Kamaralzaman arudi kwao

SAFARI YA KURUDI NYUMBANI Kamaralzamani siku hiyo akamfuata baba mkwe wake na kmueleza ukweli wa mambo na kuwa yeye si mganga.

Kamaralzaman arudi kwao

SAFARI YA KURUDI NYUMBANI
Kamaralzamani siku hiyo akamfuata baba mkwe wake na kmueleza ukweli wa mambo na kuwa yeye si mganga. Historia hii ilibidi iandikwe kwa wino wa dhahabu na ihifadhiwe kwenye kumbukumbu za kifalme. Mfalme alifurahi sana baada y akusikia kuwa Kamaralzamani alikuwa ni mtoto wa mfalme wa nchi ya Peshia. Basi baada ya mazungumzo Kamaralzamani akaomba apewe ruhusa ya kwenda nyumbani kwenda kuwaona wazazi. Hakukuwa na kipingamizi kwa upande wa sultani hivyo akawakubalia waende ila alipenda zaidi warudi wote kwa pamoja.


Safari ikaanza kutoka nchi za mbali kuelekea Peshia. Wakiwa kwenye gaei la kuendeshwa na farasi wawili, kijumba kidogo kilichobeba watu wawili kilikuwa kikikokotwa taratibu. Kwenye kidole kimoja kati ya kila mmoja kuna pete yenye kupendeza sana. Shingoni mwa binti sultani kulikuwa na mkufu wenye cheni ya dhahabu lakini ua kifurushi kinning;inia. Unaweza kusema ni kijiwe chenye thamani sana lakini ukweli wa mambo kuna siri nzito ndani yake. Wawili hawa walikwenda hata siku inaisha wakalala na siku inayofaa ikaisha wakalala tena. Kutoka kwao mpaja Peshia wataweza kuchukuwa mwendowa mwezi mmoja kutokana na mwendo wao.


Siku ya 6 ya safari walipumzika chini ya mti wakati wa jioni. Kamaralzamani akiwa anamsifia mewe aliyelala uzuri wake. Ghafla akataka kujuwa kuna nini kwenye kile kifurushi kilicho kwenye shingo ya binti sultani. Alipomvua kwa upole sasa wakati anakiangalia akaja panya na kukibeba akizani ni nyama ama chakula. Panya yule alitoka nje ya hema na kuelekea msituni. Kamaralzamani akiwa anamfarilia panya yule ghafla panya akabebwa na bund. Kamaralzamani akawa sasa anamkimbiza bundi ambaye alimeza kale kafurushi alipokuwa anajaribu kumla panya. Kamaralzamani akiwa anamkimbiza pundi ghafla budi yule aling'atwa na nyoka aliwa juu ya mti. Alipoangauka alibebwa na kunguru mmoja mkubwa sana. Ukubwa wa knguru huyu si wa kawaida.


Bundi alianza kuliwa. Kamaralzamani hakuweza kufanya kitu maana alipomchukuwa akakwea ne juu sana ya mtu. Sasa Kamaralzamani akasubiri chini ya mti eidha mkufu uanguke ama atakaposhiba ataweza kumpata. Kwa kuwa kunguru anapeda kula utumbo kuliko nyama, aliweza kuumeza mkufu na kuanguasha chini mzoga mtupu. Sasa Kamaralzamani akawa anamkimbiza kunguru. Usiku ukaingia wote wakalala kunguru juu ya mti na kamaralzamani chini. Aubuhi kamaralzamani akaanza kumtafuta tena na kuendelea kumkimbiza. Hadi alipokata tamaa akakumbuka kumbe alikuwa akisafiri na binti sultani. Loo hakuwa na la kufanya na hata njia aliisahau.


