HATMA YA NURDINI NA NCHI YAKE

Hadithi za alif lela u lela kitabu cha tatu sehemu ya 9

HATMA YA NURDINI NA NCHI YAKE

HATMA YA NURDINI NCHINI KWAKE.
Baada ya mfalme kuondoka pale ndani zilipita siku tatu bila hata kuongea na mte yeyote yule. Jambo hili lilileta taharuki kubwa sana. Hatimaye siku ya nne na mapema mfalme akaonekana kwenye baraza la asubuhi. Akiwana barua yake mkononi alionekana kuhoji baadhi ya walinzi. Alikuwa akihoji ni kitu gani kilitokea kwa Nurdini na wapi alipo. Majibu aliyopatiwa huwenda hayakumfurahisha kwa sababu uso wake haukuonekana kufurahia kabisa. Moja kwa moja alikwenda kuketi kwenye kiti chake cha kifalme. Kilikuwa ni kiti kirefu chenye vishikizo vya dhahabu, vilalio vya hariri iliyo laini vyema. Ijapokuwa kiti kilikuwa ni kizuri na lakini mfamle hakuwa na raha kabisa."nimepokea barua kutoka kwa Haru Rashid wa Baghadad ananitaka nijivuwe madaraka kwa amani ili nimkabidhi Nurdini kijana wa hayati waziri wangu mzee Farid". Yalikuwa ni maneno ya mfalme yaliyoonekana kumstaajabisha kila mtu aliyekuwepo pale ndani ya ukumbi ule. Hapo zamani mfalme wa nchi hii hupata uthibitisho wa kuendelea na madaraka ama kuyawacha kutoka Baghadad.Ni kuwa wakati fulani nchi hii ilivamiwa na majeshi kutoka meneo ya India. Hivyo mfalme wa Baghadadi akiwa anatokea Maka kuhiji aliweza kuokoa nchi hii dhidi ya jeshi la wahindi. Tokea hapo wakaweka mkataba kuwa mchi hii mfalme hatakuwa halali mfapa athibitishwe na mfalme Harun Rashid wa Baghdad. Mkataba huu utaendelea kuwa hai mpaka pale ambapo Mfalme Harun Rashid atakapofariki.Sasa kabla ya mfalme huyu walisha pita wafalme watatu nyuma. Mzee Farid pia alikuwa katika orodha ya kuwa Mfalme lakini alikatwa kutokana na upole wake. Hivyo kwa mkataba walioweka mfalme wa Baghadad ataweza kumuachisha madaraka mfalme wa nchi hiyo endapo hataridhishwa na utendaji wake kama kunyanyasa wananchi ama kupuuza majukumu yake. Hivyo basi kwa barua aliyoleta Nurdini inamaana mfalme huyu anatakiwa ajivue na Nurdini awe mfalme mpya.Baada ya majadiliano marefu sana mawaziri walionekana kutokukubaliana na maamuzi hayo. Nusu walikuwa wanataka mfalme wao aendelee, kiongozi wa kundi hili alikuwa ni Masoud. Na nusu nyingine ilitaka mfalme akubali kuachia madaraka na kiongozi wa kudni hili walikuwa na rafiki na jamaa wa mzee Farid. Mwisho Masoud alitowa hitimisho kwa kusema "kwanza barua yenyewe haipo sahihi, ilipaswa iletwe na waziri ama kiongozi yeyote kutoka serikalini kwake, sasa haiwezekani Nurdini alete barua hii, mimi naona nurdini ni muongo, ameghushi barua hii hivyo akamatwe kisha auliwe"Yalikuwa ni maamuzi magumu lakini mfalme alikubaliana nayo. Mfalnme akaruhusu Nurdini akamatwe atiwe kwenye gereza lililo madhubuti sana . swala la kumuuwa hakutaka lifanyike mpaka ainarishe ulinzi kwanza maana kunaweza kukatokea vita kutokana kupuuza barua ile endapo itakuwa ni ya kweli. Masoud ijapokuwa alisisitiza nurdini auliwe lakini hakuwa na pingamizi kwa maamuzi ya mfalme wake.Siku arobaini sasa zimepita toka Nurdini aondoke baghadad. Siku hiyo mfalme alipita kwenye nyumba ambapo mke wa Nurdjini yupo. Alimkuta anaimba mashairi ambayo yalikuwa ni kuilaumu nafsi yake kwa kumuachia mune wake kipenzi kuondoka peke yake. Mfalme alisikitishwa sana pia akaijona yupo makosani. Ikabidi aitishe mkutano kidogo kuhusu barua yake aliyoituma. Katika mkutano wakakubaliana liondoke jeshi la watu 3000 kajini lisiibgie nchini likae nje ya mji ama mipakani, kisha waziri wawili akiwepo Jafari waingie kwa mfalme wa nchi ile ili kufuatilia barua ya mfalme Harun rashid. Endapo mfalme ataipinga jeshi linatakiwa limtoe kwa nguvu.Katika msafara huu mke wa Nurdini pia likuwepo. Wakatoka kuelekea huko. Siku ya tatu wanaingin, kumbe na kule mfalme aliitaka kumuuwa Nurdini. Taarifa za jeshi la wa tu 3000 zikamfikia mfalme na wakati huo mawaziri wa mfalme harun rashid wanaingia. Mfalme Muhammad ibn Suleiman hakuwa na njia nyingine ya kuema barua ni feki. Hivyo ikabidi akabidhi madaraka kwa amani kabisa kwa Nurdini.Kutoka hapo Nurdini akawa ndio mfalme mpya wa nchi hii. Mahusiano mazuri ya nchi mbili hizi yalitanuka na kuchanua vyema. Wananchi waliweza kusafiri na kushirikiana kibiashara kati ya nchi mbili hizi. Uongozi wa Nurdini ulipenda sana kwani hakuweza kuwabaguwa wanyonge. Kwa masaada wa mke wake aliyekuwa na akili na busara kubwa Nurdini alibadilika sana na kutoka Nurdini mzembe kuwa Nurdini bora sana.
Huu ndio mwisho wa hadithi hii. Ahsante sana kwa kuwa mvumilivu tukutane hadithi ya Badrudini, bila sjaka utaipenda zaidi kuiko hii.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 206


