MAWAZIRI WA MFALME:
Alikuwepo mfalme aliyetambulika kwa jina la Muhammad Suleiman Azeyn. Mfalme huyu alikuwa ana mawaziri wakuu wawili. Hakika hili halikuwa ni jambo la kawaida luwa na mawaziri wakuu wawili lakini kwa mfalme huyu alipendelea kweli. Alifanya hiv kusudi ili kuinua chachu ya maendeleo maana kila waziri alikuwa akishindana kufanya mambo kwa ajili ya kupata sifa na heshima kwa mfalme na nchi. Ijapokuwa mawaziri hawa waliwekwa wawe na ushindani lakini mambo yalikuwa tofauti kidogo kwa Masoud mmoja kati ya hawa wawili. Na mwingine alitambulika kwa jina la Faridi.Faridi alikuwa akisimama upande wa kuliani mwa Mfalme na masoud alikuwa akiimama upande wa kushoto. Masoudi siku zote alikuwa akifanya mabo kwa ajili kutaka sifa kwa mfalme wake. Kwa lugha nyingine alikuwa ni mpambe na ni shushushu la mfalme. Wakati Faridi alikuwa akifanya mabo kwa kwa masilahi ya nchi na maendeleo ya watu wote. Basi wananchi walimpenda sana Faridi na kumchukia waziri Masoudi. Jambo hili hata masoudi mwenyewe alilitambua, hata mfalme alitambua pia. Hata hivyo kama ilivyo moyo hupenda kwenye maslahi, mfalme alikuwa akimpeda pia Faridi lakini hakuweza kudhihirisha hilo.Basi ijapokuwa mawaziri hawa walikuwa na ugomvi wa moyoni hasa bwana Masoud, lakini hata siku moja hawajawahi kugombana. Hakika mfalme alikuwa akilipenda sana jambo hili. Alikuwa akiwaalika kula pamoja hasa nyakati za usiku. Waziri Faridi alikuwa na kijana wake aliyetambulika kwa jina la Nurdin. Nurdini alikuwa ni kijana mtanashati mwenye sauti nzuri na sura ya kupendeza. Kijana huyu alisifika sana kwa utundu na ukorofi. Hakuwa akipigana na mtu wala kugombana na mtu, ila hakuwahi kumuacha mtumwa, mfanyakazi wala mtoto wa kike yeyote atakayekwenya kwao bila ya kufanya naye uchafu. Tabia hii ilikuwa ikimuhuzunisha sana bwana Faridi maana alimshauri sana mwanaye aoe lakini alikataa katakata na kudai kuwa yeye bado mdogo.Basi mambo yakawa kama hivyo na siku zikaenda. Ssiku moja mfalme alikuwa na mawaziri wake hawa wawili wakiwa wanazungumza hapa na pale. Mfalme akasema “hivi kuna uwezekano wa kuweza kumpata mtumwa wa kike ambaye atakuwa ni msomi wa dini na dunia, pia awe anajuwa taaluma ya kuburudisha wanaume na hadhira, pia awe ni mzuri sana wa sura, umbo, sauti na tabia. Awe na ngozi nyororo, na nyusi nyeusi sana zilizo pamba macho meupe makubwa haya yote yaambatane na sifa kuwa anunuliwe kwa thamani ya vipande 100 tu vya dhahabu” hili lilikuwa ni swali la mfalme wakati anachomekea na kunogesha mada. Mawaziri hawa siku zote walikuwa ni wenye kupingana. Hili hata mfalme alilijuwa na alichomekea maada hiyo kusudi.Kama kawaida waungwana hawa wawili wakaanza kubishana bwana Faridi akasema ndio inawezekana bila wasi ila si kwa maramoja. Bwana Masoud akasema haiwezekani kabisa. Sifa hizo ulizozitaja Haziwezi kupatikana kwa mtumwa hata kwa mara moja. Na hata kama angelikuwa ni mtumwa wangu basi ningelimuacha huru. Kwa hakika ninapibgwa vikali kauli ya bwana Faridi. Hapo mzozo uliendelea kuwa mkubwa sana na kila mmoja alionekana kuwa na hoja za msingi. Mfalme akaamuwa kumaliza hoja kwa kumtupia mzigo bwana Faridi.Mfalme akasema “nimeridhishwa na hoja zako ewe bwana Faridi na hoja za Bwana Masoudi pia ni za ukweli, sasa naamuwa kuwa nitakupatia vipande 1000 vya dhahabu unitafutie huyo mtumwa. Na ewe bwana Masoud utathibitisha sifa nilizozitaja pindi atakapopatikana huyo mtumwa. Basi hapo mzozo ukaishia, wazee hawa watatu wakamaliza kikao chao na kutawanyika. Moyoni bwana Masoud aliwaza kuwa hakika Faridi hataweza kumpata huyo mtumwa na hata akimpata mimi ndiye nitathibitisha sifa kama zipo, naweza kumfanyia ulaghai mbele ya Mfalme. Kwa upande wa bwana Faridi yeye alitaka kuwaonyesha walimwengu kuwa hata watumwa wasidharauliwe kwani wanaweza kuwa na elimu, na faida kubwa ambazo hata mtu muungwana asiwe nazo.Tunaweza kusema kuwa bwana faridi aliamuwa wazo ambalo lilikuwa na faida kwa umma na si kwa faida yakwake pekeyake. Lakini bwana Masoudi siku zote alijifikiria yeye mwenyewe na namna gani ataweza kujisafisha mbele ya mfalme. Kwa sababu hii viongozi wengi wa serikali walmchukia bwana Masoudi. Basi waziri Faridi alianza kutembelea masoko yote ya watumwa na kuweka oda kuwa asiuzwe mtumwa yeyote wa kike mpaka amuone kwanza. Mambo yalikuwa hivyo ikawa kila watumwa wanapoletwa wakike hawauwi mpaka bwana faridi athibitishe.