NDOA YA UTATA KISIWANI Mfalmee wa serendib alipouona msafara ule alivutiwa sana.
NDOA YA UTATA KISIWANI
Mfalmee wa serendib alipouona msafara ule alivutiwa sana. Alitamani kijana yule awe mkwe wake. Mfalme aliamini kuwa mtoto wake hata kataa. Lakini mfalme alikuwa akijiuliza je kama ni masikini si mawaziri watanicheka. Mfalme alikuwa anatarajia awe mtoto wa waziri ama awe ni mtoto wa tajiri yeyote angalau aendane na mwanaye. Sasa kwa kuwa mfalme leo yupo pale hakuna haja ya kuomba ruhusa kwa mlolongo. Mke wa Kamaralzamani aliyejifanya ndie kamaralzamani mwenyewe akapiga goti mbele ya mfalme na kujieleza kuwa yeye n mtoot wa mfalme wa peshia naomba ruhusa ya kakatiza kwenye kisiwa chako.
Mfalme alistaajabi kwa kuraha kuona sasa amepata mkwe. Kumbe ni mtoto wa mfalme. Akaagiza aletewe kijana huyo kwenye kumbi za kifalme wapate chakula pamoja. Halikuwa jambo gumu kwani watu wote walizania bibie nurat ni yupo kwenye gari la farasi na huyu ndie kamaralzamani mwenyewe. Katika ukumbi wa kunywea chai, binti wa mfalme wa Serendib naye aliitwa kwa siri kuja kunawisha wageni. Lengo la mfalme ni kutaka kukutanisha watu hawa. Basi viti vikapangwa vyema, wageni wakaingia kwa ajili ya chakula. Bibie Nurat akawadanganya watu wake walinde gari la farasi na haruhusi mtu kuchungulia kwani mtoto wa Mfalme yumo mule.
Katika ukumbi wa chai, binti mfalme wa serendib Naira Khan alishindwa kutembea kwa mshangao. Hivi kumbe kuna wanaume wazuri hivi. Alishangaa sana, aliamuwa kurudi ndani kwa haraka na kuanza kujiwazia. Baba aligunduuwa hali hiyo na kuomba wageni wake waendelee. Moja kwa moja akaenda kwa bint yake na kumwambia “Mwanangu Naira nimekuletea mchumba je umekubwali”. naira Khan alimrukia baba yake na kumkumbatia kwa furaha “baba nimekubali nataka hata iwe sasa hivi”. baada ya mazungumzo mfalme akarudi kwa wageni wake. Chai ilipoisha akaomba kuzungumza na kamaralzamani faragha. Mazungumzo yako yalikuwa ni mfalme kumuomba Kamaralzamani awe mkwe wake. Kila bibie Mtaotao wa Sulatania lipokuwa anajaribu kukataa alishindwa. Hovyo kumsitiri mume wake aliubali. Wakati huo mfalme hakujuwa kabisa kuwa anayeongea nae ni mwanamke na si mwanaume.
Hali ikawa hivyo , Nurat mtoto wa Sultani wa nchi za chini alipata awazo kuwa alipopote;lea mume wake sio mbali sana na pale. Hivyo akiwa na madaraka maeneo yale itakuwa ni rahisi kwake limtafira mume wake popote alipo. Maana mumwe wake asingeweza kwenda Peshia bila ya kupita pale. Basi ilibidi afanye makubaliano na nairat mtoto wa mfalme wa Srendib. Alimueleza kila kitu na kumwambia kuwa jinsi anavyomuona yeye ndivyo alivyo Kamaralzamani. Kuthibitisha kauli hii watu wote pale walikuwa hawajui kuwa Kamaralazamani mwenyewe hayupo pale. Basi walifanya makubalianao ya doa kuwa Nairat atakuwa mke mdogo pindi kamaralzamani atakapopatikana, pia walikubaliana kuwa kwa pamoja watalinda siri ile mpaka atakapokuja mwenyewe. Walikubaliana mambo mengine kadhaa.
Basi baada ua kwenda Peshia walibalia pale Serendib na kufanya nmdoa ya kifahari kubwa sana katika kamaralzamani wa uongo na Nairat bint mfalme wa Serendib. Watu mbalibali walihudhuria katika shnguli hii ya harusi. Ni miezi 6 sasa imepita bila ya taarifa zozote za Kamaralzamani. Mfalme wa Serendib akaanza kumuuliza mwannembona mapaka sasa hawajapata mtoto. Maswali haya yalikuwa yakimuumiza sana lakini aliheshimu makubaliano yao. Kwa upande wa kamaralzamani alikuwa muadilifu na mtiifu sana wa yule mzee anayeishi kwake. Aliweza kufaya kazi zotezakutunza bostani la matunda na kwenda kuuza matunda.
Siku moja akiwa kwenye bostani ghafla akaona kunguru wawili wakipigana. Ilikuwa ni ugomvi mkubwa sana ambao hakupatapo kuuona. Kunguru wale walipigana hata mmoja akafariki. Alipofariki yule mmoja akawa anamtoboa mwenzie utumbo na kuula. Ghafla kamaralzamani akaona kitu kinametameta. Loo ulikuwa ni ule mkufu wake. Mara ukaanguka kutoka kwenye mdomo wa kunguru. Bila ya kupoteza muda alaenda kuuwahi na kuukumbatia. Kwa furaha aliubusu mara 100. alitambuwa kuwa sasa furaha inakaribia.