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

HADITHI ZA SINBAD
Soma Zaidi...

KUTOKA NYANI MPAKA KUWA CHONGO
Download kitabu Hiki Bofya hapa KUTOKA NYANI MPAKA KUWA CHONGO. Soma Zaidi...

HADITHI YA SAMAKI WA RANGI NNE
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA SAMAKI WA RANGI NNE. Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 17
5. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII YUSUFU(A.S.): Ndoto ya nabii Yusufu
Mtume Yusufu(a. Soma Zaidi...

Kitabu Cha Kiapo Cha Mfalme
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

HADITHI YA MZEE WA TATU NA MBWA
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MZEE WA TATU NA MBWA WAKE MWEKUNDU Kama nilivyotangulia kusema , huyu ni mkewangu wa ndoa tulioishi pamoja kwa muda wa miaka zaidi ya kuni na tano sasa. Soma Zaidi...

hatima ya kinyozi
Soma Zaidi...

ALIF LELA U LELA: UTANGULIZI
ALIF LELA U LELA. Soma Zaidi...

HATMA YA NURDINI NA NCHI YAKE
Hadithi za alif lela u lela kitabu cha tatu sehemu ya 9 Soma Zaidi...

ndege wafikishe
NDEGE WAFIKISHE Hebu paa ndege paa, ufise habari hizi, Ufike wanako kaa, imi kufika siwezi, Paa bila kuzubaa, upae anga iwazi Naujumbe huu twaa, tekeleza hiikazi, Kawa pe utawafaa, wata po fa nyia kazi Kwa watakaokataa, usifanye lazimizi, Wambie lama Soma Zaidi...

Utajiri wa Baba na kifo chake
UTAJIRI WA BABA NA KIFO CHAKE. Soma Zaidi...