image

HADITHI YA NURDINI 05: Rafiki wa Kweli

Mungu ashukuriwe sana, hatimaye miezi kadhaa ikapita bila ya waziri Masoud kugundua siri nzito.

HADITHI YA NURDINI 05: Rafiki wa Kweli

RAFIKI WA KWELI




Mungu ashukuriwe sana, hatimaye miezi kadhaa ikapita bila ya waziri Masoud kugundua siri nzito. Mfalme aliendelea kumkumbusha waziri Faridi hatimaye akasahau kabisa lile swala. Miezi saba ikapita. Maradhi ya ajabu yakampata waziri faridi na akafariki dunia. Baada ya taratibu za mazishi kukamilika haikupita hata miezi mitatu mama Nurdini akafariki dunia. Loo !!!!! yalikuwa ni maonzi juu ya majonzi kwa Nurdini ambaye siku zote alitegemea baba na mama. Kwa kweli kizuri hata hakidumu kwa muda mrefu. Ukweli ni kuwa mzee Faridi aliishi mika mingi na kula chumvi nyingi. Alifariki akiwa na miaka 81. je kizuri hakidumu kweli?



Nurdini sasa akiwa yaima, akawa ndiye mrithi wa pekee wa mali za baba. Hakuweza kuwafahamu ndugu za baba yake hatammoja. Maisha yaliendelea, aliendelea kula mali za baba bila kuzalisha. Aliendelea kufurahi na mkewe kipenzi. Marafiki zake waliendelea kula na kusaza. Waliendelea kutanua na mengineyo kibao. Kama ilivyo mali bila daftari huisha bila habari, hatimaye mali ya Nurdini ikaendelea kupungua kwa kasi sana. Kweli bandubandu hualiza gogo. Baada ya miezi kadhaa pesa zilimuishia. Nurdini akaanza kuuza Watumwa wote apate pesa ya kutumi,.



Mambo hayakumnyookea, marafiki wakakata mguu kabisa kuonana naye. Akaanza kuuza vitu vya ndani hata vikamwishia na kubakiwa na kitanda na vitu vichavche kwa ajili ya kupikia. Mwishowe akaamuwa kwenda kumuuza mewe ambaye alikuwaga ni mtumwa hapo mwanzo. Hii ni kutokana na ushauri wa mkewe kumuonea huruma mumewe hivyo akamwambia amuuze apate pesa, huwenda akazalisha pesa ya kumkomboa na wakakutana mbele ya safari. Nurdini alimpenda sana mkewe lakin aliamini kuwa ushauri huu ni mzuri.



Alimchukuwa mkewe na kwenda kumuuza kwa pesa ile ambayo baba yake alimnunulia. Waziri Masoud alimuona Nurdini akimuuza mtumwa ambaye anafanana sifa na yule aliyekuwa akitafutwa na baba ake. Hapo aliamini kuwa baba yake alimpatia mwanaye mtumwa wa mfalme. Masoud aliweka oda ya kumnunua yule mtumwa, lakini Nurdini alipotambuwa hili akagoma kumuuza maana aliamini kwa ukorofi wa Masoud asingeweza kumpatia pesa. Ikabakia ugomvi kati ya Masoud na Nurdini. Nurdini wakati huo akamchukuwa mkewe na kumtia kwenye farasi tayari kuondoka mbio.



Masoud alitaka kutumia uwaziri wake lakini alishindwa, kwani Nurdini alikuwa ni mjeuri. Masoud akamvuta shati Nurdini na akaanguka chini yeye na mkewe, tena kwenye matope. Nurdini alimpiga ngumi waziri, ngumi iliyomtoa damu. Kisha akatimua mbio. Waziri bila ya kujifuta damu akaenda kwa mfalme kushitaki. Hiko akaeleza wazi kila ambacho kilitokea kwa yule mtumwa aliyemtaka kuwa bwana faridi alimuozesha mwanaye na sasa mtoto anataka kumuuza.



Mfalme alikasirika sana, na akatangaza aletewe Nurdini popote alipo. Jeshi kubwa liliamuriwa likamchukuwe Nurdini. Katika jeshi lile alikuwepo kijana mmoja aliyekuwa na ukaribu sana na baba Nurdini, hivyo akaenda mbio kwa Nurdini na kumtaarifu akimbie haraka sana. Nurdini hakuamini anachoambiwa ila akakubali kuamini, hivyo akajiandaa kuondoka yeye na mkewe. Yule askari akampatia nurdini kiasi cha pesa alicho nacho na kuwafanyia mipango ya kupata jahazi dogo la kuondokea kwasiri. Mambo haya yalifanyika kwa siri sana na haikuchukuwa muda Nurdini akaondoka, na mkewe kuelekea Baghadad.







           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 420


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Ndoa ya utata ya Kamaralzaman
NDOA YA UTATA KISIWANI Mfalmee wa serendib alipouona msafara ule alivutiwa sana. Soma Zaidi...

HADITHI YA NURDINI 05: Rafiki wa Kweli
Mungu ashukuriwe sana, hatimaye miezi kadhaa ikapita bila ya waziri Masoud kugundua siri nzito. Soma Zaidi...

HATMA YA NURDINI NA NCHI YAKE
Hadithi za alif lela u lela kitabu cha tatu sehemu ya 9 Soma Zaidi...

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA KITABU CHA TATU: HADITHI YA NURDINI
Soma Zaidi...

Taharuki na mwisho wa Kmaralzaman Feki
TAHARUKI Siku hiyo kamaralzamani Feki alikuwa ufukweni kukaguwa mendeleo, alikuwa yeye na mke mwenzie. Soma Zaidi...

ASUBUHI YA VARANGATI NA KAMARALZAMAN
VARANGATI ASUBUHI; Baada ya kugunduwa kuwa haikuwa ndoto kamaralzamani aliamini kuwa yule ndio mke ambaye baba yake alimchagulia. Soma Zaidi...

Kamaralzaman akiwa katika ndoto ya kweli
NDOTO AMA KWELI? Soma Zaidi...

TAHARUKI YA MFALME WA BAGHADANI
Soma Zaidi...

HADITHI YA NURDINI 03: Mtumwa wa Gharama
Kama wasemavyo waliokula chumvi nyingi kuwa muomba mungu hachoki, basi waziri Faridi aliendelea kuomba Mungu hata siku moja akapata taarifa kuwa kuna watumwa wametokea nchi za Uajemi. Soma Zaidi...

KWENYE BOSTANI LA MFALME WA
KATIKA BOSTANI LA KIFALME BAGHADADBasi Nurdini na mke wake bila hata ya kujuwa wapi watafikia waliingia kwenye mashua na kuwasili Baghada wakati wa jioni. Soma Zaidi...

HADITHI YA NURDINI 03: Nurdini na Mtumwa
Siku ya tano Nurdini alipata taarifa kutoka kwa watu wake yaani wafanyakazi wa chumba chake kuwa kuna binti mgeni ameletwa ila ametengewa sehemu yake maalumu. Soma Zaidi...

kamaralzamani
HADITHI YA CAMARALZAMANI PRINCE PEKEE Inapata mwendo wa safari ya siku 4 kwa farasi kutokea nchi ya Peshia alikuwepo mfalme maarufu sana aliyefahamika kwa jina la Shahzaman. Soma Zaidi...