image

HADITHI YA NURDINI 03: Mtumwa wa Gharama

Kama wasemavyo waliokula chumvi nyingi kuwa muomba mungu hachoki, basi waziri Faridi aliendelea kuomba Mungu hata siku moja akapata taarifa kuwa kuna watumwa wametokea nchi za Uajemi.

HADITHI YA NURDINI 03: Mtumwa wa Gharama

MTUMWA WA AJABU
Kama wasemavyo waliokula chumvi nyingi kuwa muomba mungu hachoki, basi waziri Faridi aliendelea kuomba Mungu hata siku moja akapata taarifa kuwa kuna watumwa wametokea nchi za Uajemi. Hapo waziri alitabasamu kwani alifahamu sasa anakwenda kupata alilolitaka. Kwani alitambuwa kuwa maeneo hayo ndipo watumwa wenye sifa hizo wanapatikana. Basi alifika akauta kuna mabinti wasiopungua 150. waziri aliwaangalia vyema sana huku akagunduwa kuwa kuna wwengine walikuwa wakitabasamu. Alitambuwa kuwa hawa hawafai maana wanadiriki kuuza tabasamu lao bila ya sababu.Kwa mara ya kwanza waziri akachaguwa walio wazuri kuliko wote. Aliamii kuwa mfalme angeanza kuangalia uzuri hata kabla ya kumthaminisha mtumwa wake. Katika mchujo huu akapata mabinti 21. kisha akaanza kuangalia sauti zao, nywele zao, nyusi na rangi za macho yao. Katika mchujo juu akabahatika kupata 12. kisha akaangalia vigezo vya elimu ya dini na dunia, hapa kabahatika kupata 5. kisha akaangalia hati za uanishi, na ufasaha wa kuzungumza hapa akabahatika kupata 3. sasa akaangalia kama wanafahamu kuburudisha hadhira na kumbrusisha mwanaume. Hapa ndipo akampata binti mmoja aliyefahamika kwa jina la An-neese.Hakika binti huyu alikuwa mzuri aliyepitiliza vigzo vya sultani. Maana urefu wake haukuwa wa kuchuchumia, hakuhitaji kupaka mafuta ndipo kulainisha ngozi yake. Siku zote alitumia vyakula asili kuweza kuweka mwili wake katika afya na urembo. Hakuwa ni mkwaro wa sauti, mach meupe makubwa, yaliyopambwa na nyuzi nyeysi sana zilizotengeneza umbo la mwezi mwandamo. Nywele nyefu na ngumu zenye afya. Alitambuwa kusoma hati za lugha kadhaa zilizokuwa zikitumia maeneo yale kama kiarabu, kihindi, kiroam (latini) na baaadhi ya lugha za hispatia na fursi.Waziri alikabidhi pesa palepale. Hapo muuzaji wa watumwa akampa ushauri waziri kuwa, “kwa ;leo usimpeleke kwa mfalme maana ametoka mbali,hivyo kwa uchovu alio nao, uzuri wake utajificha kidogo. Hivyo nakushauri, nenda naye kwanko kwa kiasi cha wiki na atakapozoea hali ya hewa uzurio wake utazidi mara dufu na hapo itakuwa vyema kumpeleka kwa mfalme. Waziri alikubwali ushauri huu japo kwa shingo upande akihofia mwanaye Nurdini.Waziri siku hiyo alikuwa akirurahia na kuamini sasa amempata wazri Masoud. Ila alihitaji iwe ni mshangao hivyo hakuthubuti kumwambia yeyote kuwa amempata mtumwa wa mfalme. Basi siku hiyo wazir wakati anakwenda na mtumwa wake kwake kwa ushauri wa muuzaji alimueleza kila kitu kuwa awe mbali sana na Nurdin maana ataweza kumuharibia kwani hajawahi kuacha sketi ya mtumwa wala mfanyakazi aliyeletwa nyumbani.yule binti mtumwa akaahidi kuwa hatakuwa na mahusiano na Nurdini kabisa. Basi alipofika nyumbani akamueleza mke wake kila kitu na kumtaka ampatie mtumwa yule kila anachohitaji ili baada ya wiki kupita ampeleke kwaMfalme.Binti mtumwa akatengewa eneo lake mwenyewe kwa ajili ya malazi na makazi. Mabinti wengine waliandaliwa kwa ajili ya kumpatia kila alichohitaji kuhakikisha kuwa anazea hali ya hewa na uzuri wake unaboreka. Hata hivyo baadhi ya vibinti vifanyakaz wa waziri walikuwa wakichukizwa na uwepowa mtumwa ambaye alikuwa ni kama malkia. Mtumwa ambaye alikuwa akifanyiwa kazi. Hakika mambo haya yalikuwa yakiwachokesha. Walikuwa wana kazi ya kumpikia, kumsugua anapokwenda kuoga, kumpamba na kumfanyia mambo mengine zaidi.Mambo yote haya yalikuwa yakitokea bila ya Nurdini kutambuwa uwepo wa binti yule. Mambo haya yalifanywa kwa siri ili aibu kubwa isijempata Waziri. Waziri aliamini kuwa kama atamueleza Nurdini kuwa asijekwenda kumuona yule binti basi huenda Nurdini ndio angekwenda kwa makusudi, kwa ajili ya kuridhisha udadisi wake. Basi mambo yakawa kama hivyo haimaye siku mbili zikaisha na ya tatu ikaingia. Uzri wa binti ulikuwa ukiongezeka kila siku zinapozidi. Mawazo ya kubadili maamuzi ya waziri yalikuwa yakimjia. Na hata me wake wivu ulianza kumkamata ijapokuwa hakuweza kudhihirisha.