Siku hiyo hiyo akiwa kwenye bostani alihisi kama kuna shimochini. Akafukuwa akakuta kuna kama zega. Alipochimuwa akakuta kuna viande vingi vya dhahabu vimefukiwa. Kaenda kumueleza mzee wale yule mzee akasema kuwa vile vipande sio vyake. Hivyo wakakubaliana wagawane. Mzee alichukuwa vitano na vilivyobaki vyeote akamuachia kijana. Siku hiyo kamaralzamani alijihisi kuwa maisha yote ni ya kwake. Siku inayofaya akapata habari kuwa kuna marekebu pya inatarajia kuanza safari yake ya kwanza kuelekea serendib. Hii ilikuwa ni marekebu iliyokuwa ikitengenezwa kisiwani pale. Na sasa imekamilika. Ilitarajiwa kuanza safari yake siku tati zijazo.
Siki iliofata Kamaralzaman akuchukuwa maboga na kuatoa nyama zake kisha akayaanika. Yalipokauka akayakata tundi ndogo zinazowez kuingia vipande vya dhahabu.alifnya maandalizi haya kwa kujihami maana vipande vya dhahabu ingekuwa salama kuwa kwenye maboga watu watadhani ni mzingo wa maboga. Basi akatafuta boga kubwa na kuweka ule mkufu wa mkewake. Kisha akapanga na mzee wake na mambo yao. Siku hazikukawia hatimaye siku ya safari ikawadia. Siku hiyo usiku wa kuamkia siku hiyo mzee alikuwa naumwa. Kamaralzamani ilipofia asubuhi mabaharia walikuwa kumsisitiza kuwahi hivyo akawakabidhi mizigo yake watangulie nayo yeye atafata baadaye.
Lisaa limoja kabla ya safari mzee alizidiwa sana na kufariki. Kamaralzamani akawa bize na kuanda maiti ya mzee na kumzika pale shambani kwake. Anakuja kukumbuka kuhusu safari loo jahazi limeshaondoka inapata masaa mawili yaliopita. Nini afanye ni kusubiri tena mwaka ujao. Alibakia pale kibandani kwa mzee akiwa hana dhahabu wala mkufu wa mkewe. Alijuta sana lakini alijifariji kuwa hakuwa mgeni mbaya, alimuuguza mzee wake aliyemkaribu hadi akamzika.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela3 Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 645
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani
👉2 Kitau cha Fiqh
👉3 kitabu cha Simulizi
👉4 Kitabu cha Afya
👉5 Simulizi za Hadithi Audio
👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
kamaralzamani
HADITHI YA CAMARALZAMANI PRINCE PEKEE Inapata mwendo wa safari ya siku 4 kwa farasi kutokea nchi ya Peshia alikuwepo mfalme maarufu sana aliyefahamika kwa jina la Shahzaman. Soma Zaidi...
HADITHI YA NURDINI 02: mawaziri wa Mfalme
Alikuwepo mfalme aliyetambulika kwa jina la Muhammad Suleiman Azeyn. Soma Zaidi...
Ndoa ya utata ya Kamaralzaman
NDOA YA UTATA KISIWANI Mfalmee wa serendib alipouona msafara ule alivutiwa sana. Soma Zaidi...
HADITHI YA NURDINI 04: Mtihani wa Nurdini
Mama aliendelea kugomba sana kisha akamfungia binti ndani na kuweka walinznwa kiume, kisha akawaambia “haruhusiwi kuingia wala kutoka yeyote humu ndnai, hata mbwa Nurdini” neno mbwa lilimtoka tu mama Nurdini kisha akajilaumu kwa kumfana nisha ... Soma Zaidi...
TAHARUKI YA MFALME WA BAGHADANI
Soma Zaidi...
Taharuki na mwisho wa Kmaralzaman Feki
TAHARUKI Siku hiyo kamaralzamani Feki alikuwa ufukweni kukaguwa mendeleo, alikuwa yeye na mke mwenzie. Soma Zaidi...
ASUBUHI YA VARANGATI NA KAMARALZAMAN
VARANGATI ASUBUHI; Baada ya kugunduwa kuwa haikuwa ndoto kamaralzamani aliamini kuwa yule ndio mke ambaye baba yake alimchagulia. Soma Zaidi...
Kamaralzaman akiwa katika ndoto ya kweli
NDOTO AMA KWELI? Soma Zaidi...
HADITHI YA NURDINI 05: Rafiki wa Kweli
Mungu ashukuriwe sana, hatimaye miezi kadhaa ikapita bila ya waziri Masoud kugundua siri nzito. Soma Zaidi...
Ndoa ya kwanza ya kamaralzamani
NDOA YA HAMU Basi hali ikawa kama hivyo wawili hawa binamu na Kamaralzamani wakaanza kupanga njama ya kuweza kuondoka eneo lile kuelekea nchi za mbali kwa ajili ya kukutana na binti mfalme. Soma Zaidi...
KWENYE BOSTANI LA MFALME WA
KATIKA BOSTANI LA KIFALME BAGHADADBasi Nurdini na mke wake bila hata ya kujuwa wapi watafikia waliingia kwenye mashua na kuwasili Baghada wakati wa jioni. Soma Zaidi...
HADITHI YA NURDINI 03: Nurdini na Mtumwa
Siku ya tano Nurdini alipata taarifa kutoka kwa watu wake yaani wafanyakazi wa chumba chake kuwa kuna binti mgeni ameletwa ila ametengewa sehemu yake maalumu. Soma Zaidi...