Vitamini C Ni nini?

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana na historia ya vitamin C

VITAMINI C NI NINI?

 

 

Vitamini C ni katika vitamini muhimu sana katika mfumo wa kinga mwilini. Vitamini hivi vina sifa ya antioxidant. Antioxidant zenyewe ndani ya mwili ndizo ambazo husaidia kuupa mwili nguvu na kinga ya kupamba na na sumu, na vijidudu shambulizi. Vvitamini C ina pendelewa kuwepo ndani ya miili yetu kwa wingi muda wowote.

 

Maana na Historia ya vitamini C

Vitamini C kitaalamu pia hufahamika kama “ascobic acid” ama ascorbate. Vitamini C ni katika water soluble vitamini ambayo husaidia kukinga mwili dhidi ya maradhi ya kiseyeyee au kitaalamu scurvy. Ni maradhi hatari sana yanayodhurua afya. Kwa maelezo zaidi ya maradhi haya enelea kusoma makala hii.

 

Vitamini C vimegunduliwa miaka ya 1920 na Mwanasayansi aliyejulikana kwa jina la Albert von Szent Györgyi. Pia itambulike kuwa hapo mwanzo mwanasayansi aliyejulikana kwa jina la Kazimierz Funk yeye alieleza kuwa kuna maradhi yanasababishwa na upungufu wa virutubisho mwilini. Katika maradhi hayo aliyoyataja ugonjwa uitwao scurvy yaani kisehehe aliupa virutubicho kwa herufi C.

 

Baada ya ugunduzi wa Albert von Szent na haworth wakaipa herufi C kemikali iitwayo ascobic acid. Na hii ndiyo vitamini C. hivyo herufi C kwenye vitamini C ina maana ascobic acid hii ni tindikali. Wataalamu wa afya wanatueleza kuwa wanyama katu hawawezi kuishi bila ya vitamini C mwilini mwao.Vitamini C ndio vitamini vya kwanza kuweza kutengenezwa na binadamu kikemikali.

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Vyakula Main: Afya File: Download PDF Views 1681

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Bongolite - Game zone - Play free game    👉6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

VYAKULA VYA MADINI

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
Vyakula vya madini kwa wingi, na kazi za madini mwilini

Utajifunza vyakula vyenye madini kwa wingi, kazi za madini mwilini na athari za upungufu wake

Soma Zaidi...
Faida za kula magimbi (taro roots)

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula magimbi

Soma Zaidi...
UPUNGUFU WA VITAMIN NA MAJI

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula mihogo

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula mihogo

Soma Zaidi...
Karanga (groundnuts)

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula karanga

Soma Zaidi...
Nini maana ya protini

Unaijuwa maana ya virutubisho vya protini, na kazi zake mwilini. Soma zaidi hapa

Soma Zaidi...