Sababu za kushuka kwa surat al-Fiil

SURAT AL-FIILSura hii imeteremshwa Makkah na ina Aya Sita pamoja na Basmallah.

Sababu za kushuka kwa surat al-Fiil

Sababu za kushuka kwa surat al-Fiil

SURAT AL-FIIL
Sura hii imeteremshwa Makkah na ina Aya Sita pamoja na Basmallah. Sura hii imeshuka ili kueleza kuhusu tukio la kuangamizwa kwa jeshi la tembo. Na hii ni katika sura ambazo zinataja neema ambazo wamepewa Maquraysh, nao ni ule ushindi dhidi ya Makafiri walotaka kuvunja Al-Ka'abah. Tukio hili limeelezwa kwa kirefu kwenye vitabu vya Sirah na hapa nitaleta kwa ufupi zaidi



Kiongozi mmoja wa kiyemeni aliyetambulika kwa jina la Abrah aliona waarabu kutoka maeneo mbalimbali wanafunga misafara kuelekea Makkah kwa lengo la kwenda kuhiji. Hivyo akaamuwa kujenga kanisa kubwa sana ambalo alifikiri kuwafanya waarabu wasiende Makkah ila waende kuhiji kwenye kanisa lake. Kulikuwa na kijana mmoja kutoka katika kabila la Kinana alifahamu jambo hili la Abraha. Hivyo akaingia kwenye kanisa wakati wa usiku kisha akachafua ukuta wa kanisa kwa kuupaka vinyesi. Abraha alipolijuwa jambo hili akaandaa jeshi kubwa sana ili akaivunje Al-ka'aba. Jeshi la Abraha lilikuwa na washujaa elfu sitini (60,000). kisha akachaguwa tembo aliye mkubwa ndio akampanda yeye. Katika jeshi hili kulikuwa na tembo kati ya tisa mpaka kumi na tatu. (9-13)



Safari ya Abraha iliendelea mpaka akafika sehemu inayoitwa Magmas. Na hapo ndipo akaliweka sawa jeshi lake na akaliweka tayari kwa kuingia Makkah. Akaendelea mpaka akafika sehemu iitwayo Bonde la Muhassar bonde hili lipo kati ya Muzdalifah na Mina. Na hapo ndipo tembo wa abraha akakataa kuendelea na safari. Tembo alipiga magoti na kukaa chini, na kugoma kabisa kuelekea upande wa Makkah. Basi akimuelekeza upande mwingine anakubali lakini pindi akimuelekeza upande wa Makkah anagoma kabisa.



Na hapo ndipo Allah alipoleta jeshi la ndege waliobeba vijiwe vya moto na kuwapiga nvyo jeshi la Abraha. Ndege hawa kila mmoja alibeba vijiwe vitatu, kijiwe kimoja kwenye mdomo na viwili kwenye miguu yao. Kila kijiwe kiliuwa mtu katika jeshi la Abraha. Kuna wengine walikufa palepale na wengine walikimbia na kufia mbele ya safari. Abraha alibahatika kukimbia kwani alijeruhiwa vibaya, alipofika sehemu iitwayo San'a hali yake ikawa mbaya zaidi na akafariki.



Kwa upande mwingine wakazi wa Makkah walikimbia mji na kujificha kwenye majabali. Na huu ni ushauri walopewa na kiongozo wao Abdul Al-Muttalib. Baada ya maombi waloyaomba kwa Allaha na hatimaye wakamuachia Allah ailinde Nymba yake na wao wanusuru maisha yao. Basi jeshi la Abraha baada ya kuangamizwa wakazi wa Makkah wakarudi majumbani kwao wakiwa salama.



Tukio hili lilitokea mwezi wa Muharram siku hamsini aua hamsini na tano kabla ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w) ambapo ni sawa nan Mwezi wa Pili au mwanzoni mwa Mwezi wa Tatu mwaka 571 B.K. na hii ilikuwa ni zawadi kutoka kwa Allah kwenda kwa mtume wake na watu wa familia yake. Na hapo ndipo Nyumba ya Allah yaani Al-ka'aba ilipata maarufu kwa utukufu wake. Na mwaka huu waarabu wakauita mwaka wa Tembo



                   



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 130


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Kisa cha Malkia wa Sabaa.
Sabaa ulikuwa mji katika nchi inayojulikana leo kama Yemen. Soma Zaidi...

NAMNA ZA ZAKA (AINA NA MGAWANYIKO WA ZAKA) ZAKA IPO MAKUNDI MANGAPI?
Soma Zaidi...

Kuingia Kwa Uislamu Tanzania na Afrika Mashariki
Soma Zaidi...

HUKUMU ZA KUSOMA QURAN, HUKUMU ZA TAJWID, HUKUMU ZA NUN SAKINA, MIM SAKINA, QLQALA NA IQLAB, TANWIN NA MADA
Soma Zaidi...

DUA ZA SWALA
DUA ZA SWALA 1. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Isa(a.s)
Kutokana na Historia ya Nabii Isa(a. Soma Zaidi...

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat Al-Anfal (8:2-4) na Al-Hujurat
"Hakika wanaoamini kweli ni wale ambao anapotajwa Allah nyoyo zao hujaa khofu; na wanaposomewa aya zake huwazidishia imani na wanamtegemea Mola wao tu basi. Soma Zaidi...

Wajbu wa wazazi kwa watoto wao
Wajibu wa Wazazi kwa Watoto Wazazi wanawajibu kwa watoto wao. Soma Zaidi...

Dua Sehemu ya 01
Zijue fadhila za kuomba dua, tambua umuhimu na mahimizo juu ya kuomba dua? Soma Zaidi...

Hadithi inayokataza bidaa (bid's) uzushi katika dini
' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ': ': ' ' ' ' ' ' ' "... Soma Zaidi...

Usiku wa lailat al qadir maana yake na fadhila zake. Nini ufanye katika usiku wa lailat al-qadir
Soma Zaidi...

Haki na Wajibu wa mume kwa mkewe na familia
Soma Zaidi...