SURAT AL-QURAYSH Sura hii ina majina mawili.
SURAT AL-QURAYSH
Sura hii ina majina mawili. Inaitwa Qureish na pia inaitwa Li ii laafi. Ibni Abbas anasimulia ya kuwa ilishuka Makka. Qureish ni jina la kabila lililotoka kwa Nadhir bin Kinana (Razi). Wengine wanasema neno Qureish limetoka katika neno Qarsh ambalo ni jina la samaki mkubwa wa bahari anayekula samaki lakini yeye haliwi. Hivyo kwa ukubwa wa kabila lao na kwa kuheshimiwa na watu wote nao wakaitwa Kureish. Makureish walikuwa watu wa Makka na walinzi wa Kaaba, na kwa sababu ya kuilinda Kaaba waliheshimiwa sana.
Sura hii imeshuka kwa maqurayshi kama alivyosema Mtume (s.a.w) βAllah amewapa neema Maquraysh ambayo hajampa yeyote kabla yao na hatampa yeyote baada yao: Ukhalifa umepewa mtu katika wao, uangalizi wa nyumba tukufu ya Allah umepewa mtu miongoni mwao, kazi ya kuwapa maji mahujaji imepewa mtu katika wao, utume umepewa mtu katika wao, wamepewa ushindi dhidi ya jeshi la tembo, walimuabudu Allah kwa miaka saba ambapo hakuna yeyote aliyekuwa akimuabudu Allah, na sura kwenye quran imeshushwa kwa ajili yao na hakuna yeyote aliyetajwa kwenye surahiyo ila wao (kwa kupewa jina la al-quraysh)
Umeionaje Makala hii.. ?
Hapa utajifunza maana ya Tajwid kilugha na kisheria. Pia nitakujuza jukumu ya kusoma tajwid.
Soma Zaidi...Sura hii inazungumzia kuhusu hali ya Abulahab namke wake wakiwa kama Watu waovu. Ni moja katika sura ambazo zilishuka mwanzoni toka Mtume alipoamrishwa kulingana dini kwa uwazi.
Soma Zaidi...Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa
Soma Zaidi...Ni zipi hizo herufi saba, na ni vipi viraa saba katika usomaji wa Quran
Soma Zaidi...SURATUL-MAMβUUN Imeteremshwa Maka, anasimulia Ibn Jurayj kuwa Abuu Sufyan ibn Harb alikuwa na kawaida ya kuchinja ngamia wawili kila wiki, hivyo siku moja yatima mmoja alikuja kwake na kumlilia shida, na hakumsaidia kwa chochote na hatimaye akampiga yat..
Soma Zaidi...Aina za idgham ni idgham al mutamathilain, na idgham al mutajanisain
Soma Zaidi...