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 254


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Kamaralzaman akiwa katika ndoto ya kweli
NDOTO AMA KWELI? Soma Zaidi...

HADITHI YA NURDINI 04: Mtihani wa Nurdini
Mama aliendelea kugomba sana kisha akamfungia binti ndani na kuweka walinznwa kiume, kisha akawaambia “haruhusiwi kuingia wala kutoka yeyote humu ndnai, hata mbwa Nurdini” neno mbwa lilimtoka tu mama Nurdini kisha akajilaumu kwa kumfana nisha ... Soma Zaidi...

Ndoa ya kwanza ya kamaralzamani
NDOA YA HAMU Basi hali ikawa kama hivyo wawili hawa binamu na Kamaralzamani wakaanza kupanga njama ya kuweza kuondoka eneo lile kuelekea nchi za mbali kwa ajili ya kukutana na binti mfalme. Soma Zaidi...

HADITHI YA NURDINI 03: Mtumwa wa Gharama
Kama wasemavyo waliokula chumvi nyingi kuwa muomba mungu hachoki, basi waziri Faridi aliendelea kuomba Mungu hata siku moja akapata taarifa kuwa kuna watumwa wametokea nchi za Uajemi. Soma Zaidi...

HADITHI YA NURDINI 05: Rafiki wa Kweli
Mungu ashukuriwe sana, hatimaye miezi kadhaa ikapita bila ya waziri Masoud kugundua siri nzito. Soma Zaidi...

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA KITABU CHA TATU: HADITHI YA NURDINI
Soma Zaidi...

HATMA YA NURDINI NA NCHI YAKE
Hadithi za alif lela u lela kitabu cha tatu sehemu ya 9 Soma Zaidi...

Taharuki na mwisho wa Kmaralzaman Feki
TAHARUKI Siku hiyo kamaralzamani Feki alikuwa ufukweni kukaguwa mendeleo, alikuwa yeye na mke mwenzie. Soma Zaidi...

kamaralzamani
HADITHI YA CAMARALZAMANI PRINCE PEKEE Inapata mwendo wa safari ya siku 4 kwa farasi kutokea nchi ya Peshia alikuwepo mfalme maarufu sana aliyefahamika kwa jina la Shahzaman. Soma Zaidi...

Ndoa ya utata ya Kamaralzaman
NDOA YA UTATA KISIWANI Mfalmee wa serendib alipouona msafara ule alivutiwa sana. Soma Zaidi...

HADITHI YA NURDINI 03: Nurdini na Mtumwa
Siku ya tano Nurdini alipata taarifa kutoka kwa watu wake yaani wafanyakazi wa chumba chake kuwa kuna binti mgeni ameletwa ila ametengewa sehemu yake maalumu. Soma Zaidi...

NURDINI ANARUDI KWAO NA BARUA YA MFALME WA BAGHADAD
Hadithi za Alif lela u lela kitabu cha tatu sehemu ya nane Soma Zaidi...