Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula blueberry
Buluu beri (blueberry)
Ni katika matunda yanayotambulika kuwa na virutubisho vingi mwilini.. Tunda hili hutambulika kuwa na vitamini c kwa wingi, vitamini K na madini ya manganese. Pia tunda hili lina kambakamba yaani fiber. Itambulike kuwa vitamini C ni katika vitamini vinavyofanya kazi kubwa sana kulinda afya na kuupa mwili uwezo wa kupambana na maradhi kuliko aina nyinginezo za vitamini.
Pia tunda hili lina antoxidant kwa wingi. Hii husaidia katika kupambana na maradhi ndani ya mwili. Antoxidant huzuia mwili usipatwe na maradhi hatari shambulizi kama shambulizi la moyo, kisukari na mengineyo.
Tunda hili pia husaidia katika kufanya madhubuti mfumo wa kinga wa mwili yaani immune system. Wataalamu wamegundua kuwa tunda hili husaidia katika kuuwa seli yaani natural killer cell hali hii husaidia mwili katika kupambana na athari za stress yaani msongo wa mawazo pamoja na mashambulizi ya virusi yaani viral infections.
Pia tafiti za kisayansi zimeonesha kuwa tunda hili husaidia katika kuimarisha afya ya ubongo na utunzaji wa kumbukumbu. Husaidia tatizo la kupoteza kumbukumbu hasa kwa wazee. Tunda hili ni katika orodha ya matunda ambayo yanajulikana kwa uwezo wake wa kusaidia katika kutunza kumbukumbu na kuondoa tatizo la kusahausahau.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowSomo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula murajabu kea mwenye presha ya kushuka
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula nanasi
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi tiba ya lishe ya ugonjwa wa kisukari ni tiba ambayo utumiwa sana na wagonjwa wa kisukari na walio wengi na wamefanikiwa kupona
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula bamia
Soma Zaidi...Je ungependa kujuwa vyakula hivyo ama vyanzo vya madini? Na je ungependa kujuwa ni zipi hasa kazi za madini katika miili yetu?. makala hii ni kwa ajili yako, hapa utakwenda kujifunza mengi kuhusu somo hili.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu orodha ya madini chanzo chake na faida zake
Soma Zaidi...