Tafsir ya suratul quraysh na mafuzoyake

Tafsir ya suratul quraysh na mafuzoyake

Tafsir ya suratul quraysh na mafuzoyake

Naomba Tafsir ya suratul quraysh na mafuzoyake



Namba ya swali 000

Suratul-Quraysh (106)

Kwa jina la Allah,mwingi wa Rehma, Mwenye Kurehemu.
1.Ili kuwafanya Makurayshi waendelee.


2.Waendelee na Safari zao za wakati wa kusi (kwenda Yemen) na wakati wa kaskazi (kwenda Shamu).


3.Basi nawamuabudu Bwana wa nyumba hii (Al-Kaaba).


4.Ambaye anawalisha (wakati Waarabu wenzao wamo) katika njaa, na anawapa amani (wakati wenzao wamo) katika khofu.



Namba ya swali 000

Mafunzo yake je?



Namba ya swali 000

Mafunzo kwa Muhtasari



Kutokana na sura hii kwa muhtasari tunajifunza yafuatayo:
(1 )Neema zote zilizotuzunguka zinatoka kwa Allah (s.w).



(2)Amani, usalama na ustawi wa kweli hupatikana kwa kumtii Allah (s.w) ipasavyo. Kwa mfano amani na ustawi wa Makka ulipatikana kutokana na dua ya Nabii Ibrahim (a.s) ambaye kwa kumtii Mola wake aliacha familia yake mahali pakavu na papweke pasipo na msaada wowote wa kibinaadamu. Wakati anatekeleza amri ya Allah (s.w) ya kuiacha familia yake pale, Nabii Ibrahim (a.s) aliomba:



"Mola wetu! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya kizazi changu (mwanangu Ismail na mama yake, Hajar) katika bonde (hili la Makka) lisilokuwa na mimea yoyote katika nyumba yako takatifu. Mola wetu! Wajaalie (wawe) wasimamishaji swala. Na ujaalie nyoyo za watu zielekee kwao na uwaruzuku matunda ili wapate kushukuru" (14:37)



3)Mahusiano, maingiliano na mawasiliano baina ya mataifa katika nyanja mbalimbali za kijamii ni katika neema za Allah (s.w)



Namba ya swali 000

Shukraa, Allah akuzidishie Elimu



Namba ya swali 000

Aaamin Nawe pia ndugu yangu, Allah akupe Neema nyingi



Namba ya swali 000

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Quran Main: Post File: Download PDF Views: 4896

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
πŸ‘‰1 Dua za Mitume na Manabii     πŸ‘‰2 kitabu cha Simulizi     πŸ‘‰3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     πŸ‘‰4 Kitau cha Fiqh     πŸ‘‰5 web hosting     πŸ‘‰6 Kitabu cha Afya    

Post zinazofanana:

Aina saba za Viraa vya usomaji wa Quran

Post hii inakwenda kukuorodheshea aina saba za viraka vya usomaji wa Quran.

Soma Zaidi...
HUKUMU ZA MIIM YENYE SAKINA (MIIM SAKINA)

HUKUMU ZA MIYM YENYE SAKNA : Mym sakina ni miym ambayo haina i’rab ( Ω…Ω’).

Soma Zaidi...
IDGHAAM KATIKA LAAM

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka surat al Quraysh

Qurayh ni jina la kabila la Mtume Muhammad S.A.W. Sura hii itakwenda kukujulisha neema ambazo Maquraysh wamepewa na hawataoewa wao wowote baada ya wao.

Soma Zaidi...
Hukumu ya Ikhfau katika tajwid

Ikh-fau ni moja ya hukumu za nun sakina na tanwin kwenye hukumu za Quran tajwid

Soma Zaidi...
MAANA NA HUKUMU YA TAJWIDI

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

Soma Zaidi...