Loo kamaralzamani yupo matatizoni sasa. Akaanza japo kutafuta pa kutokea baada ya mwendo wa siku moja na nusu mcha na akakuta kuna kijiji karibu. Akaona kuna nyumba ipo pale. Akapiga hodi na kuanza kujieleza alipotoka na anapokwenda. Yule mzee aliyemlkuta kwenye kibanda kle akamueleza kuwa kutoka hapa mpaka huko unakokusema ni mwendo wa mwezi, na hakuna njia zaidi ya kupitia baharini. Na hapa tulipo dau la kwenda huko kuja kila baada ya mwaka mmoja. Hivyo kwenda huko usubiri mpaka mwaka uingi emaana dau limeondoka yapata siku tatu nyuma.


Kwa hali hii kamaralzamani alianza kuishi kwa huyu mzee maisha mapya. Kwa upande wa binti sultani aliweza kumsubiri kamaralzamani pela kwa siku mbili. Aliogunduwa kuwa mumewe hayupo hakutaka watu waelewe siri ile. Basi kwa kuwa walikuwa wakifanana aliachukuwa nguo za mumewe na kuzivaa. Alikuwa kama vile yeye ndie Kamaralzammani. Safari ikaanza. Kale kafurushi kalikuwa ni hirizi aliyopewa na mmoja kati ya waganga na akamwambia ukikapoteza kahirizi haka ujuwe hutoweza kuishi maisha ya furaha kamwe. Na hii ndio sababu ya kuwa alikuwa akikavaa kahirizi kale huku watu wakajuwa ni mkufu. Sasa kahirizi hakapo tena na mumewe hauypo tena wapi atapata furaha?


Walipofika kisiwa cha Serendib wakaomba kuvushwa. Ilikuwa ni lazima uruhusiwe na mfalme ama waziri ama kwa ushahidi maalumu ndio utoke nje ya kisiwa hiki. Hakuna njia ya mkato ila mpaka ukatishe kisiwa hii. Siku hiyo mfalme wa kisiwa hiki alikuwa akitembea maeneo ya baharini. Mfalme huyu alikuwa naye hana mtoto wa kiume na ana wa kike mmoja tu. Siku zote alikuwa akimtaka mwanae aolewe lakini mtoto hakutaka kuolewa. Mtoto stori yake ni kama wenzie alitaka mchumba ambaye atakuwa anampenda yeye na si kwa sababu ya madaraka ya baba. Hivyo alikuwa kila akiletewa mchumba hakubali. Naye ikafikia hatuwa ya kufungiwa ndani.

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 137

Post zifazofanana:-

SAFARI YA MAJIBU JUU YA MASWALI MAWILI
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA MAJIBU JUU YA MASWALI MAWILI. Soma Zaidi...

KIAPO CHA SULTANI
Download kitabu Hiki Bofya hapa KIAPO CHA SULTANI. Soma Zaidi...

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA: KIFO CHA DAMU
Soma Zaidi...

HADITHI YA MZEE WA TATU NA MBWA
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MZEE WA TATU NA MBWA WAKE MWEKUNDU Kama nilivyotangulia kusema , huyu ni mkewangu wa ndoa tulioishi pamoja kwa muda wa miaka zaidi ya kuni na tano sasa. Soma Zaidi...

Watu wa Mji Waliomuua Muislamu kwa Kuwa Amewasadikisha Wajumbe wa Allah(s.w)
Katika Suratul Yassin Allah(s. Soma Zaidi...

HADITHI YA CHONGO WA TATU MTOTO WA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA CHONGO WA TATU MTOTO WA MFALME Mimi ni mtoto wa mfalme kama nilivyotangulia kusema na ni mtoto wa kipekee kwa baba na mama. Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 25
26. Soma Zaidi...

MSHENGA WA ALADINI MBELE YA MFALME KWA MARA YA PILI
Soma Zaidi...

SHAIRI -CHUKI
Soma Zaidi...

DARSA ZA DINI YA KIISLAMU KAMA QURAN, FIQH, SIRA, AFYA, TAJWID NA TAFSIR ZA QURAN
Soma Zaidi...

HADITHI YA ALADINI NA TAA YA MSHUMAA WA AJABU
Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 17
5. Soma Zaidi...