yako iwafikie watu wengi, au unataka kazi yako iweze kukuingizia kipato, Bongoclass ndio mtatuzi wako sasa.

Soma Zaidi...